Kodi kwa mfanyakazi na matumizi yake na familia

samakinchanga

JF-Expert Member
Aug 24, 2014
2,024
1,232
Kodi ya nyumba kwa mwezi vyumba vitatu 200,000/-kiwango cha kawaida,mara miezi 6=1,200,000/ chakula cha familia takribani 20,000 kwa siku kiwango cha kawaida mara siku 30 =600,000/-basi kama ana kagari walau kwa mkopo cc 1500 kodi ya TRA road licence tshs 230,000 hapo bila penalty ukichelewa tu 280,000/-inakuhusu jamani jamani bado hujalipia maji ya mita walau 15,000 kwa mwezi, umeme wa 30,000 kwa mwezi bado kodi ya mshahara ambayo watumishi wengine hukatwa kufikia 350,000/- hadi 400,000/- kwa mwezi zidisha kwa mwaka unapata milioni 4 na ushee niishie hapo tu kwanza hapo hajaenda hospitali,hajanunua nguo,n.k

Je mtumishi huyu mbona anaishije kama haishii kujikimu kwa njia zingine za mkato? mahesabu kwa mwaka ni takribani 7,800,000 na mshahara wake kwa mwaka ni 5,000,000 kwa mwaka.

Basi watazamwe kwani ni walipa kodi wakubwa
 
Hawasikii viziwi hawa wa ccm. Wao wanaishi kwa posho zinazozidi mishahara yao ndio maana hawajui mshahara wake ni kiasi gani. Dawa ni kufisidi tu ili tufanane nao kwani ni upuuzi kumsubiri aliye juu kushuka.
 
Hakuna kitu kibovu kama kodi kubwa kwenye mshahara kiduchu. Raisi wangu naamini utaliangalia hili kwa macho yote mawili Mwenyezi Mungu akuongoze ulifanyie maamuzi ya busara. Nakuhakikishia watumishi wakipata mshahara wa kutosha bila kodi kubwa za kukera na makato mengine ya hovyo kama tughe na talgwu ambao hatuoni umuhimu wala ufanisi wao. Watumishi watapiga kazi kwa nguvu zao zote kwani stress za maisha zitapungua kiasi kikubwa.
 
Kodi za sasa hazilingani na hali halisi ya maisha.

Serikali imeng'ang'ania kutoza kodi kubwa bila kuangalia gharama kubwa za maisha yanayowakabili wananchi, hasa wa hali ya chini.

Hali hii haiwezi kupunguza rushwa hata kidogo.

Aidha wapunguze kodi au wazidishe mishahara.
 
sasa wapite na huku wasome tena kuanzia wabunge watakakwenda kwenye bajeti ili waone uhalisia.maana TUCTA ipo kimya kama vile
 
Mkuu, gari na nyumba ya laki mbili nadhani ni anasa kubwa sana. Mbagala kuna hadi chumba cha buku saba... Hujaamua tu mzazi!
 
Kodi za sasa hazilingani na hali halisi ya maisha.

Serikali imeng'ang'ania kutoza kodi kubwa bila kuangalia gharama kubwa za maisha yanayowakabili wananchi, hasa wa hali ya chini.

Hali hii haiwezi kupunguza rushwa hata kidogo.

Aidha wapunguze kodi au wazidishe mishahara.
Rushwa ni hulka kwanza, kabla ya chochote. Unless uniambie Luwasa na viongozi wengine walioibia taifa wakiwa CCM walikuwa wana malipo kiduchu na kodi kubwa...
 
Back
Top Bottom