Kodi ya serikali kwa wafanyakazi (PAYE)

Mr.mzumbe

JF-Expert Member
Oct 11, 2011
935
1,000
Salaam,

Ndugu zangu naombeni kujua kitu kidogo kuhusiana na PAYE (Paye As You Earn). Kila siku magufuli na CCM wanatukalilisha kodi imeshuka mpaka 9% lakini mm kwenye mshahara wangu sioni kushuka chochote kile. Ndiyo kwanza naona kama % zimezidi mara dufu baada ya mshahara kupanda.

Kwa mfano mwanzo nilikuwa napata 600,000 tsh na paye ilikuwa ni 10% baada ya makato ya nssf i.e 10% ya nssf ni 60,000 tsh na kubaki 540,000 tsh then 10% ya paye ni 54,000 tsh na kubaki 480,000 tsh kama net paye. Kwa kifupi baada ya makato yote nabakiwa na 480,000 tsh.

Kwasasa napokea 935,000 tsh na paye ni 18%. Mchanganuo ni kama ufuatatvyo:-
10% ya 935,000=93,500 as NSSF na kubaki 841,500 tsh
18% ya 841,500=151,470 as PAYE na kubaki ~~ 700,000

Point yangu ya msingi ni kwamba mshahara wangu umepanda kwa tsh 300,000 tsh tu, lakin kodi imepanda kwa asilimia 9% zaidi, sasa kweli hili ni ongezeko fair wakuu??!! Na hata kama ni ongezeko fair, mbona wanasiasa wanatuambia kodi imeshuka mpaka asilimia 9 na wakati wanajua kodi hyo imeshuka kwa wachache kabisa, mbaya zaidi wanalisema hili bila ya kutoa ufafanuzi kuhusu hii kodi!! Kweli wafanyakazi tunaweza kuendelea au kusonga mbele kwa aina ya makato kama haya?!

Au hii kodi ni mimi pekee yangu naibiwa? lakini nimejaribu kucheck kweny link ya tra naona makato ni hayo hayo...Tanzania Revenue Authority - Calculators & tools
 
dapangi

JF-Expert Member
Jul 28, 2015
529
250
Utozaji wa PAYE (Pay As You Earn) huongezeka kwa asilimia kwa kila kiwango cha ongezeko la mshahara kwa mafungu yaliyoainishwa kuanzia kiwango cha kima cha chini cha mshahara. Siyo rahisi kujua kiwango cha kodi unayostahili kutozwa bila kuwa na muainisho wa utozaji. Haitozwi kwa asilimia sawa kwa vipato vyote. Kila kipato kinavyoongezeka ndivyo kodi inavyoongezeka.
 
NAKWEDE

JF-Expert Member
Aug 1, 2007
27,918
2,000
Mie nilidhani hilo punguzo la kodi litaanza mwezi Julai, 2016 kumbe ilikuwa baada ya yeye kutamka tu!? hebu tusubiri tuone mwezi wa saba kama kutakuwa na mabadiliko
 
Mkuu hapo ni sawa ila shida mbona makato ni makubwa sana na hayana uhusiano na ongezeko la mshahara!!? Ongezeko la kodi linabidi lihakisi na ongezeko la mshahara.
 
Mr.mzumbe

JF-Expert Member
Oct 11, 2011
935
1,000
Hiyo 9% sio kwa wale wa kima cha chini???
Okay kwa kima cha chini,lakini kwa nini wanapotosha watu kuhusu hiyo kodi?? Manake wanajisifia kwamba imeshuka till 9 % lakini hawatuambii imeshuka kwa watu gani?? Na kwann kwa watu wachache tu.
 
