Kodi toka Watanzania wanaofanya kazi nje ya Tanzania | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kodi toka Watanzania wanaofanya kazi nje ya Tanzania

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by Ndachuwa, Jun 20, 2012.

 1. Ndachuwa

  Ndachuwa JF-Expert Member

  #1
  Jun 20, 2012
  Joined: Mar 8, 2006
  Messages: 4,529
  Likes Received: 725
  Trophy Points: 280
  Katika mapendekezo ya bajeti ya Serikali na ile ya Upinzani rasmi bungeni sijasikia kodi toka kwa wafanyakazi wanaofanya kazi nje ya nchi kama moja ya vyanzo vya mapato.

  Mojawapo ya nchi inayonufaika na mchango toka hii sekta (export labour) ni Sri Lanka. Tanzania kwa sasa tunazalisha nguvu kazi inayozidi mahitaji ya soko la ndani.

  Ni wakati mwafaka kuanza kulegeza masharti ya kupata pass ya kusafiria na kuweka utaratibu wa hawa wenzetu kuchangia pato la Taifa.

  Sisi watanzania ni wepesi kusikia mgeni aliyeoko kwenye NGO kodi yake analipa nchini kwake lakini hatufuatilii watu wetu nao waje walipe kodi huku nyumbani.

  Kwa kuanzia, ningeshauri pendekezo la Waziri kuvuli kuwa kila Mtanzania ajaze ritani yake kwa mwaka lichukuliwe na serikali na litekelezwe kwa Watanzania wote wenye pass ya kusafiria.


  Kielelezo cha Sri-Lanka
  http://www.cuts-citee.org/pdf/Article-HMPSanjeevani.pdf
   
 2. NTINGINYA

  NTINGINYA JF-Expert Member

  #2
  Jun 20, 2012
  Joined: Oct 5, 2010
  Messages: 255
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Wewe ssm kweli yani badala ya kuitaka serikali iweke msimamo wa watanzania kuwa na hakina na kusaminiwa unataka walipe kodi unajua watu wanavyo menyeka huku nje nyie huko simpo kazini kama holday mnaingia mnavyo penda mnatoka mnapoamua. Ssm kweli hakuna kitu zaid ya hela
   
 3. Kituko

  Kituko JF-Expert Member

  #3
  Jun 20, 2012
  Joined: Jan 12, 2009
  Messages: 9,366
  Likes Received: 7,002
  Trophy Points: 280
  Mkuu, we unafanya kazi nje ama Upo Tanzania, WAtu wanaofanya kazi nje pesa yao huwa inakatwa kodi kwenye nchi husika, na unataka pesa hiyo ikatwe tena Tanzania, ni bora ungeshauri kitu unachokuwa na uhakika nachoAustralia wanafanya hivyo kama unavyotaka wewe,

  Lakini inapotokea huyo mfanyakazi asimamishwe ama mkataba wake ukiisha, serikali ya Australia inachukua jukumu la kumlea yeye na familia yeke (yaani inampa mshahara), sasa kwa Tanzania huyo mtu wa nje hata kama alikuwa anakatwa kodi na kazi yake kama imeeisha serikali itakuwa ipo tayari kumsaidia?
   
 4. Ndachuwa

  Ndachuwa JF-Expert Member

  #4
  Jun 20, 2012
  Joined: Mar 8, 2006
  Messages: 4,529
  Likes Received: 725
  Trophy Points: 280
  Ndugu yangu NTINGINYA pamoja na kumenyeka sana huko ughaibuni, pengine utarudi na gari ambalo litatumia barabara ambazo tumejenga sisi kwa kodi zetu wewe hujachangia hata sumni; pengine umeacha nyumba na mali nyingine na utazikuta salama kutokana na kazi nzuri ya Mambo ya ndani, wizara inayoendeshwa kwa kodi zetu sisi uliotuacha huku bongo.

