Serikali Yaagiza TRA Kuchunguza NGO's Zinazofanya Biashara na Kuimarisha Mazingira ya Uwekezaji

mstahiki

JF-Expert Member
Jul 14, 2007
308
5
Serikali imeiagiza Mamlaka ya Mapato Nchini (TRA) kuzifanyia uchunguzi wa kina asasi zisizo za kiserikali (NGO`s) zinazosamehewa kodi kwa kuwa baadhi yao zinafanya biashara.

Aidha, imeiagiza Mamlaka hiyo kulegeza masharti ya kutoa vibali kwa wawekezaji wapya ili kuwavutia kuwekeza ikiwa ni njia ya kuongeza walipa kodi.

Maagizo hayo yalitolewa na Rais Jakaya Kikwete jana jijini Dar es Salaam wakati akifunga maadhimisho ya pili ya Siku ya Walipa Kodi nchini iliyoandaliwa na TRA.

Akizungumzia misamaha ya kodi inayotolewa kwa baadhi ya asasi hapa nchini kama vile vituo vya kulelea watoto yatima, Rais alisema kuna haja ya kuzichunguza kwa kina na zile zinazofikiriwa kupewa.

Alisema nyingi ya asasi hizo zinafanya biashara kwa kuwatumia watoto yatima badala ya kutoa huduma.

Alitoa mfano wa asasi moja ya kulelea watoto yatima ya Manyoni mkoani Singida kwamba ilipata msamaha lakini iliagiza tani nyingi za sukari kutoka nje na badala ya kuwahudumia watoto hao, ilikutwa Makambako ikitafutiwa wateja.

Kuhusu wawekezaji, Rais Kikwete lisema kumekuwa na urasimu wa kuwasajili wawekezaji, hali inayowakatisha tamaa na kusababisha kuwepo kwa upungufu wa idadi ya walipa kodi wakubwa.

Mamlaka hiyo imetakiwa kupanua wigo wa kuwavutia wawekezaji na kupunguza vikwazo vya kuanzisha biashara nchini.

Rais Kikwete alisema pamoja na Mamlaka hiyo kuongeza idadi ya mapato inayokusanya, lakini isibweteke kwani bado mapato hayo hayatoshi kwa serikali kufikisha huduma za kijamii kwa Watanzania.

`Pesa ya serikali sitaki ichezewe kabisa, fedha hiyo ni kwa ajili ya kupeleka maendeleo kwa wananchi, lazima mhakikishe kila senti ya mlipa kodi inafanya kazi iliyokusudiwa.

Kwa hili sina mchezo,` alisema na kuongeza Mheshimiwa Waziri (Waziri wa Fedha, Bi. Zakia Meghji) usichelee kuniambia mahala penye tatizo, kama mtu anakuzidi kimo, mimi hakuna anayenizidi, Rais alisisitiza.�

Aidha, ameiagiza pia mamlaka hiyo kuharakisha kurasimisha mali za wanyonge ili ziweze kutambulika kisheria na kumfanya aweze kutumia rasilimali yake kukopa kwenye benki na taasisi nyingine za kifedha.

Awali mwakilishi wa walipa kodi nchini Bw. Elisante Muro, alisema TRA imeboresha huduma zake kiasi kwamba hata walipa kodi hawaoni kufanya hivyo kama kero.

Aliipongeza kwa kufanya kazi kwa haraka hasa ya kuondoa mizigo bandarini, lakini akaishauri TRA kushirikiana na asasi nyingine ili kuharakisha zaidi utoaji wa mizigo ya wateja.

Aliiomba serikali kuongeza muda wa kodi inayolipwa hadi miaka mitano, badala ya kila mara kupandisha kodi, hali aliyosema inawadhoofisha wafanyabiashara na biashara zao.

Mwakilishi huyo pia aliomba Kodi ya ongezeko la Thamani (VAT) ipunguzwe kutoka asilimia 20 hadi 15.5 ili viwango hivyo vilingane na vya nchi jirani.

Naye Kamishna Mkuu wa TRA, Bw. Harry Kitilya, alisema mfumo wa ukusanyaji kodi umeboreshwa kiasi kwamba walipa kodi wamekuwa rafiki wa TRA tofauti na zamani inafikia hata wafanyabiashara kufungiwa biashara zao.

Waziri wa Fedha Bi. Meghji alisema, TRA imetia fora kwa ukusanyaji wa mapato yaliyofikia Sh. bilioni 320 kwa mwezi Septemba mwaka huu.

Hata hivyo, alisema kwamba wanatarajia kuvunja rekodi ya ukusanyaji katika miezi ya Desemba mwaka huu, Machi na Juni mwakani.

Aidha Rais pia alitoa tuzo kwa kampuni zilizoshinda kwa kulipa kodi.

Vigezo vilivyoshindaniwa ni kwa mfanyabiashara anayetunza kumbukumbu vizuri, kiwango cha kodi, ulipaji mzuri usio na usumbufu, uaminifu wa kulipa kwa wakati na uwasilishaji kodi muda muafaka.

Aidha mfanyabiashara mwenye kesi na TRA mahakamani au anafanyiwa uchunguzi wa masuala ya kodi, hakuwa na sifa ya kuingia katika ushindani huo.

Washindi kumi wa kitaifa walitajwa kuwa ni Benki ya CRDB, kiwanda cha sukari cha Kilombero, Benki ya NBC, Benki ya NMB, Songas, benki ya Standard Charter, kampuni ya Sigara (TCC), TANESCO, Mamlaka ya Bandari Tanzania, na Kiwanda cha Saruji cha Wazo.

SOURCE: Nipashe

Tuma Maoni Yako
 
TANESCO wanapata hasara na bado wanalipa kodi kubwa kiasi hicho kwanini?

Wanalipa kodi kisha wanapata ruzuku, kuna faida hapo kweli?
 
Mtz hata mimi hii ya Tanesco imenishangaza sana, nimerudia huo mstari mara mbilimbili.Labda tungepata na figs kwamba wamelipa ngapi ingetoa picha pana zaidi.Lakini ni moja ya shirika lenye matatizo makubwa kuanza hapo nyuma mpaka navyoandika sasa hivi.Lakini kama wamo kwenye walipaji 10 makini basi wale 5.
 
TANESCO wanapata hasara na bado wanalipa kodi kubwa kiasi hicho kwanini?

Wanalipa kodi kisha wanapata ruzuku, kuna faida hapo kweli?

TANESCO iko kwenye category ya overall winner, ambayo ni kutokana na vigezo kama vitano hivi,,, ngoja ni jaribu kama nakumbuka.

1. Kodi kubwa.
2. Kulipa kwa wakati.
3. Kutokua na query ya kodi.
4. supporting document zinapohitaji zinapatikana kwa urahisi etc..


Sidhani kwamba wanalipa Hela nyingi lakini ni waadilifu, au ni marafiki wa TRA, hawafichi kitu....

Hii mara nyingi inasababishwa na kuwa na watu wazuri kwenye idara ya Uhasibu....

Hurreee TANESCO, na Hongera kwa Washindi Wote especially Mshindi wa Kwanza!!!


Tunasikitika,,, kwamba SUMARIA GROUP, METL, BAKHRESA & CO. IPP never featured out!!!
 
Kilitime, kwa mtaji huu uliotaja hapo juu, hata biashara yangu ingestahili kupewa tuzo! Maana vigezo hivyo vitatu ulivyotaja hata sisi tunafit!;)

Mi nadhani haitoshi kusema wana vigezo hivyo kama kodi wanayolipa si kubwa.

Akina METL na Bakhresa naomba wafuatiliwe na tupate sababu za wao kutoingia katika walipaji kodi wakubwa, wakati tunasikia wanatesa mpaka nchi jirani eti wamekuwa regional players! Alafu unakuta Mohamed Dewji ni mbunge! Jamani Bongo yetu!
 
TANESCO kulipa kodi kubwa inatokana na majumuisho ya aina zote za kodi. Hii ni pamoja na ile :

- inayolipwa na wateja k.m. VAT, service charges
- inayolipwa na wafanyakazi k.m. PAYE

Hapo sifa kubwa kwa TANESCO ni kuwasilisha makato kama inavyotakiwa na kwa wakati mwafaka.
Just imagine, (formerly at Mdaula kwi, kwi, kwi) kwenye kila unit ya umeme inayotumika kuna 20% VAT. Kwanini makusanyo yasiwe makubwa!!

Sidhani kama TANESCO inalipa Corporate Tax kutokana na hasara inayopata kila mwaka.
Lakini, kubwa la kujiuliza: IPTL inayolipwa billions na TANESCO kila mwaka kwa kazi isiyofanya au kwa gharama kiduchu, inalipa kiasi gani cha kodi kwa serikali?
Hivyo hivyo kwa makampuni ya serikali yaliyobinafsishwa k.m. TICTS ( Container Terminal). Ilinganishwe kodi wanayolipa kwa sasa na kiasi Serikali ilichokuwa ikikusanya hapo awali kama kodi na dividends. Hii itatuwezesha kujua vizuri effects za privatisation kwenye pato la Taifa.
 
Wakuu,

Haya magroup of companies ni wajanja sana huwa wanafomu kampuni kibao (21st Century, Nabico, East Coast Oils and Fats, Mo Cashewnuts, Tradeco Soaps Industries, n.k.). Hayo makampuni yote ni ya Mohamed Enterprises (METL Group). Lakini wanakuwa wanafile different tax returns kwa kila kampuni. Hawawasilishi consolidated account za group, hivyo wanapoona turnover ya kampuni moja inakuwa wanaunda kampuni nyingine. Kuwemo kwenye TOP 10 ni ndoto, na hii inatumika kwa magroup yote kama Sumaria, Bakressa, Murzah Oil, n.k.

Sijui kwa nini TRA hawalioni hili?
 
TANESCO kulipa kodi kubwa inatokana na majumuisho ya aina zote za kodi. Hii ni pamoja na ile :

- inayolipwa na wateja k.m. VAT, service charges
- inayolipwa na wafanyakazi k.m. PAYE

Hapo sifa kubwa kwa TANESCO ni kuwasilisha makato kama inavyotakiwa na kwa wakati mwafaka.
Just imagine, (formerly at Mdaula kwi, kwi, kwi) kwenye kila unit ya umeme inayotumika kuna 20% VAT. Kwanini makusanyo yasiwe makubwa!!

Sidhani kama TANESCO inalipa Corporate Tax kutokana na hasara inayopata kila mwaka.
Lakini, kubwa la kujiuliza: IPTL inayolipwa billions na TANESCO kila mwaka kwa kazi isiyofanya au kwa gharama kiduchu, inalipa kiasi gani cha kodi kwa serikali?
Hivyo hivyo kwa makampuni ya serikali yaliyobinafsishwa k.m. TICTS ( Container Terminal). Ilinganishwe kodi wanayolipa kwa sasa na kiasi Serikali ilichokuwa ikikusanya hapo awali kama kodi na dividends. Hii itatuwezesha kujua vizuri effects za privatisation kwenye pato la Taifa.


Hivi ule mpango wa kununua IPTL umefikia wapi kwa serikali?
TANESCO wangeweza hata kuwa wa kwanza kulipa kodi VAT, sema wateja wangi sana hawalipi umeme- haswa vijijini huwa wanaiba!
 
huyu mdudu anayeitwa PAYE namchukia sana sana sana!!!

Wenzetu wanaendelea shauri ya huyo mdudu.

Laiti tungefanikiwa kuwafanya Watanzania wengine kama milioni 5
wakapata ajira na kukatwa kama 10,000 kwa mwezi, hizo ni bilioni 50, tunaweza kujenga hospitali moja kwa kila mkoa kwa kila mwezi.

Wachina na Wahindi wamegundua kuwa na watu wengi sio liability bali ni asset.
 
huyu mdudu anayeitwa PAYE namchukia sana sana sana!!!

Huyu mdudu ni mzuri sana the only problem anamtesa mlipakodi mtiifu tu kuliko yeyote hapo TZ naye ni mfanyakazi...

