Kobe wa ajabu anayepindua gari

Ngongo

JF-Expert Member
Sep 20, 2008
18,894
31,106
Kobe mkubwa anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka zaidi ya 120, (pichani), bado anaendelea kuishi kwenye shamba la kahawa la Kibo na Kikafu, Wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro.
Kobe huyo anadaiwa kuwa na nguvu kubwa kiasi cha kuweza kuangusha hata baadhi ya vitu likiwemo gari.
Inadaiwa kwamba kobe huyo amekuwepo katika shamba hilo tangu enzi za ukoloni kabla ya Tanzania haijapata uhuru.
Meneja wa shamba hilo lenye ukubwa wa ekari 2,054, Jackson Matenge, alisema kobe huyo anajulikana kwa jina la Tony na kwamba hivi karibuni alionyesha uwezo wake baada ya kulipindua lori la tani saba na kusababisha ajali.
Alisema kobe huyo alikuwa amelala barabarani ambapo lori hilo liliegeshwa mahali alipokuwepo na aliponyanyuka, alilipindua lori hilo lakini hakuna mtu aliyepoteza maisha wala kujeruhiwa.
Naye Mwenyekiti wa Vyama vya Msingi vya Masama Saawe, Modio na Masama, Roo na Sonu Ngira, Hatibu Mwanga, alisema mwaka 1952 akiwa na umri wa
miaka minne, walikuwa wakicheza na kobe huyo akiwa mkubwa kama alivyo na kwamba hadi sasa ana miaka 58 lakini bado ana nguvu.
Alisema wakoloni waliokuwa wanamiliki shamba hilo kabla ya serikali kuyataifisha mwaka 1975, ndio waliomuweka shambani humo ambapo baada ya kuondoka walirudi na kutaka kumnunua kwa zaidi yaSh. milioni 100 lakini wanachama walikataa na kudai kuwa hiyo ni sawa na hirizi ya shamba hilo.
Alisema wazungu hao walirudi tena na kuomba kuuziwa kobe huyo lakini bado walikataliwa na kwamba idadi kubwa ya wazungu hufika katika shamba hilo kwa ajili ya kumuona kobe huyo na kupiga naye picha.
Kwa upande wake, Mkuu wa wilaya hiyo, Dk. Norman Sigalla aliutaka uongozi wa shamba hilo kumjengea mazingira mazuri ya kuishi kobe huyo ili aweze kutumika kama sehemu ya utalii kwa watalii wa ndani na nje.
CHANZO: NIPASHE

Duh hii kali wanaoishi karibu na hilo shamba tunaomba habari za huyu kobe



moz-screenshot.jpg
 

Attachments

  • Kobe.jpg
    Kobe.jpg
    18.9 KB · Views: 302
haya ni maajabu ya dunia Kobe mwenye uwezo wa kupindua loli ?

Tanzania watu wanaathiriwa sana kutamka matamshi kutokana na asili ya mtu atokapo.Kwa mfano watu watu wa kanda ya ziwa hasa mkoa wa Mara mahali pa l wenyewe wanaweka r.watu wa pwani mahali pa r waweka l,labda First lady anatoka maeneo ya pwani tumsaidie badala ya kumkejeli.




Hapa umesaidia nini?.
 
Hilo la umri pengine ni kweli.
There are many old wives tales about the age of turtles and tortoises, one of which being that the age of a tortoise can be deduced by counting the number of concentric rings on its carapace, much like the cross-section of a tree. This is not true, since the growth of a tortoise depends highly on the access of food and water. A tortoise that has access to plenty of forage (or is regularly fed by its owner) will grow faster than a Desert Tortoise that goes days without eating.

Tortoises generally have lifespans comparable with those of human beings, and some individuals are known to have lived longer than 150 years. Because of this, they symbolize longevity in some cultures, such as China. The oldest tortoise ever recorded, almost the oldest individual animal ever recorded, was Tu'i Malila, which was presented to the Tongan royal family by the British explorer Captain Cook shortly after its birth in 1777. Tui Malila remained in the care of the Tongan royal family until its death by natural causes on May 19, 1965. This means that upon its death, Tui Malila was 188 years old.

Source: Wikipedia


Inapokuja kupindua gari ya tani saba, pengine tunahitaji uthibitisho zaidi.
 
Wakuu, kupindua gari?? kama ni mboga ya kwenye bakuli imetiwa chumvi mfuko mzima atii,
 
Hilo la umri pengine ni kweli.


Inapokuja kupindua gari ya tani saba, pengine tunahitaji uthibitisho zaidi.

Heshima kwako SMU,

Kwanza nakushukuru kwa kujaribu kutulea data zaidi kuhusiana na umri anaoweza kuishi kobe.

Kuhusu kupindua lori tani saba nadhani pia inawezakana,kama ukisoma habari yenyewe kwa umakini utabaini gari lilipinduliwa kwasababu lilikuwa limeengeshwa sehemu kobe aliyokuwa amepumzika/kalala.Kobe anapokuwa amelala anaingiza kichwa na miguu ndani ya gamba lake anapoamka anatoa kichwa na miguu ili aweze kutembea kitendo cha kuanza kutembea lazima kitaongeza urefu na kama kuna kitu juu yake [Lori] lazima litanyanyuliwa.
Nikiri kwamba hata mimi nilipoiona hii story kwa mara ya kwanza akili yangu iligoma kukubaliana hili jambo linawezekana lakini baada ya kutafari sana nikagundua ni kitu kinachowezekana.
 
heshima kwako smu,

kwanza nakushukuru kwa kujaribu kutulea data zaidi kuhusiana na umri anaoweza kuishi kobe.

kuhusu kupindua lori tani saba nadhani pia inawezakana,kama ukisoma habari yenyewe kwa umakini utabaini gari lilipinduliwa kwasababu lilikuwa limeengeshwa sehemu kobe aliyokuwa amepumzika/kalala.kobe anapokuwa amelala anaingiza kichwa na miguu ndani ya gamba lake anapoamka anatoa kichwa na miguu ili aweze kutembea kitendo cha kuanza kutembea lazima kitaongeza urefu na kama kuna kitu juu yake [lori] lazima litanyanyuliwa.
nikiri kwamba hata mimi nilipoiona hii story kwa mara ya kwanza akili yangu iligoma kukubaliana hili jambo linawezekana lakini baada ya kutafari sana nikagundua ni kitu kinachowezekana.

hivi kweli ana nguvu kiasi cha kupindua kilo elfu saba?
Je mifupa yake ni calcium au chuma cha pua?
 
Back
Top Bottom