  Bwana NTINGINYA ni mambo mengi kama Taifa yanayogharamiwa kupitia kodi ningetegemea mlio nje mngeona fahari kuchangia mapato ya Taifa tofauti na kulalama. Kwa mfano tuu tunaye naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, is she feeling okay if she has contributed nothing in terms of taxes for all period she has served UN?
   
 5. Ndachuwa

  Ndachuwa JF-Expert Member

  #5
  Jun 20, 2012
  Joined: Mar 8, 2006
  Messages: 4,529
  Likes Received: 725
  Trophy Points: 280
  Jamaa yangu Kituko sitofautiani sana na wewe ilia kutoa "Assurance" ya kuendelea kulipwa baada ya kazi kumalizika hilo hapana ila wachangie mapato ya Taifa. Mfano mtu aliyesomeshwa kwa kodi zaTanzania hada kupata PHD, kwanini dhamira isimsute pale ambalo mchango wake kwa Taifa ni sifuri?
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 6. DullyM

  DullyM Member

  #6
  Jun 20, 2012
  Joined: Mar 24, 2011
  Messages: 74
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 15
  Mkuu mi naona bora utafute mada zingine za kuzungumzia ili taifa liendelee. Ingekuwa vizuri ukajaribu kutia changamoto kwenye kodi zinazokusanywa za watanzania waliopo nchini zinatumika vipi kabla hujaanza kutafuta mfarakano na wanaoishi nje! ama mzee na wewe upo katika ukusanyaji?

  Na unapozumzia export na import na kumuuliza huyo muungwana kwamaba anatumia barabara akirudi nyumbani. fikiria pia nani anachangia upatikanaji wa fedha za kigeni nchini kwako. Inama ufikiri mkuu.
   
 7. M

  MANAKE MKARI Senior Member

  #7
  Jun 21, 2012
  Joined: Jan 25, 2011
  Messages: 123
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Mnaacha kukusanya mapato kwenye rasilimali tulizopewa bure na Mungu mnaafikiria wabeba box. Yaani mtu alale masaa 4 tu then alipe kodi ughaibuni na Tz pia?Uliona wapi kodi inalipwa mara mbili. Nchi inasaidiaje wabeba box wakati hata kupata passport tu huwa ni shughuli. Pia kumbuka kuwa hela nyingi za wabeba box zinarudi TZ kwa njia nyingi tu.
   
 8. Money Stunna

  Money Stunna JF-Expert Member

  #8
  Jun 21, 2012
  Joined: Aug 9, 2011
  Messages: 13,105
  Likes Received: 284
  Trophy Points: 160
  Wewe ungejua kodi nje zilivyo kuwa nyingi na mzigo wala usingesema na tanzania wakate tena kodi,kwa nje bill ni nyingi,kodi ni nyingi bila kufanya overtime uwezi kumudu,njia pekee ni kuzibiti na kuhahakisha makampun makubwa ndani ya tz ayaepuk kutoa kodi,

  Inakuaje kwenye sector ya madini serikali ipate asilimia 3 tu ya mauzo wakati botswana wanapata asilimia 40 na wanawaforce investors kujenga miundo mbinu,uoni tatizo apa?

  Tatizo sio walio nje walipe kodi, bali kusimamia makampun makubwa ya ndani ya sikwepe kodi na kubadilisha sheria za zamani kwa miongo kazaa bey ya dhahabu imepanda sana lakin kodi ile ile asilimia 3,wap na wap?
   
 9. Kitope

  Kitope JF-Expert Member

  #9
  Jun 21, 2012
  Joined: Oct 12, 2011
  Messages: 228
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Mtoa mada Unatafuta uchokozi na watu wenye machungu na senti zao za mabokisi. Uchumi/maendeleo yetu hayawezi kukua kwa kuwakaba wabeba maboksi. uchumi tumeukalia wenyewe kama alivyosema babu. Mimi ningekushauri ufunge virago toweka bongo kabebe boksi kisha rudi utuambie kama uliyoyasema bado unayafikiria yafanyike hivyo.
   
Loading...