KNCU na shamba na nyumba zake - CCM kwenye kashfa nzito Kilimanjaro

dira

Member
Jun 8, 2012
18
1
Pamoja wizara ya kilimo kutangaza wazi kuwa nyumba za kampuni ya kukobolea kahawa hazitauzwa wala mashamba ya kncu, tayari taarifa zimeenea katika mji wa moshi ya kuwa alienunua nyumba ya tccco iliyoko moshi mjini tayari ameshalipa fedha zote pamoja na kwamba wizara inayoongozwa na waziri chiza kusema asilipe fedha hizo baada ya kikao kilichokaa dodoma hivi karibuni.

Habari hizo zinaeleza kuwa baada ya kuona amebanwa katika kikao cha dododma kati ya naibu waziri godfrey zambi mwenyekiti wa kncu aliporudi moshi alimwambia alienunua nyumba hiyo alipe fedha zote ili apate nafasi ya kufanya madai yake mahakamani.

Habari hizo zinaeleza ya kuwa mnunuzi huyo aliwasiliana na wakili maarufu wa moshi elizabeti minde ambae pia ni mwenyekiti wa ccm moshi vijijini ambae kwa kushirikiana na mbunge wa moshi vijijini sirili chami walimwambmia alipe fedha hizo na kwamba kwa vyovyote vile hata raisi hana mamlaka ya kuzuia tccco isiuze mali zake

Pia taarifa hizo zinaeleza kuwa wakili huyo ambae pia ni mwenyekiti wa ccm wilaya ya moshi mjini ameiandikia barua kncu kuhakikisha inampa mnunuzi huyo hati yake baada ya siku 7 na kama hawatafanya hivyo wataanza kuitoza kncu riba

Habari zaidi zinasema kuwa chama cha mapinduzi kina mkono wake kwenye mauzo ya nyumba hiyo pamoja na shamba la garagagua ikiwa ni njia ya kupata fedha za uchaguzi mwaka 2015. Ndiyo maana hata kuhusu kuuzwa shamba la garagagua mbunge wa moshi vijijini anamekana ndiye alikwenda hadi kwa mkuu wa mkoa wa kilimanjaro na kumshawishi akubali liuzwe kwa mnunuzi ambae tayari ashajulikana na ni mweka hazina wa ccm wilaya ya moshi vijijini sirili mushi

Inasmekana chami, wakili minde na sirili mushi wamemzidi waziri chiza nguvu kwa kuwa wanamawasiliano na vigogo wa ccm ngazi ya taifa ambao wanahakikisha mali hizo zinauzwa kwa manufaa ya ccm. Habari zingine zinaeleza kuwa shamba hizo linasemekana kuwa lina la ekari 5,000 na si 3,000 kama inavyodaiwa na uongozi wa kncu na hii ni baada ya vigogo wa ccm kugawana sehemu ya shamba hilo akiwemo mfanya biashara felix mosha wa daressalaam

Pia kuna taarifa kuwa mwenyekiti wa kncu menad swai amekula rushwa ya shilingi milioni 5 kutoka kwa mnunuzi wa nyumba ya tccco ya moshi mjini na kwamba kutokana na hali hiyo baadhi ya wajumbe wa bodi ya kncu na meneja wake mkuu wamegundua sababu ya mchakato wa kuuzwa kwa nyumba za tccco na shamba la gararagua limeshughulikiwa na mwenyekiti huyo badala ya kutumia taratibu za kawaida

Pia inasemekana sababu ya waziri chiza kutokuingilia swala hilo badala yake anamwachia waziri mdogo zambi ni kwa kuwa kncu waliifanyia ukarabati nyumba yake kwa dhamani ya shilingi milioni 200 sasa ukichanganya shinikizo la ccm, wakili minde, chami na mushi anakuwa hana ujanja


Hali hii imezua tafarani kubwa kiasi cha kwamba tayari wana ccm wenye sauti na nafasi kubwa ndani ya chama hicho wakiwemo madiwani kutoka wilaya za siha, hai, moshi vijijini na siha wamejitayarisha kujitoa kutoka kwenye chama hicho tena mbele ya katibu mkuu wa chama kinana wakati atakapotembelea mkoa wa kilimanjaro hivi karibuni


Wamesema wao ambao tayari washajiunga tayari kujitoa wataweka historia kwa kurudisha kazi zao ccm kupitia katibu mkuu huyo tofauti na wengine ambao huwa wanarudisha kwa wapinzani. Habari kutoka ndani ya wapinzani wakubwa wa ccm chadema zinaeleza tayari wameandaa mkutano mkubwa wa kuzungumzia swala hilo na ambapo watapitusha azimio ya kuwa mali hizo hazitauzwa kwa vile ni za wananchi na kwa wale ambao watakuwa washalipa fedha zao kwa chochote walichonunua kutoka kwa ushirika kncu itazirudisha kwa nguvu ya umma kabla viongozi hao wa chadema hawajaondoka moshi

Cha kushangaza ni kuwa di ra kupitia mtandano huu huu wa jamii forum ilishazungumzia ya kuwa kncu itawauzia hawa hawa walionunua mali hizi yaani nyumba ya tccco na shamba la gararagua na ndiyo hao hao walionunua.

Pia dira ilizungumzia ya kuwa kuna mkono wa chami, mweka hazina wa ccm moshi vijijini na ccm kwa ujumla lakini hakuna mtu alifuatilia hilo, sasa yametokea kama ilivyo ripotiwa na dira kwenye mtandao wa jamii forum na mmoja wa wanunuzi ni mweka hazina wa ccm yenyewe na tunaambiwa hata raisi hawezi kutoa maamuzi yoyote ya kubatilisha
 
Tumeshachoka kusikia uozo wa huu uozo wa ukoo wa panya. Najiuliza kwanini nisibebe rpg yangu!
 
Yaani kusema ukweli WACCM ifike mahali waone aibu! Wakeiba kila kitu, Wamefisadi kila kitu! Vyama vyote vya Ushirika, Mashirika makubwa ya Uma, Mamlaka na miradi mingi wamefanya vitoweo na familia zao. KNCU hii iliyoliwa ikabaki mifupa ndo wanamalizia kuchukua kila kitu. Tutafunga safari tukalipue watu hata kwa mtutu wa bamboo. kwa kweli! Ni aibu sana kuwa Mwanaccm. Ni fedheha sana kusimama na kujisifu wewe ni CCM katika hali hii. Ndo maana mnatumia hila zote ili mambo yasigundulike. Hilo shamba lindegawiwa wananchi wa mkoa huo ambao ni wanachama wa KNCU ambao hawajapata faida yoyote kutokana na uanachama na KNCU na sio kuuzwa. Wananchi waliochangia KNCU wanapata nini hapo? Ndo waliokamuliwa miradi ya KNCU ikaanzisha, therefore ni wamiliki halali wa KNCU, iweje CCM wasione hili! UKOO WA PANYA unaiba mpaka visivyoibiwa. Hili la KNCU ni SUMU na Mtakufa na ulafi wenu.
 
Hivi kumbe na watu wa Moshi mnaweza kuibiwa kirahisi na CCM? Poleni sana wakulima wa kahawa huko Kilimanjaro
 
CCM wanakula kila kitu hata mikono hawataki kunawa,....
 
Kashfa kwenye nzito Kilimanjaro ndo nini?

Rekebisheni heading!
 
Elizabert Maro Minde ndo yule aliyemfunga mumewe,ni wakili na mwenyekiti wa CCM Moshi Mjini na ndo Mwenyekiti na Bodi Mamlaka ya Majisafi na taka Moshi Mjini(MUWSA) leo amegeuka kuwa mtetezi wa haki za binadamu,majanga
 
Back
Top Bottom