Kocha Yanga (inawahusu zaidi wana Yanga) | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kocha Yanga (inawahusu zaidi wana Yanga)

Discussion in 'Sports' started by Anselm, Jun 24, 2012.

 1. Anselm

  Anselm JF-Expert Member

  #1
  Jun 24, 2012
  Joined: Nov 16, 2010
  Messages: 1,705
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Bila shaka deal la Maximo limeshaota mbawa,whether ni kwasababu ya yanayosemwa kuhusu e-mail za wasiolitakia mema soka la Tanzania(mana'ke kwa kiasi kikubwa Yanga ndo Tanzania) au ni ksbb ya mkataba mgumu-kuvunjika alionao Mtaalamu Maximo na team yake anayoifundisha sasa ya Democrata Gv, hatunabudi kuyaacha hayo na kuangalia tunapoelekea...ni wakati muafaka sasa wa Viongozi wa Yanga kuhakikisha wanapata Mwalimu(Kocha) mzuri haraka iwezekanavyo atakayeweza kutumia ujuzi wake pale na kuifanya Yanga itishe, kuiacha team mikononi mwa Fred Felix Katalaiya Minziro "Baba Isaya" pekee tunapoelekea kwenye Kagame naona ni jambo la hatari sana.
  Binafsi namkubali Minziro ksbb najua ni Mwana'Yanga wa kihalisia aliyecheza pale kwa kujitolea sana na amekuwa akijitahidi kufundisha kwa uwezo wake wote lkn naamini uwezo wake hauwezi kuviunganisha vipaji vya kina Kiiza,Meddy Kagere(kama tutampata),Febregas,Domayo,Nizar,Yondani na wengineo na kutengeneza team itakayotisha mathalani kwenye michuano ya Kagame inayotarajia kuanza hivi karibuni,nimekuwa nikimfatilia kwa karibu Minziro na kugundua amekuwa aki'lack vitu fulani ambavyo Mwalimu mzuri wa soka la kisasa anapaswa kuwa navyo na ndo maana amekuwa akivuna matokeo yasiyo mazuri mara zote ambazo amekuwa akiachiwa team kama kocha mkuu(mkifuatilia records zake mtakubaliana na mimi),ni vema Viongozi wakatafuta Kocha mzuri zaidi wakati Minziro akiendelea kujifunza baadhi ya mambo kama Kocha msaidizi kwani atakuwa anaji'accumuletia maujuzi ambayo yanaweza kumfanya aje kuwa Kocha mzuri sana baadaye kama ilivyotokea kwa AVB.
  Naomba kuwasilisha!
   
 2. M

  Mzawa Halisi JF-Expert Member

  #2
  Jun 24, 2012
  Joined: Feb 25, 2009
  Messages: 499
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 35
  Naona tatizo la Yanga kama
  Zilivyo klabu zingine ni zaidi ya kocha. Hakuna kocha makini anayeweza kukubali kufundisha klabu ambayo ina mfumo wa uongozi wa kibabaishaji ikiwa ni pamoja na kutokuwa na vyanzo vya uhakika vya mapato. Nilcheka sana niliposikia mzee mmoja anadai Yanga ina millioni 700 sijui kwa chanzo kipi. BTW mm ni mpenzi ya Yanga lakini sikubaliana na mngt style ya miaka ya 70 kuwa inaweza kuivusha timu kwenda mbele.
   
 3. Anselm

  Anselm JF-Expert Member

  #3
  Jun 24, 2012
  Joined: Nov 16, 2010
  Messages: 1,705
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Ndo maana tutafurika hapo tarehe 15 July kwenye uchaguzi ksbb baadhi yetu tunafahamu kuwa figures fulanifulani zikiingia kwenye uongozi Club itakuwa imepiga kona kuachana na Mgt style za mwaka 70,lkn pamoja na hilo Mkuu siyo kwamba Makocha wazuri hawataki kujitokeza kuifundisha Yanga la-hasha Jamaa walikuwa na applications za makocha kama 30 hv,wa maana tupu wakawachuja mpk wakafikia 5,sasa hapo kama wame'stuck hakuna kinachoendelea Mzigo wote wameuacha kwa Baba Isaya na Kagame hiyooo...
   
 4. M

  Masuke JF-Expert Member

  #4
  Jun 24, 2012
  Joined: Feb 28, 2008
  Messages: 4,606
  Likes Received: 108
  Trophy Points: 160
  Kila la heri watani, mpira sio ugomvi sie tutawakia kila lililojema ila tukikutana Kagame safari hii hatukubali.
   
 5. Likwanda

  Likwanda JF-Expert Member

  #5
  Jun 24, 2012
  Joined: Jun 16, 2011
  Messages: 3,854
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Dah, unayosema ni kweli kabisa, tena tunahitaji kocha atayekuwa anainua vipaji pia.
   
Loading...