Kodi ya Majengo - Nani wanahusika?

Mama Joe

JF-Expert Member
Mar 30, 2009
1,504
828
Jamani naomba msaada hapa, nimekuwa nikisoma matangazo kuwa Majengo yatalipiwa kodi sasa kupitia TRA na maelezo mengine mengi ya TIN iliykwishatolewa etc.
Swali nauliza iweje majengo haya ambayo sijui yalipaswa yawe chini ya serikali za mitaa then Local Govt au sana wizara ya Ardhi yakusanyiwe kodi na TRA?
Nauliza hivi kwasababu ni muda mrefu wananchi tumekuwa tukifuatilia Hati hasa Kinondoni bila sababu zozote za msingi tumezungushwa wee.
Unakuta tatizo lolote hakuna, unaanzia serikali ya mtaa, unaenda Manispaa wanakwambia lipia kodi unatoa - then unakwama hapo hapo ukipitiliza uende Ardhi wakijaribu kuwasaidia Manispaa wagumu, hivyo wananchi wwanajenga bila hati, building permit wala plani maalumu za barabara yaani mitaa ni utahsi tu wa wakazi wenyewe kwamba hapa tuweke barabara.
Swali hiyo kodi inayotajwa inanihusu nini mimi mkazi ambae sijawahi kuiona Manispaa yangu mtaani? Au ni ya majengo ya Kisutu na Upanga? labda waishie maeneo waliyoruhusu ardhi wakapima na kuwapa hati lakini vinginevyo itakuwa ngumu - nitjueje kuwa serikali inajua nina nyumba au ni "servant quarter" ya tajiri aliyeziba njia yangu?
Mapato ndiyo yapo lakini bila kuwa na sensa kamili ya nyumba na hii itawezekana kwa kutupa hati miliki wananchi tutajuaje kuwa haya ndiyo mapato kamili?
Miaka ya Magufuli tulianza kuona mwanga kwa mbali lakini sasa hivi giza tupu, jamani is this too much to ask:
"Land title is the owners privilege and not a favour!"
 
Wana JF swali langu kwa wale wanaofahamu ni kuwa je hawa TRA wanafanya Valuation upya ya nyumba au wanachukua rates zilezile za kodi za majengo kama zamani? Huu ni ulaji tutaona mengi kabla ya Uchaguzi wa 2010.
 
Back
Top Bottom