Zikomo Songea

JF-Expert Member
May 15, 2016
672
1,000
Mie nilidhani hilo punguzo la kodi litaanza mwezi Julai, 2016 kumbe ilikuwa baada ya yeye kutamka tu!? hebu tusubiri tuone mwezi wa saba kama kutakuwa na mabadiliko
Ndiyo ni kuanzia mwaka mpya wa fedha yaani Julai. Kama wameshaanza kukata huenda itakuwa ni mambo mengine (siyo kodi mpya). Binafsi hakuna mabadiliko katika mshahara wangu. Yawezekana ni bodi ya mikopo (HESLB) kama ulisoma kwa mkopo wa serikali. Nakushauri ufuatilie ili kupata uhakika.
 
KICHUNGWANI

Senior Member
Jan 20, 2016
135
225
Katika P A Y E makato yake sio kwa asilimia ya mshahara moja kwa moja inakuwa kwa wenye iliyozidi kiasi fulani inakuwa kiasi unajumlisha na kiasi kilichozida kiasi fulani ndio unatafuta asilimia
 
Asante

JF-Expert Member
Dec 18, 2009
2,086
2,000
Kodi mpya itaanza kulipwa mwaka mpya wa serikali kuanzia mwezi July 2016
 
Bulah

JF-Expert Member
Aug 19, 2011
230
225
Nnavyojua calculation haipo ivo mkuu
Hela ya makato ya mifuko ya jamii haikatwi kodi... so unadeduct
baada ya hapo unacharge 10% kwa kiasi kile cha kima cha chini then unadeduct
baadae kiasi kilichobaki kodi inaenda kati ya 20% to 30% kwa amount inayozidi kima cha chini... ingia tra ucheki formular vizuri
 
Lepanto

JF-Expert Member
Jan 5, 2015
1,165
1,500
Utozaji wa PAYE (Pay As You Earn) huongezeka kwa asilimia kwa kila kiwango cha ongezeko la mshahara kwa mafungu yaliyoainishwa kuanzia kiwango cha kima cha chini cha mshahara. Siyo rahisi kujua kiwango cha kodi unayostahili kutozwa bila kuwa na muainisho wa utozaji. Haitozwi kwa asilimia sawa kwa vipato vyote. Kila kipato kinavyoongezeka ndivyo kodi inavyoongezeka.
Ni progressive tax, lengo kupunguza gap ya wenye kipato kikubwa na kipato cha chini.
 
data

JF-Expert Member
Apr 9, 2011
22,580
2,000
Okay kwa kima cha chini,lakini kwa nini wanapotosha watu kuhusu hiyo kodi?? Manake wanajisifia kwamba imeshuka till 9 % lakini hawatuambii imeshuka kwa watu gani?? Na kwann kwa watu wachache tu.
Haiwezi kuwa sawa... ndo maana yaitwa Pay AAs You Earn.

Anaepokea M 3 usikute anakatwa 1 M point sth.
 
umande

JF-Expert Member
May 11, 2012
314
250
Mi nilisikia haiwahusu kwa watu wenye mishahara kuanzia milion mbili na zaidi. lakini kwa kiwango kama chako inatakiwa upande. Mi pia sijaona ongezeko, nikahisi hadi mwezi wa saba
Okay kwa kima cha chini,lakini kwa nini wanapotosha watu kuhusu hiyo kodi?? Manake wanajisifia kwamba imeshuka till 9 % lakini hawatuambii imeshuka kwa watu gani?? Na kwann kwa watu wachache tu.
 
KWEZISHO

JF-Expert Member
Jan 29, 2016
7,531
2,000
Ongezeko linatolewa mkono wa kulia halafu linapokwa mkono wa kushoto, halafu unatangaziwa kwa sauti kubwa TUMEPUNGUZA KODI KWA WAFANYAKAZI!
 
manizzle

JF-Expert Member
Apr 29, 2015
3,415
2,000
Hata hivyo katika historia serikali imejitahidi sana. Kukuongezea mshahara laki 3 tena kabla ya mwezi wa 7 kufika. Mkuu hebu furahia kwanza kabla ya kusikitika
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom