tpaul
JF-Expert Member
- Feb 3, 2008
- 21,776
- 18,192
Serikali imefuta kodi ya ushuru ya Shilingi 1,000 kwa kadi ya simu kwa kila mwezi na kupandisha kiwango cha ushuru wa huduma za mawasiliano kutoka asilimia 14.5 hadi asilimia 17, kuanzia Januari mwakani.
Akiwasilisha Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria ya Ushuru wa Bidhaa ya mwaka 2013, bungeni jana kwa hati ya dharura, Kaimu Waziri wa Fedha, Saada Mkuya Salum, alisema utaratibu huo uliopendekezwa utamwezesha kila mtumiaji wa huduma za mawasiliano kulipa ushuru unaolingana na matumizi yake.
Akifafanua alisema, mtu atakayetumia kidogo atalipa kidogo na mtu anayetumia zaidi atalipa zaidi tofauti na mfumo wa kulipa kiwango kimoja bila kuzingatia kiasi cha matumizi.
Aliwaeleza wabunge kuwa pendekezo hilo lina lengo la kupanua wigo wa kutoza ushuru huo kwa kujumuisha huduma zote za mawasiliano ya kielektroniki, huduma za kusafirisha mawasiliano kwa njia ya waya, optical fibre, njia zisizotumia waya na teknolojia nyingine yoyote ya aina hiyo, huduma za usambazaji wa mitandao, huduma za kusafirisha data, huduma za nukushi na huduma zingine za kielektroniki za namna hiyo.
Aina zote mbili zinatarajia kuipatia Serikali kiasi cha Sh. bilioni 148. Aidha, shilingi bilioni 30 zitalipwa na makampuni ya simu ili kukamilisha makadirio ya mapato ya ushuru wa huduma za mawasiliano katika mwaka wa fedha 2013/13 ili kukamilisha mafungu ya bajeti iliyopitishwa ya maji na umeme vijijini, alisema na kuongeza, hatua hiyo inatarajiwa kuipatia Serikali mapato ya Sh. bilioni 178,414.
Alisisitiza kwamba mapato yanayotokana na kodi hiyo hayajabadilishwa matumizi yake ya kugharimia huduma za maji na umeme vijijini kama ilivyopitishwa katika Bajeti ya Serikali kwa mwaka 2013/14.
Hata hivyo, alisema kutokana na changamoto zilizojitokeza, Serikali itaendelea kuangalia namna bora ya kuongeza mapato ya ndani katika bajeti ya mwaka 2014/15.
Mbunge wa Kisesa, Luhaga Mpina (CCM) alisema hali ya mapato ya nchi si shwari hali ambayo inalifanya taifa kuwa tegemezi na hivyo kutegemea misaada na mikopo.
Mbunge wa Mbozi Magharibi, David Silinde (Chadema), alisema malengo ya kodi hiyo ni mazuri lakini wananchi wanatakiwa kuona fedha zinazokusanywa zinatumika kwa malengo yaliyokusudiwa.
Mbunge wa Kuteuliwa, James Mbatia (NCCR-Mageuzi), alitaka katika bajeti ya mwaka ujao, Serikali iangalie namna ya kupunguza gharama ushuru wa huduma hizo za mawasiliano ili zilingane au kufanana na nchi zingine za Afrika Mashariki ambazo alisema ni ndogo.
Mbunge wa Iramba Magharibi, Mwigulu Nchemba, (CCM), alisema sekta ya mawasiliano ni muhimu na kiini katika maendeleo ya nchi hivyo ni Watanzania ni lazima waelimishwe kulipa kodi.
CHANZO: NIPASHE JUMAPILI :israel: