Koboko (black mamba) ana kiburi, jeuri na dharau sana ila nitamfundisha adabu

Njemba Soro.

JF-Expert Member
Oct 5, 2013
1,591
2,000
Habari za muda wandugu,

Huyu mpumbavu koboko kuna mahali ameamua kuhamia na sasa anaishi kama kwake, kila asubuhi nakuta yupo juu ya mti halafu anafoka sana na hataki nipite.

Sasa usiku huu narejea nakuta kachelewa kurudi halafu kanifokea tena na nimempotezea tu akatulia nikapita.

SASA KESHO NAHAKIKISHA ANAKUFA NA PICHA NITAWEKA HAPA MAANA NAONAANAVUKA MIPAKA HUYU MSHENZI.

ana speed sana na anapanda kwenye mti kwa kurukia matawi kama kima, yani hapandi kwa kutumia shina la mti, yeye anajiinua anasimamia mkia halafu anatega juu huko. Ukisikia fuuuuuuuuu....UJUE MSHIKAJI YUPO ILA KESHO NAKULA NAYE SAHANI MOJA.
 

Khantwe

JF-Expert Member
Dec 20, 2012
51,706
2,000
Mwanzoni mwa uzi nilijua anasemwa mtu ila nimepitia hadi comments naona koboko kweli ila sijui, ngoja niendelee kusoma
 

Frank Wanjiru

JF-Expert Member
Apr 12, 2012
13,428
2,000
Zamani sana niliwahi kumkuta kwenye ka kichaka fulani hivi lakini nilikuwa cjajua kama ni yeye, nikaanza kumrushia mawe na fimbo yeye akawa anajirudisha nyuma na mi namfuata, ghafla nikastukia nanyakuliwa navutwa kwa nguvu kurudishwa nyuma, wakati bado nashanga shangaa nikatulizwa na vibao viwili matata sana, akili kuja kukaa sawa nikamsikia aliyenivuta anasema (mama mmoja hivi hata simjui) we mtoto mjinga sana, hivi KOBOKO ni kuchezea hivyo unadhani huyo ni kifutu eeh (KIFUTU ni yale manyoka manene ambayo ni nadra sana kukuuma, lakini likikuuma unaoza kwa haraka sana kuanzia pale ulipoumwa)

Kumbe lile dude wakati linarudi nyuma lilikuwa limeshakasirika, basi ile jioni tukasikia kwenye ka kichaka kalekale mbuzi 12,ngombe 2, kondoo 4 na mchungaji wao walikuwa wamepoteza maisha, basi yule mama aliyeniokoa pale kimiujiza akaja kusema nyumbani......nikajikuta nachezea kipigo kizito kutoka kwa mama, halafu baadae ndio akanipa darasa kuhusu hilo DUBWASHA......ndugu yangu wewe nakusihi tu ungeachana na huo ujinga unaotaka kujaribu kuufanya
Mkuu naona umerudi kivingine, karibu sana
 

Mr Miller

JF-Expert Member
Jan 24, 2017
11,187
2,000
Akikugonga ukafa...utuletee na mrejesho pia...

Huyo jamaa hachezewi wala hataniwi...ukisema upambane nae...utakufa wewe yeye atabaki...
Huyu mnyama ni bora umsikie tu,, na ukijaribu kumchokoza yatakayokukuta huu yako
Mkuu hao viumbe sio wamchezo angalia asikudhuru hataniwi muache tu
Uwe makini sana, kuna mwenzako aliyewahi kumtafuta kama wewe. Alipofika Alipokuwa, akawa anachomachoma kwenya majani alipoingilia.

Akachoma mara ya kwanza, ya pili, ya tatu nyoka akapanda na fimbo yake iliyo mkononi na kumuumauma. Haikuchukuwa muda jamaa akavuta.

Kwa hiyo uliposema hivyo umenikumbusha yule marehemu.
Umeandika wosia?
Alete na picha anapoenda kuzikwa baada ya kugongwa na huyo kiumbe.
Hao viumbe hawanaga utani kabisa...
Ushauri tafuta watu wa maliasili wadili nae. Ni hatari mkuu.
Hii koboko nyoka kweli au mambo ya codes
aisee mbona mnamtisha sana?
 

carter

JF-Expert Member
Jan 23, 2009
3,082
2,000
Uwe makini sana, kuna mwenzako aliyewahi kumtafuta kama wewe. Alipofika Alipokuwa, akawa anachomachoma kwenya majani alipoingilia.

Akachoma mara ya kwanza, ya pili, ya tatu nyoka akapanda na fimbo yake iliyo mkononi na kumuumauma. Haikuchukuwa muda jamaa akavuta.

Kwa hiyo uliposema hivyo umenikumbusha yule marehemu.
Kwa Hiyo una mpa ushauri gani huyu...... mtarajiwa? (Kama akienda kumchokoza kweli lakini)

Ila akienda akiwa anapuliza lile jana la Mh kasheku na mzee wa imalaseko anaweza kushinda hiyo vita kiulaini.
 

DsmicSound

JF-Expert Member
Dec 26, 2015
1,562
2,000
Duuuuuh..mkuu kuwa makini..huyo kiumbe msikie tu
Mimi nilipo kwasasa ni nje ya mji na hao jamaa wanaishi jirani tu kama mita 200 kutoka kwenye makazi ya watu...kuna mchunga ng’ombe alipita na mifugo yake ikawa kero kwa wajomba ..huwezi amini baada ya dakika 40 ng’ombe 20 walikuwa walipotoka kabla hawajaja duniani..
Koboko mmoja anaweza akang'ata watu 100, mmoja baada ya mwingine...na wala asichoke...lbd mkimbie wenyewe...
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom