Koboko (black mamba) ana kiburi, jeuri na dharau sana ila nitamfundisha adabu

Njemba Soro.

Njemba Soro.

JF-Expert Member
Oct 5, 2013
1,595
2,000
Habari za muda wandugu,

Huyu mpumbavu koboko kuna mahali ameamua kuhamia na sasa anaishi kama kwake, kila asubuhi nakuta yupo juu ya mti halafu anafoka sana na hataki nipite.

Sasa usiku huu narejea nakuta kachelewa kurudi halafu kanifokea tena na nimempotezea tu akatulia nikapita.

SASA KESHO NAHAKIKISHA ANAKUFA NA PICHA NITAWEKA HAPA MAANA NAONAANAVUKA MIPAKA HUYU MSHENZI.

ana speed sana na anapanda kwenye mti kwa kurukia matawi kama kima, yani hapandi kwa kutumia shina la mti, yeye anajiinua anasimamia mkia halafu anatega juu huko. Ukisikia fuuuuuuuuu....UJUE MSHIKAJI YUPO ILA KESHO NAKULA NAYE SAHANI MOJA.
 
Ahmad Abdurahman

Ahmad Abdurahman

JF-Expert Member
Mar 5, 2016
1,267
2,000
Vipi umeshamfundisha adabu Koboko huyo? Kama bado, mimi ninakushauri ufanye mojawapo ya mambo haya:
(a) Pulizia petroli eneo alipo; atakimbia na kabla hajafika mbali iwapo mvuke wa pteroli utamgusa basi atakufa polepole kulingana na wingi wa petroli iliyomgusa.
(b) Leta nguchiro kama watano hivi eneo alipo
(c) Tafuta jamaa wa maliasili-wanyamapori wadili naye
Heshima kwako mkuu. Sema lile jukwaa limepoa sana. Mijadala imepoa sana.

Vipi mbona kama huyu mleta mada hujamuelewa au mm ndo sijamuelewa?
 
kwenda21

kwenda21

JF-Expert Member
Mar 11, 2014
2,371
2,000
Mkuu usipate shida chuma tairi chini ya huo mti yeye akiwa Juu, au pilipili mwendo kasi
 
PROF NDUMILAKUWILI

PROF NDUMILAKUWILI

JF-Expert Member
Mar 25, 2016
9,253
2,000
Kuna kamnyama flani kako kama paka huwa kanamwazibu sana koboko na koboko akisha mwona tu hako kamnyama ujanja huwa unamwisha hivi huwa kanatumia njia gani kumwenyesha koboko?
 
Escaper

Escaper

JF-Expert Member
Nov 11, 2018
1,797
2,000
Kana speed na akili ya ziada, pia yupo mnyama mwingine hapati madhara ya sumu anang'atwa ila hafi.
Kuna kamnyama flani kako kama paka huwa kanamwazibu sana koboko na koboko akisha mwona tu hako kamnyama ujanja huwa unamwisha hivi huwa kanatumia njia gani kumwenyesha koboko?
 
Escaper

Escaper

JF-Expert Member
Nov 11, 2018
1,797
2,000
Wasikutisheeee...deal nae braza..

Binadamu tumepewa atashi mkubwa na uwezo wa kuvitawala viumbe vilivyomo katika mazingira yetu....

Huyo koboko mshamba tu ukiamua kucheza nae perpendicular...

Ziba mashimo yoote yaliyo karibu...
Deal nae muda ambao jua ni kali.
Vaa gunbut na nguo ya mikono mirefu...
Mwaga mafuta ya taa maeneo yke..

Tembeza kichapo heavy.. Utaleta mrejesho
We mpoteze mwenzako
 
financial services

financial services

JF-Expert Member
May 17, 2017
5,833
2,000
Unavoongea its like mshkaji flani hivi aisee, huogopi??, sijawahi kumwona ila hilo jina imebidi nigoogle tena aisee joka hilooo. Mi ningehama kabisa mji uwiii, be careful mkuu, bado tunakuhitaji huku
 
financial services

financial services

JF-Expert Member
May 17, 2017
5,833
2,000
Uwe makini sana, kuna mwenzako aliyewahi kumtafuta kama wewe. Alipofika Alipokuwa, akawa anachomachoma kwenya majani alipoingilia.

Akachoma mara ya kwanza, ya pili, ya tatu nyoka akapanda na fimbo yake iliyo mkononi na kumuumauma. Haikuchukuwa muda jamaa akavuta.

Kwa hiyo uliposema hivyo umenikumbusha yule marehemu.
Aisee, hatari sana
 
financial services

financial services

JF-Expert Member
May 17, 2017
5,833
2,000
Upo sehemu gani ili tunaogopa nyoka tusikaribie kabisa maeneo hayo?
Hahaa, kweli nimeshangaa anasema eti alikua anamfokea asipite. Mimi hata asingenifokea nisingekatiza kabisa hayo maeneo,nnavoogopa
 
black sniper

black sniper

JF-Expert Member
Dec 10, 2013
16,075
2,000
Mnaendeleza ubabe kwenye mitandao tu
Unavuta bangi unakuwa mpole lakini huyu anakula bangi ndio maana hata akikutana na mfu anagonga sumu tu
Nawapenda nyoka ila huyu ana ushetani na ni the most aggressive
Nafuga cobra shambani ila huyu anatisha
 
PROF NDUMILAKUWILI

PROF NDUMILAKUWILI

JF-Expert Member
Mar 25, 2016
9,253
2,000
Mnaendeleza ubabe kwenye mitandao tu
Unavuta bangi unakuwa mpole lakini huyu anakula bangi ndio maana hata akikutana na mfu anagonga sumu tu
Nawapenda nyoka ila huyu ana ushetani na ni the most aggressive
Nafuga cobra shambani ila huyu anatisha
Mkuu sababu ya kumfuga huyo Cobra ni nini?
 
Top Bottom