Salary Slip
JF-Expert Member
- Apr 3, 2012
- 48,694
- 149,917
Wabunge wanatarajiwa kukatwa asilimia 30 ya kiinua mgongo chao ambacho kimeelezwa kuwa ni Sh200 milioni.
Taarifa zilizopatikana kutoka kwenye Kamati ya Bajeti iliyopitia muswada huo, zimeeleza kuwa asilimia hiyo inatokana na marekebisho yaliyofanywa na kupitishwa na wabunge wenyewe kwenye Sheria ya Mapato ya 2010.
“Marekebisho ya asilimia 30 yalifanyika 2010 lakini huu muswada wa sasa unafuta msamaha hivyo, wabunge watakatwa kodi ya asilimia hiyo ambayo ni sawa na Sh60 milioni kila mmoja,” kimeeleza chanzo chetu.
Alipoulizwa kuhusu makato hayo Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Ashatu Kijaji amesema anayeweza kuzungumzia mambo ya Kamati ya Bajeti ni mwenyekiti wa kamati hiyo, Hawa Ghasia.
Hata hivyo, Ghasia alipoombwa kutoa ufafanuzi huo, ameeleza kuwa kamati yake bado inaendelea na kazi.
Chanzo:Mwananchi online
Hii ni sawa kabisa.Milioni 200 baada ya utumishi wa miaka 5 wakati watumishi wengine wanafanya kazi serikalini kwa miaka zaidi ya 30 hata miliono 100 hawapati alafu wao miaka 5 tu milioni 200!
Wacha wote tuisome namba.