Kodi za ardhi ziwe na viwango sawa nchi nzima kama kodi za majengo

mpimamstaafu

JF-Expert Member
Jul 18, 2018
4,445
4,704
Wizara ya Ardhi kama inataka kodi za ardhi zilipwe bila kusumbuana na kuwapeleka wananchi mahakamani ni lazima ifanye marekebisho makubwa katika viwango na namna ya ulipaji wake.Napendekeza iwe kama ifuatavyo:
1.Kodi zilipwe kwa njia ya Mtandao kila Halmashauri iwe na code namba zake.
2.Kodi zifanane kwa viwanja vyote vya
-ujazo mkubwa(HD) kwa mfano Sh.5,000/= kwa mwaka
-ujazo wa kati(MD) kwa mfano Sh.10,000/=kwa mwaka
-ujazo mdogo(LD)kwa mfano Sh.15,000/= kwa mwaka
3.Kusiwe na adhabu kwa waliochelewa kulipa
4.Kodi ziruhusiwe kulipwa kila baada ya miezi 4
5.Watu wengi hawaendi kwenye ofisi za Ardhi kwani wanasumbuliwa na watendaji wa ardhi na kubambikiziwa kodi)
*Kitendo cha kodi za Majengo kuwa sh.10,000/= na sh 50,000 /=kwa nyumba ya kawaida na ghorofa bila kujali thamani ya nyumba (valuation)ni utaratibu mzuri.Naomba wamiliki wa viwanja tuboreshe mawazo yangu .Lipa kodi kwa Maendeleo yako.Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nadhani Utakuwa unaongea peke yako Wenye Mamlaka wako bize na Kupika Majungu dhidi ya Lissu.

Wao ni Wanachojali ni kukaa madarakani na huku wakiendelea kutafuta Mikopo hala Wewe ndio utailipia kwa hiyo kodi.
Wao wanajimegea wanapanua Midomo halafu wanameza.
 
Back
Top Bottom