Kama walipakodi wengine wangelipa kama huyo mdudu walahi tungekuwa mbali sana.
 
Tanzania tumekuwa hatujali au ni ujinga hata sielewi, huu mtindo wa wafanya biashara kubwa kubwa kutokulipa kodi katika mauzo sio mgeni tena kwa uwazi kabisa. Wafanya biashara kwenye maduka yao kila wanachouza hawawezi kutoa jibu sahihi kwamba wamekilipia kodi sahihi.

Maendeleo hayawezi kuja wakati kuna kundi kubwa la wafanya biashara ambao hawataki kulipa kodi kwa makusudi au kukwepa. Nani amefungwa kwa kutokulipa kodi sahihi? Sheria hazina meno tunategemea wataalam kutoka Norway waje watusaidie sijui watafika lini?

Kwa mimi the best tax payers ni wale wanaolipa PAYE.
 
ni ajabu sana kama bakhresa kwenye top ten hajatokea ..wakati kati ya makampuni yanayouza nchi hii ukitoa TBL na sigara, wanafuatia wauzaji wa vyakula BAKHRESSA FOOD PRDUCTS,MOHAMED ENTERPRISE,ZAKARIA...sichangae j.shah na sumaria yake kuytotokea kwa sababu investment yake kubwa ipo kwenye viwanda vya madawa..ukiacha vya plastics na sabuni...inabidi TRA wafanye research ya kuwatambua wakwepaji KUMI BORA WA KODI[WAKUBWA].....
Kweli bakhressa na ucha mungu wake anakwepa kodi au?? kule uganda ,malawi,kenya,msumbiji AMABAKO amewekeza viwanda wakisikia yeye kwenye kumi bora walipa kodi hayumo watatucheka sana...na ataonekana si MZALENDO kwa kuwa tumemuona akijichumia utajiri wake hapa kwa pesa zetu wateja....ndani ya miaka 15 kwa kasi.ya ajabu ...anao wajibu wa kuanza kulipa fadhila kwa kulipa kodi kihalali...
 
Hata hivyo si haba ukilinganisha na tulikotoka kwenye Bilioni 25 1995 hadi bilion 320 Sept 07. Laiti kama Serikali ingepunguza matumizi yasiyo ya lazima (Safari za Rais na ujumbe lukuki nje ya nchi, ziara za mawaziri mikoani, Ununuzi wa magari ya fahari, Ukubwa wa baraza la mawaziri, ufisadi n.k) I hope pesa hii ingepunguza kwa kiasi kikubwa utegemezi kutoka nje.
 
[QUOTE=Saharavoice;102054]Hata hivyo si haba ukilinganisha na tulikotoka kwenye Bilioni 25 1995 hadi bilion 320 Sept 07.

Ongezeko hili, ukilichunguza kwa makini ni kiini macho.

Kilichotokea mwanzoni wa miaka ya 2000 ni Serikali na taasisi zake kuanza kulipa kodi. Tofauti na miaka ya nyuma ambapo kulikuwa na blanket exemptions. Hii ilisababisha kupanda kwa ulipwaji kodi kwani:

-Serikali ndiye mnunuzi mkubwa hapa nchini. Piga-ua, hapa malipo ya VAT (+ other Duties) lazima yapande astronomically. Fikiria VAT ya shangingi moja halafu zidisha kwa mashangingi yaliyopo barabarani and u will see the impact.Hii ni kwa item moja. Fikiria zingine 10 - including ujenzi mbalimbali!
-Serikali ndiye mwajiri mkuu. Ongezeko la wafanyakazi na mishahara lina maana ya ongezeko la kodi.

Lakini, huu ni mzunguko tu wa pesa kutoka mkono wa kushoto kwenda wa kulia. Sioni kwamba ni ongezeko la pato kwa Serikali.

Ongezeko la kodi lingekuwa na maana zaidi kama lingekuwa kwa kodi kama Export Duties, Import & Excise Duties, Corporate Taxes (kama hizo za TCC, TBL etc).
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom