Kocha wa Yanga, Luc Eymael ailalamikia Mbeya City baada ya kushindwa kuifunga

DullyJr

JF-Expert Member
Apr 10, 2011
13,979
11,816
Kocha wa Yanga, Luc Eymael amesema kuwa sababu iliyopeleka kushindwa kupata pointi tatu dhidi ya Mbeya City ni kutokana na aina ya mchezo waliocheza wapinzani wao.

Mchezo huo uliopigwa katika uwanja wa taifa na kulimalizika kwa sare ya bao 1-1, Mbeya City ikipata bao katika kipindi cha kwanza na Yanga ikisawazisha kipindi cha pili.

Akizungumza baada ya mchezo huo, Luc Eymael amesema, "sisi tumecheza vizuri lakini unaona wapinzani wetu walivyocheza, walikuwa wamejaa nyuma na kubakiza mchezaji mmoja mbele".

"Makosa yalifanyika katika kipindi cha kwanza na kupelekea bao tulilojifunga, lakini tulikuwa bora zaidi kipindi cha pili na tukapata bao lakini shida bado ilikuwa namna walivyokuwa wakicheza nyuma", ameongeza

Basi bora ungewaambia wajipange utakavo wewe ili uwafunge
 
Malalamiko FC
Screenshot_20200213-105955.jpeg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huu ni umbumbumbu pure kabisa. Sasa wapi alipolalamika zaidi ya kuelezea mbinu za mchezo?
 
Sasa hapo si kila Kocha na mbinu yake, Mbona Ndala game na Simba wanapaki basi.
 
Kocha wa Yanga, Luc Eymael amesema kuwa sababu iliyopeleka kushindwa kupata pointi tatu dhidi ya Mbeya City ni kutokana na aina ya mchezo waliocheza wapinzani wao.

Mchezo huo uliopigwa katika uwanja wa taifa na kulimalizika kwa sare ya bao 1-1, Mbeya City ikipata bao katika kipindi cha kwanza na Yanga ikisawazisha kipindi cha pili.

Akizungumza baada ya mchezo huo, Luc Eymael amesema, "sisi tumecheza vizuri lakini unaona wapinzani wetu walivyocheza, walikuwa wamejaa nyuma na kubakiza mchezaji mmoja mbele".

"Makosa yalifanyika katika kipindi cha kwanza na kupelekea bao tulilojifunga, lakini tulikuwa bora zaidi kipindi cha pili na tukapata bao lakini shida bado ilikuwa namna walivyokuwa wakicheza nyuma", ameongeza

Basi bora ungewaambia wajipange utakavo wewe ili uwafunge
Lucy anapenda kulalamika kama mke mkubwa kwenye ukewenza!
 
Back
Top Bottom