Kodi zinatokana na Rasimali zifufue na kanzisha viwanda vipya

chachu

Senior Member
May 17, 2011
141
195
Uchumi wa nchi unaweza kuwa mzuri tu tukifanya mapinduzi ya viwanda. Madini na rasilimali nyingine zitaisha na tutabaki
 
iMind

JF-Expert Member
Mar 27, 2011
2,181
2,000
Uchumi wa nchi unaweza kuwa mzuri tu tukifanya mapinduzi ya viwanda. Madini na rasilimali nyingine zitaisha na tutabaki
Ndugu yangu, serikali haiwezi kuanzisha viwanda. Hata mimi sishauri serikalli kuanzisha viwanda. Pia sera ya ccm ni kuwa na uchumi ambao unaendeshwa na kumilikiwa na sekta binafsi.

Ndo maana viwanda viliuzwa. Binafsi nashangaa kuona watu tena wakati mwingine hata wabunge wa ccm wakishauri serikali kufufua viwanda au kuanzisha viwanda vipya.

Mawazo kama haya siyo tu yataturudisha huko tulikotoka lakini vile ville hayaitakii mema watanzania.

Amin usiamin serikali yoyote ya Tanzania haitaweza kuanzisha shirika likawa productive

Unaona TANESCO unaona TTCL unaona TRL, how can you suggest serikali kuanzisha mashirika mengine wakati Nyerere mwenyewe yalimshinda.

Tunachotakiwa kufanya ni kushawishi wawekezaji wa nje na ndani kuanzisha viwanda
Serikali yaweza kununu hisa katika viwanda hivyo kama ambavyo imekua ikifanya.

Tatizo letu hatupendi wawekezaji, tunawaona kama wezi. Lakini hiyo ndo njia pekee ya kuwa na viwanda
 
chachu

Senior Member
May 17, 2011
141
195
Kodi tunazozipata kutokana na rasilimali kama madini zingefanya mapinduzi ya viwanda kwanza tungenyanyua uchumi wetu, kodi inayotoka kwenye hivyo viwanda ndio ikajenge hizo barabara na miradi mingine. pili tungepunguza tatizo la ajira kwa kiasi kikubwa. Kodi tunazopata zinajenga barabara na miradi mingine Rasilimali zitaisha tutabaki na nini cha kuinua uchumi pamoja na ajira tusipotazama na kuona mbali kwa sasa....! Tax relief ingekuwa sawa kama wangepewa wawekezaji wanaojenga viwanda kwa sababu hata wakiondoka tutabaki navyo. Tax relief kwa mwekezaji anaechuma rasilimali na badae kukuachia mashimo/mahandaki kumpa hiyo relief ni mtazamo uliokuwa hasi na si msaada kwa taifa.
Ni kweli tulishindwa na viwanda vilikufa, tunaweza kuwa na fikra nyingine za kuvianzisha na kufufua vilivyokufa halafu tukavitafutia wawekezaji na serikali ikawa mwanahisa. Serikali ikaweka mikakati ya kilimo kitakachotoa malighafi na mambo mengine. Leo hii Kenya wananua matunda kwetu wanakwenda kuyaprocess wanaleta kutuuzia. Tanzania, Serikali yangu sasa ni wakati wa kuwa sera na siasa zenye tija kwenye taifa letu. Yote yanawezekana. Tuache kulalamika kila mwenye nguvu na afanye kazi.

Nawakilisha.

[NQUOTE=iMind;5121010]Ndugu yangu, serikali haiwezi kuanzisha viwanda. Hata mimi sishauri serikalli kuanzisha viwanda. Pia sera ya ccm ni kuwa na uchumi ambao unaendeshwa na kumilikiwa na sekta binafsi.

Ndo maana viwanda viliuzwa. Binafsi nashangaa kuona watu tena wakati mwingine hata wabunge wa ccm wakishauri serikali kufufua viwanda au kuanzisha viwanda vipya.

Mawazo kama haya siyo tu yataturudisha huko tulikotoka lakini vile ville hayaitakii mema watanzania.

Amin usiamin serikali yoyote ya Tanzania haitaweza kuanzisha shirika likawa productive

Unaona TANESCO unaona TTCL unaona TRL, how can you suggest serikali kuanzisha mashirika mengine wakati Nyerere mwenyewe yalimshinda.

Tunachotakiwa kufanya ni kushawishi wawekezaji wa nje na ndani kuanzisha viwanda
Serikali yaweza kununu hisa katika viwanda hivyo kama ambavyo imekua ikifanya.

Tatizo letu hatupendi wawekezaji, tunawaona kama wezi. Lakini hiyo ndo njia pekee ya kuwa na viwanda[/QUOTE]
 
FRANCIS DA DON

JF-Expert Member
Sep 4, 2013
20,241
2,000
Ni dhahiri hakuna nchi itakayo endelea bila uwepo wa viwanda (uzalishaji). Viwanda vingi vya serikali vilikufa kwa sababu zinazofahamika na kila mtu, ila ninachojiuliza, hakuna uwezekano wowote ule wa kuondoa vile vizingiti vinavyofanya viwanda hivi vife ili walau watu wapate ajira kwenye kiwanda angalau cha baiskeli tu?! mfano tuhakikishe takataka zinazotoka nje zinabamizwa kodi kubwa ili tusiue viwanda vya ndani, its that simple..
 
Chona

JF-Expert Member
Mar 8, 2010
517
500

Heading yako na maelezo yako haviendani!!!:juggle:
Msoma heading anaweza dhani Kiwanda kimefufuliwa tayari, na hivyo kutaka kujua zaidi mathalani strategy gani zimetumika, ajira zitakazo tolewa kiwango cha uzalishaji nakadha wa kadha. Uandishi wa aina hii hauvumiliki.
 
Mshomba

JF-Expert Member
Apr 7, 2013
1,642
2,000
Urafiki textile,sungura,kile cha matairi kule arusha na vinginevyo vingi endapo vingefufuliwa na kuanza uzalishaji hakika kungepunguza idadi kubwa ya tatizo la ajira hapa nchini
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom