Koboko (black mamba) ana kiburi, jeuri na dharau sana ila nitamfundisha adabu

Vipi umeshamfundisha adabu Koboko huyo? Kama bado, mimi ninakushauri ufanye mojawapo ya mambo haya:
(a) Pulizia petroli eneo alipo; atakimbia na kabla hajafika mbali iwapo mvuke wa pteroli utamgusa basi atakufa polepole kulingana na wingi wa petroli iliyomgusa.
(b) Leta nguchiro kama watano hivi eneo alipo
(c) Tafuta jamaa wa maliasili-wanyamapori wadili naye

Heshima kwako mkuu. Sema lile jukwaa limepoa sana. Mijadala imepoa sana.

Vipi mbona kama huyu mleta mada hujamuelewa au mm ndo sijamuelewa?
 
Mkuu usipate shida chuma tairi chini ya huo mti yeye akiwa Juu, au pilipili mwendo kasi
 
Kuna kamnyama flani kako kama paka huwa kanamwazibu sana koboko na koboko akisha mwona tu hako kamnyama ujanja huwa unamwisha hivi huwa kanatumia njia gani kumwenyesha koboko?
 
Kana speed na akili ya ziada, pia yupo mnyama mwingine hapati madhara ya sumu anang'atwa ila hafi.
Kuna kamnyama flani kako kama paka huwa kanamwazibu sana koboko na koboko akisha mwona tu hako kamnyama ujanja huwa unamwisha hivi huwa kanatumia njia gani kumwenyesha koboko?
 
Wasikutisheeee...deal nae braza..

Binadamu tumepewa atashi mkubwa na uwezo wa kuvitawala viumbe vilivyomo katika mazingira yetu....

Huyo koboko mshamba tu ukiamua kucheza nae perpendicular...

Ziba mashimo yoote yaliyo karibu...
Deal nae muda ambao jua ni kali.
Vaa gunbut na nguo ya mikono mirefu...
Mwaga mafuta ya taa maeneo yke..

Tembeza kichapo heavy.. Utaleta mrejesho
We mpoteze mwenzako
 
Unavoongea its like mshkaji flani hivi aisee, huogopi??, sijawahi kumwona ila hilo jina imebidi nigoogle tena aisee joka hilooo. Mi ningehama kabisa mji uwiii, be careful mkuu, bado tunakuhitaji huku
 
Uwe makini sana, kuna mwenzako aliyewahi kumtafuta kama wewe. Alipofika Alipokuwa, akawa anachomachoma kwenya majani alipoingilia.

Akachoma mara ya kwanza, ya pili, ya tatu nyoka akapanda na fimbo yake iliyo mkononi na kumuumauma. Haikuchukuwa muda jamaa akavuta.

Kwa hiyo uliposema hivyo umenikumbusha yule marehemu.
Aisee, hatari sana
 
41 Reactions
Reply
Back
Top Bottom