tajirijasiri
JF-Expert Member
- Oct 13, 2012
- 2,864
- 3,851
Mwanasiasa hupenda sifa na kufurahisha watu anaowaongoza. Sheria za kodi hutungwa na Bunge na baadae kusimamiwa na TRA. Ukubwa au unafuu wa kodi ni lazima uwe katika viwango na utetezi wa sheria na uhalisia. Majadiliano ya kikodi kati ya Afisa wa kodi na Mlipakodi ni haki na wajibu wa pande zote mbili.
Endapo Serikali inataka kodi halali yenye mizania sawa, basi itunge sheria, kanuni na miongozo rafiki, ili huyo mkusanya kodi, aenende vile Mamlaka inavyotaka.
Ukubwa au unafuu wa makadirio hutegemea sana ulipaji kodi wa hiari wa mlipakodi. Ukwepaji kodi wa muda mrefu hupelekea malimbikizo ya kodi, riba na adhabu na hivyo kodi kuwa kubwa.
Endapo Afisa wa kodi akapunguza kiwango cha kulipa, chini ya kiwango halisi anachostahili mlipakodi, basi serikali hiyo hiyo itambana tena kupitia CAG/NAOT. Na pengine kodi ikaongezeka tena au muda mreeeefu wa utetezi ukachukua muda wa Afisa na Mlipakodi katika kujibu hoja.
Tunapotamka kodi, hatuishii kwa TRA/ Afisa wa kodi pekee yake, hata CAG/ Mkaguzi na Bunge wahusishwe pia.