Koboeni mahindi muondoe sumu

real G

JF-Expert Member
Feb 7, 2013
5,227
5,287
Shirika lisilo la kiserikali la World Vision limesema kuna umuhimu wa kukoboa mahindi ili kuondoa sumu zenye athari kwa binadamu.

Akizungumza katika mkutano wa wazalishaji hao jana, meneja mradi wa urutubishaji vyakula wa World Vision, Symphrose Uisso alisema: “Kwanza uhifadhi wa mahindi katika nchi yetu uko duni sana. Matokeo yake mahindi huota sumu ambayo ni hatari kwa afya ya binadamu kwani inaweza kusababisha saratani. Vilevile viuatilifu vinavyotumika kuzalisha na kuhifadhia nafaka vina madhara.“Baada ya kukoboa mahindi tunayo teknolojia ya kuongeza virutubisho vinavyokosekana kwenye unga wa mahindi,” alisema.

Shirika hilo pia linakamilisha mchakato wa kuwafadhili wazalishaji na wasambazaji wa unga wa mahindi jijini Dar es Salaam mashine za kuongeza virutubisho.
 
Ndiyo...hata karanga zilizoanza kuharibika na kutengeneza rangi/blue ni hatari pia inaweza kuwa chanzo cha saratani. Watu waelewe ukweli huu na wachukuwe hatau. Tunapaswa tule chakula kisicho na sumu.
 
Hata panya hushambulia mahindi kwa kula hicho kiini lishe ambacho ukiyakoboa unakipoteza. Watuachie dona letu tutaendelea kuosha mahindi kabla ya kuyasaga.
 
Sasa mbona wataalamu wa Afya huwa wanatushauri sana kutumia Dona badala ya Sembe ambayo haina faida ktk ustawi wa afya zetu? Haya sasa ona wataalam hawa wengine wanatushauri tutumie unga uliokobolewa. Sijui tufuate lipi !!
 
Huyu jamaa atatupotosha. Badala ya kuleta teknolojia ya kuongeza virutubisho angeleta teknologia ya kuhifadhi mahindi. Hatukoboiiiiiiiiiiiii tunakula dona. Pakua hiyo picha kisha nenda Moshi utawakuta barabarani kama km 10 baada ya njia panda ukielekea Moshi.
upload_2016-6-30_13-58-47.jpeg
au google www.riela.co.tz/
 
Attachments

  • riela.jpg
    riela.jpg
    11.2 KB · Views: 54
Sasa mbona wataalamu wa Afya huwa wanatushauri sana kutumia Dona badala ya Sembe ambayo haina faida ktk ustawi wa afya zetu? Haya sasa ona wataalam hawa wengine wanatushauri tutumie unga uliokobolewa. Sijui tufuate lipi !!
Hii dunia bana ukisoma sana unaweza ukawa chizi yaani full of contradictions.. Leo tena dona imekuwa na madhara kwa binadamu halafu kunguruwe anapata afya isiyo na shaka kwa kula zile pumba.
 
Sasa mbona wataalamu wa Afya huwa wanatushauri sana kutumia Dona badala ya Sembe ambayo haina faida ktk ustawi wa afya zetu? Haya sasa ona wataalam hawa wengine wanatushauri tutumie unga uliokobolewa. Sijui tufuate lipi !!
Issue ni maandalizi....mahindi yamekaa ghalani mwaka mzima yanapuliziwa dawa wewe ukasage tu ule ni hatari.
 
Back
Top Bottom