Kodi ya majengo kuanza kukatwa kwenye Luku kuanzia Agosti 20, 2021. Je, Serikali imekosa Dira, mbinu zimewaishia?

ngebe

JF-Expert Member
Jun 8, 2020
1,789
5,105
E9IhhM_XsAIEuJp.jpeg

Naomba kuuliza maswali machache.

Ni sababu ipi hasa ya msingi iliyopelekea kutoka mfumo wa malipo wa zamani kuleta mfumo wa sasa?

Kwa hiyo kwanzia agost 20 kodi ya jengo inalipwa na mpangaji?

Vipi kuhusu nyumba ambazo kila chumba kina mita yake?

Vipi kususu mpangaji mmoja ambaye kapanga nyumba mbili?

Vipi nikiwa nikiamua miezi miwili ipite sijanunua luku?

CCM imekosa mbinu za kuendesha hii nchi.
 
Upumbavu tu!

Ndio mtajua kwamba nchi hii Rais wake alifariki toka tarehe 17/03/2021

Hivi inakuwaje?

Yani ile elfu 7 tuliyokuwa tunatozwa kipindi kile kabla ya Magufuli kuiondoa ndio wameirudisha kwa njia hii?

Hivi anaetakiwa kulipa kodi ya jengo ni mpangaji au mwenye jengo?

Unapokata kodi ya jengo kwenye luku maana yake mpangaji ndio atakuwa mlipaji wa kodi ya hilo jengo maana mwenye jengo yeye anachojali ni nyumba yake alishaingiza umeme na anakusanya kodi yake ya pango basi! Habari ya kwamba umenunua luku au laa yeye haimuhusu.

Tuliambiwa mafuta yanapanda sababu kwenye soko la dunia yanepanda,! Haya huko kwenye soko la dunia saa hii mafuta ni dola 64 kwa pipa, vipi wameshusha bei hapa nchini.?
 
Fungua kesi udai refund bosi.

Nyumba zisizo na umeme umeambiwa wataendelea na utaratibu wa zamani.

Wengine tuassume tu ni kama kodi ya uzalendo.

Haya maujenzi ili yaishe lazima tukamuliwe wote, hatutaki tena kukopa kwa mabeberu na kudaiwa riba...sasa tukamuane tu wote za matajiri zimeisha na wengine wamefirisika.
 
... hiyo sio kodi ya jengo; ni kodi ya kununua umeme!
Kabisa mkuu!
.
Nakumbuka wakati flani ilikuwa kila mwezi lazima ukatwe elfu 7 ukinunua luku

Magufuli akikuja kuiondoa na sasa naona mama nae kairudisha kwa mlango wa nyuma.

Ili ujue hii ni kodi ya luku na si jengo, angalia kwa mfano mtu mwenye jengo moja lenye wapangaji wengi akaamua kila mtu amuwekee mita yake maana yake hilo jengo litalipiwa kodi kutoka kila chumba?
 
Hawa watu wanaishi dunia ya wapi?

Wanafikiri mwenye nyumba ndio ananunua umeme badala ya wapangaji?

Walitakiwa wakae watulie wajipange vizuri. Copy and paste nayo inatushinda.

Tulivyonyamaza kwenye tozo wakaona wapenyezee makato mengine kwa luku.

Naona tutakatwa na kwenye maji muda si mrefu.
 
Walianza na shilingi mia kwa kila lita ya Petrol, Diesel, Kerosene

Wakaja kwenye tozo kwenye miamala

Wakaja kwenye tozo za line za simu

Tena kodi ya majengo kupitia Luku

Bado wataingia kwenye kodi ya mashimo ya vyoo... tuwe na subira tuendelee kushuhudia maajabu
 
Kabisa mkuu!
.
Nakumbuka wakati flani ilikuwa kila mwezi lazima ukatwe elfu 7 ukinunua luku

Magufuli akikuja kuiondoa na sasa naona mama nae kairudisha kwa mlango wa nyuma.

Ili ujue hii ni kodi ya luku na si jengo, angalia kwa mfano mtu mwenye jengo moja lenye wapangaji wengi akaamua kila mtu amuwekee mita yake maana yake hilo jengo litalipiwa kodi kutoka kila chumba?
Jibu ni NDIYO! Atalipia kwa kila mita

Na hapa watu tunataka kujiaminisha kuwa ni Kodi ya umeme, hapana. Ni Kodi ya jengo na imewekewa sheria (wameirejea kwenye tangazo) so kusema ni Kodi ya umeme kwa mlango wa jengo ni kupotosha

Kimsingi tatizo linabaki palepale, kwamba serikali hii imekosa watu wabunifu kwenye masuala ya utengenezaji mapato ndio maana wanazidi kumnyonya huyu anayeitwa mnyonge

Ni ajabu tena ya kushangaza kupitisha sheria hii huku ukisahaulisha kuwa kundi kubwa la watu wanaishi kwenye nyumba za kupanga...Sasa mpangaji ndio alipe Kodi ya jengo la mmiliki?

Mjinga anaweza kujibu "Jenga Yako"! Atakuwa amejibu, lkn ni jibu la kijinga

Ila napenda tu vile tunakamuliwa sote, yani ule utamu wa kuisoma namba upo kotekote
 
Kodi ya jengo ni elfu 10.

Sasa fikiria una jengo moja lenye vyumba 10 vya wapangaji, ukaamua kila chumba uweke mita yake ili kuepuka usumbufu kwa wapangaji. Na kila mita ikununua umeme inakatwa kodi huoni kama hilo jengo litakuwa linalipa kodi ya sh 100,000 badala ya 10,000?
Kodi kubwa kuliko ghorofa.

Tunajenga nchi.
 
View attachment 1897744

Naomba kuuliza maswali machache...

Majengo ambayo hayana umeme hayatakua yakilipiwa kodi?

Kwa hiyo kwanzia agost 20 kodi ya jengo inalipwa na mpangaji?

Vipi kuhusu nyumba ambazo kila chumba kina mita yake?

Vipi kususu mpangaji mmoja ambaye kapanga nyumba mbili?

CCM imekosa mbinu za kuendesha hii nchi.
Hii nchi ishafika mwisho
 
Back
Top Bottom