Kocha wa timu ya taifa Uingereza ameachia Ngazi

GODLOVEME

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
1,640
493
Sam allardyce,kocha wa timu ya taifa ya UIngereza ameachia ngazi kwa makubaliano na Shirikisho na mpira wa miguu nchini humo baada ya kufanya kazi kama meneja wa timu hiyo kwa muda wa siku 67 na kucheza mechi moja tu

Moja ya sababu zilizosabaisha kuondolewa kwenye nafasi hiyo ni ushauri alioutoa wa kupindisha sheria za usajili wa wachezaji. Pia kocha huyo mwenye umri wa miaka 61 anashutuma kwa kosa la kutumua madaraka yake kuingia makubaliano yenye dhamani ya £400,000 sawa na 1,138,942,650 shilingi za kitanzania na Far East firm.

Chama cha michezo cha uingereza FA kimesema Sam allardyce tabia yake haikuwa nzuri, na Gareth Southgate atakuchukua nafasi yake kwa muda

FA waliendelea kusema "amekubali kuwa amefanya kosa na ameomba msamaha, haya siyo maamuzi mepesi bali kipao mbele cha FA ni kulinda maslai mapana ya michezo na kudumisha nidhamu ya hali ya juu kwenye mpira wa miguu(Soka)"

"kama kocha wa timu ya Taifa ya uingereza lazima awe na uwezo wa kuonyesha uongozi bora na pia awe ni mtu mwenye intergrity kwenye michez wakati wote"

Kwa kusema hivyo Sam allardyc amekuwa ni moja wa kocha aliyeifundisha timu hiyo kwa muda mfupi zaidi kwa kuifundisha timu ya Uingereza kwa muda wa siku 67 tu.


Chanzo: Ligikuu.com
 
Ndio soka mkubwa ulitaka kula mingo kama africa jo wathungu wako fasta sna juu sheria zao
 
Back
Top Bottom