Kocha Somalia aomba radhi kuchemsha

kilimasera

JF-Expert Member
Dec 2, 2009
3,068
268
Doris Maliyaga KOCHA mkuu wa Somalia, Yosof Adam amewaomba msamaha wadau waliokuwa wakivutiwa na timu yake lakini akasema ilikuwa vigumu kwake kufuzu kwa sababu ni michuano mikali. Adam ambaye ni mara yake ya kwanza kuja Afrika mwaka huu mara tu baada ya kuingia mkataba wa kuinoa Somalia akitokea kwao Qatar mapema Agosti. Ameliambia Mwananchi Jumapili kuwa anaamini kuna wapenzi ambao walikuwa wakiinga mkono timu yao lakini wakubaliane na matokeo hayo kwa sababu walizidiwa na michuano ilikuwa migumu kwao. ''Ndiyo mara ya kwanza kuja na kushiriki michuano kama hii ambayo imekuwa ni migumu mno kwa upande wangu nawaomba kubaliane na kilichotokea kwa sababu tulizidiwa lakini ndiyo muda muafaka wa sisi kujipanga kwa ajili ya msimu ujao.''alisema Adam ambaye pia ni kocha wa U-17,U-20 na hii ya wakubwa. Adams akaongeza kuwa kwa sasa anarudi Somalia kwa ajili ya kujiandaa na michuano ya kufuzu mashindano ya Afrika ambayo yanaendelea kwqa ajili ya kupata timu zitrakazofudhu fainali zitakazofanyika Sudan..
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom