Kocha wa taifa stars na kilimanjaro stars

Anfaal

JF-Expert Member
Jan 19, 2010
1,154
0
Kuna hili suala la kocha wa Timu ya Taifa kufundisha Kilimanjaro Stars wakati Zanzibar pia kuna timu nyingine.
Nadhani kuna haja ya kocha wa Taifa aendelee kubaki kuwa wa Taifa na michuano kama ya challenge ambayo haitambuliki na FIFA wawe wanapewa makocha wazalendo. Ni lini Taifa litajiaminisha kwa makocha wazalendo. Kama tunashindwa kuwapa hata nafasi katika michuano hii, lini tunawaamini. Pia michuano kama hii ingetumiwa maalum hasa kwa kocha kutafakari vipaji vilivyopo kutoka pande zoote mbili za nchi. Naomba nieleweke wazi kuwa posts hii haina malengo ya kisiasa.
 
Newvision

JF-Expert Member
Nov 9, 2010
446
0
Anfaal sawa lakini hili wazo/swali halina tija yote ni Tanzania tu au vipi? Makocha wa kizalendo hasa hapa Tanzania hawataki kujifunza ipasavyo na hakuna hata mmoja aliyeonyesha anaweza na uwezo licha ya kusoma sana ujerumani, Brazil etc etc. Mbona hapa kwenye ligi ya nyumbani vijana wanaowafundisha hawaonyeshi kitu chochote? Angalia Moro United Coast Union, Majix2 etc ni butua butua tu hakuna ufundi wowote. Hatuwezi kuwaamini watufundishe soka ya aibu ambayo inatuathiri hata kwenye Timu ya Taifa.
Mwisho si kweli kuwa Challenge cup haitambuliki na FIFA inatambulika ila huwa haisishwi kwenye ranking tu.
 
Licha ya kutohusishwa na kwenye ranking, lakini pia haipo kwenye calender ya FIFA kuruhusu wachezaji wa nje nao kucheza. Kwahiyo ukiangalia hizi sababu mbili kuu kwa ujumla tukubali kuwa michuano hii ipo kwa ajili ya kujiburudisha labda na hilo la kupata fursa ya kujipima na vijana wengine. Hebu angalia hiyo Ivory Coast. Ndio hiyo ya kombe la dunia.
Wapo makocha wazalendo na wanamafanikio pia. Mf kocha Mkwasa si wa kubeza. Julio, licha ya mafanikio yake siwezi kuelezea uwezo wake. Hawa makocha wazalendo ni muhim saana kwakweli maana ndio wanafaham namna hasa ya kuwasiliana na vijana wetu. Angalia Uingereza sasa hivi wao wamesema wazi next coach atakuwa mzawa. Licha ya hivyo, hao wa kigeni wametusaidia nini mpaka sasa hivi?
 
Newvision

JF-Expert Member
Nov 9, 2010
446
0
Licha ya kutohusishwa na kwenye ranking, lakini pia haipo kwenye calender ya FIFA kuruhusu wachezaji wa nje nao kucheza. Kwahiyo ukiangalia hizi sababu mbili kuu kwa ujumla tukubali kuwa michuano hii ipo kwa ajili ya kujiburudisha labda na hilo la kupata fursa ya kujipima na vijana wengine. Hebu angalia hiyo Ivory Coast. Ndio hiyo ya kombe la dunia.
Wapo makocha wazalendo na wanamafanikio pia. Mf kocha Mkwasa si wa kubeza. Julio, licha ya mafanikio yake siwezi kuelezea uwezo wake. Hawa makocha wazalendo ni muhimu saana kwa kweli maana ndio wanafaham namna hasa ya kuwasiliana na vijana wetu. Angalia Uingereza sasa hivi wao wamesema wazi next coach atakuwa mzawa. Licha ya hivyo, hao wa kigeni wametusaidia nini mpaka sasa hivi?
Siko optimistic na Kocha yeyote Mzawa ni mawazo yangu. Mafanikio unayosema ni yapi waliyoleta wazawa walipopewa timu?
Tanzania imeanza kujulikana na kuogopwa kidogo juzi Maximo alipokuja kwani hata butua butua za uwanjani zimeanza kukoma lakini kwa sasa toka grass root na timu zenye makocha wazawa ni mbovu hata timu yetu ni mbovu tu. Safari ni ndefu nadhani suluhisho ni kuanza huku chini kuwa na waalimu wenye taaluma tena ya kutosha na siyo mradi mpira uende. Huku Brazil kuna shule za soka, kwa hiyo kijana anasoma soka na masomo mengine ndiyo maana wanauwezo wa kuunda timu hata 4 za taifa bila wasiwasi. Siye twaweza?
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom