Kodi ya mifugo irudishwe: Sehemu ya mapato yake yaelekezwe kuboresha sekta ya mifugo

Kididimo

JF-Expert Member
Sep 20, 2016
4,017
3,654
Miaka ya tisini kurudi nyuma nchi yetu ilitoza kodi katika baadhi ya mifugo. Lengo lilikuwa pamoja na mambo mengine ni kuboresha mazingira ya ufugaji kama kujenga majosho, mabwawa,chanjo nk.

Hata hivyo,kodi hiyo kwa kiasi fulani ilidhibiti ongezeko holela la mifugo(hasa ngombe).

Hivi sasa kuna ongezeko kubwa la mifugo hususan ngombe,mbuzi na kondoo ambao huhitaji maeneo makubwa yenye malisho na maji. Wakati huohuo,wakiharibu mazingira ambapo serikali hugharamika kuyatunza.

Gharama hizi za serikali hutokana zaidi na kodi za watu wasio wafugaji japo wafugaji ni kwa sehemu ndogo. Ili kuweka usawa,mfugaji mwenye ngombe mfano 100 alipe zaidi ya yule mwenye 10 kwa vile atahitaji huduma kubwa na pia ataharibu eneo kubwa zaidi.

Haipendezi mtu ahodhi ngombe 1000 bila kulipia chochote huku akisababisha uharibifu mkubwa wa mazingira, na huku akiathiri jamii nzima kukosa maji.
Ninashauri,kodi hii irudishwe kwa ngombe,mbuzi na kondoo.

Fedha itakayopatikana ilenge;-
1. Kupima na kutenga maeneo ya wafugaji
2. Kuweka miundombinu kama mabwawa,majosho nk. katika maeneo hayo ili wafugaji wasihamehame
3. Kuendeleza nyanda za malisho ambayo baadh yatakuzwa kwa umwagiliaji
4. Huduma za ugani na utafiti
5. Mengineyo kutoka kwa wadau.

Ninaamini kwa serikali kufanya hivi, sekta ya mifugo kwa upande wa aina ya mifugo niliyoitaja,itajitosheleza.

Hakutakuwa na haja ya kukopa au kuchukua fedha sehemu nyingine kugharamia sekta hii.
 
Mifungo walivyokondeana hata wewe ungekubali kuwalipia kodi ambayo gharama zake ziko juu kuliko thamani yake?

unaakili hata mimi nawazia tunangomebe million 20 harafu tunashindwa kutoza hata sh 2500 ili tupate billion 50 ili zote tupeleke kwenya malambo na majoshi. Ndani ya miaka 5 tutakuwa na maeneon ya kuongesha na kunyweshea mifugo iliyobora.
 
Mifungo walivyokondeana hata wewe ungekubali kuwalipia kodi ambayo gharama zake ziko juu kuliko thamani yake?
Hivi sasa haina kodi. Pia ingelipa kodi ingewezesha serikali kuiboresha yenyewe na mazingira yake na isingekonda.
 
unaakili hata mimi nawazia tunangomebe million 20 harafu tunashindwa kutoza hata sh 2500 ili tupate billion 50 ili zote tupeleke kwenya malambo na majoshi. Ndani ya miaka 5 tutakuwa na maeneon ya kuongesha na kunyweshea mifugo iliyobora.
Asante kwa kuuona umuhimu wa hoja hii.
 
Ulishawahi fuatilia Hizo kodi nyingine mnazokatwa zinatumikaje?

Una uhakika gani hii kodi ikikatwa itaendeleza sekta ya mifugo?
 
unaakili hata mimi nawazia tunangomebe million 20 harafu tunashindwa kutoza hata sh 2500 ili tupate billion 50 ili zote tupeleke kwenya malambo na majoshi. Ndani ya miaka 5 tutakuwa na maeneon ya kuongesha na kunyweshea mifugo iliyobora.
Unavyoongea utadhani ndo mara ya kwanza unaifahamu serikali ya Tanzania. Hizo hela zitatumika kwenye kampeni na kuhonga maasimu wa CCM.
Hazitatumika kwa malengo yaliyokusudiwa.
 
Ulishawahi fuatilia Hizo kodi nyingine mnazokatwa zinatumikaje?

Una uhakika gani hii kodi ikikatwa itaendeleza sekta ya mifugo?
Ndiyo maana nimejaribu kuwa specific kuwa zielekezwe huko! Kodi hii iwe ni mahsusi kupunguza matatizo ya mifugo na wafugaji kuhamahama ovyo au kupigana. Pia hayo yakifanikiwa ,wafugaji watakuwa na amani. Jana nikiwa Ilula nimepata story moja ya kutisha sana. Sina uhakika sana kama ni ya kweli. Kuwa,kuna mfugaji mmoja karibuni kajitundika kisa ngombe wake 500 kati ya 600 aliokuwa nao kufa. Alikuwa akiswaga ngombe hao akitokea Morogoro kwenda Lindi kutafuta malisho na maji! Naamini mtu huyu asingekataa kulipa kodi ili aboreshewe mazingira yake ya ufugaji pale alipokuwa.
 
Hakuna kitu kama hiko. Viongozi wa Tanzania wanafahamika.
Hiyo hela itaenda kulipa deni la Tanesco au wajanja watazibeba kwenye masandarusi.
Japo una mawazo mazuri.
 
Back
Top Bottom