MZALENDOWAKWELIKWELI
JF-Expert Member
- Feb 5, 2012
- 330
- 210
Nimemsikiliza vizuri Dr. Mpango na ufafanuzi wa TRA juu ya upotoshwaji uliofanywa na CRDB kwamba VAT itakayochajiwa kwenye gharama za uhaulishaji wa fedha zingebebwa na mteja. Kimsingi uelewa wa CRDB ndio ambao niliojifunza darasani kwamba VAT inalipwa na mteja muuzaji yeye ni mkusanyaji tu, sasa ufafanuzi wa TRA na Dr. Mpango kwamba muuzaji wa huduma kwa maana ya mabenki na makampuni ya simu ndiyo yatakayoilipa hyo inayoitwa "VAT" kwenye kipato chao hilo ni la kwanza na la aina yake.....Sina tatizo na mabenki kulipa kodi but ni vema wataalam wakashirikishwa ili kushauri approach sahihi. Mkanganyiko utakaojitokeza utaipotezea serikali mapato badala ya kuongezeka coz mlaji atapewa risiti yenye VAT hivyo kustahili kuclaim input tax kwa VAT on purchase ambayo hakuilipia yeye......