mwengeso
JF-Expert Member
- Nov 27, 2014
- 9,227
- 6,666
Kuna mjadala mkali kuhusu kutozwa kodi kwenye miamala ya fedha kwa njia ya simu na benki. Bila kujiinguza katika ubishani unaojengwa kisiasa, kihisia na kinadharia zaidi kuliko uhalisia, ni vyema tukatumia takwimu za kitafiti.
Takwimu za matumizi ya kipato (tovuti ya Ofisi ya Takwimu ya Taifa, Mei, 2016) katika kugharamia maisha yao (Consumers Price Index), kuona kama gharama za huduma za mabenki na ada za miamala ya fedha katika simu, imekuwa ikichangia katika gharama za maisha ya Mtanzania, zinaonesha kuwa gharama hizo ni sehemu ndogo tu ya matumizi ya Watanzania katika mahitaji yao kimaisha.
1) Chakula na vinywaji: takwimu zinaonesha kuwa sehemu kubwa ya kipato cha Watanzania, asilimia 38.5 hutumika kugharamia chakula na vinywaji visivyo na kilevi, ambavyo havijatozwa kodi.
2) Usafiri na Usafirishaji : Huduma hii huchukua asilimia 12 ya kipato cha Mtanzania na ikipanda ina mchango mkubwa katika kuongeza mzigo wa gharama za maisha yao. Katika kuhakikisha kuwa usafirishaji na usafiri hauendelei kuwa mzigo katika maisha ya Watanzania, Serikali ya Awamu ya Tano, katika Bajeti yake ya kwanza, ilikwepa kuongeza kodi au tozo ya aina yoyote katika mafuta.
3) Nyumba, maji, nishati: huduma na au bidhaa hisi zinachukua asikimia 11.6 ya kipato cha Mtanzania. Hizi ni gharama za nyumba kwa maana ya kodi, maji, umeme, gesi na nishati nyingine inayotumika katika makazi ya watu. Katika huduma hizo, hakuna kodi iliyoongezwa ukiacha kodi katika kodi za pango na kuboresha mfumo wa ukusanyaji wa kodi za majengo. Pia, badala yake huduma kama umeme, ambayo ilishuka bei kuanzia mwanzoni mwa mwaka huu, serikali imetenga fedha nyingi kuisambaza kwa wananchi wengi zaidi ili wanufaike.
4) Mavazi, mawasiliano: Huduma na au bidhaa hizi ni kama mavazi na viatu vinavyochukua asilimia 8.3 ya kipato cha Watanzania. Pamoja na kodi katika mitumba, inayotajwa kuvaliwa na watu wengi kuongezwa kodi, lakini wengi wetu hatuichukui kuwa mzigo kwa wananchi kama tunavyochukulia gharama za huduma za benki na za kuhamisha miamala ya fedha kwa kutumia simu.
5) Huduma za mawasiliano: hizi bila kufafanuliwa kama zinahusu pia huduma za uhamishaji wa miamala kwa njia ya simu, lakini kwa hakika hazihusishi gharama za huduma za benki, huchukua asilimia 5.6 ya kipato cha Mtanzania.
6) Sigara, vilevi vingine: hizi zinachukua chini ya asilimia tano ya kipato cha Watanzania na asilimia yake katika mabano ni pamoja na huduma za migahawa na hoteli (asilimia 4.2) na huduma za vilevi na sigara, ambazo karibu kila bajeti, zimekuwa zikiongezwa kodi, lakini huchukua asilimia 3.7 tu ya kipato cha Watanzania.
7) Huduma na bidhaa zingine ambazo kutokana na kuchukua chini ya asilimia 1.5 ya kipato cha Watanzania, zimewekwa pamoja na kupewa jina la huduma na bidhaa mbalimbali, ambazo huenda ndiko ziliko gharama za mabenki, kwa ujumla wake zimetajwa kuchukua asilimia 3.1 tu ya kipato cha Watanzania.
8) Huduma za afya, hugharimu asilimia 2.9 ya kipato cha Watanzania,
9) Starehe na masuala ya utamaduni asilimia 1.6 ya kipato cha Mtanzania.
10) Gharama za elimu, ambayo kwa sasa inatolewa bure kutoka darasa la awali mpaka kidato cha nne, ikichukua asilimia 1.5 tu ya kipato cha Watanzania walio wengi.
Imenukuliwa kutoka Gazeti la Habari leo ikiandikwa na Joseph Lugendo na Ikunda Erick.
Taarifa hii inaonesha kwamba athari za kutoka kodi miamala ya fedha kwa simu au benki ni matumizi kidogo sana ya kipato cha Mtanzania.
Ukweli pia ninkwamba Watanzania wengi (bila kujali kipato chao) hupendelea vinywaji vyenye kileo. Hivyo wengi wao hunywa nyumba. Kwa mfano, gharama ya bia moja (1) ni sawa na gharama ya tofali tatu (3). Fanya hesabu kwa wewe unayekunywa bia kwa mwezi umekunywa tofali ngapi!
Pamoja na kwamba kodi mpya kwenye miamala ya fedha inachukua kiasi kidogo cha kipato cha Mtanzania, ni mhimu kufanyike tathmini nani ni waathirika wa leo na baadaye na iwekwe kwenye maandishi nani anapaswa kulipa kodi hiyo kama ni mlaji au mtoa huduma, alipendekeza Dk Haji Semboja, Mhadhiri Chuo Kikuu DSM, Idara ya Uchumi.