KMC FC Vs Simba SC (0-2) | Dimba la Benjamin Mkapa | Vodacom Premier League VPL

Ghazwat

JF-Expert Member
Oct 4, 2015
23,718
66,262
Patashika ya Ligi Kuu Tanzania Bara Vodacom Premier League (VPL) Kuendelea kupigwa leo July 7, 2021 ambapo Kinondoni Municipal KMC FC, wanawakabili Mabingwa wa Nchi Simba SC, kwenye Dimba la Mkapa Jiji Dar es salaam.

KMC FC wanaingia Dimbani wakiwa na kumbukumbu ya kupoteza mchezo wa mkondo wa kwanza, hivyo kwa upande wao wanasema wanaingia na mbinu nyingine ya kutofungwa huku Simba SC wakisema wanazitaka alama tatu ili kujiweka karibu kabisa na Ubingwa.

Kocha wa KMC FC Habibu Kondo amesema kuwa "Simba SC walitufunga mchezo wa kwanza haijalishi wamekuja kupoteza mchezo wao uliopita pia, lakini sisi tunatengeneza mbinu zetu ili wasitufunge mchezo wa kesho (leo)". Amesema Kondo.

Kwa upande wake Kocha Msaidizi Suleiman Matola amesema "Maandalizi kwenye mchezo wa kesho (leo) yamekamilika kwa kiasi kikubwa huku matumaini ya ushindi yakiwa makubwa.

Mchezo utakuwa mgumu kwasababu Ligi inaelekea ujingoni na kila timu inataka kumaliza ikiwa katika nafasi nzuri, sisi tunataka ubingwa na tunaamini tutaondoka na alama tatu muhimu". Amesema Matola.

Yote kwa Yote dakika 90 za jasho na damu kuamua.. Usikose Ukasimuliwa..Kumbuka mchezo huu ni kuanzia saa 1:00 Usiku

Kulitaka Mwana Kulipewa Mwana

....Ghazwat....


Kikosi cha KMC FC;

Kaseja, Kijili, Ramadhan, Vicent, Mwwikenda, Masoud, Mwenda, Ally, Kabunda, Anthony, Abdul.

Akiba;

Sudi, Jean, Gambo, Cliff, Samatta, Paul, Peter, Kaparata.

Kikosi cha Simba SC;

Manula, Kapombe, Hussein, Onyango, Wawa, Lwanga, Chama, Mzamir, Bwalya, Mugalu, Miquissone.

Akiba;

Kakolanya, Kennedy, Nyoni, Dilunga, Kagere, Bocco, Morrison.

=======

Timu zipo uwanjani zikifanyiwa ukaguzi, salamu tayari kwa ajili ya kuanza mchezo.

Wakati wowote mpira utaanza Dimba la Mkapa

00' Naaaam mpira umeanza ni dakika 90 Wanaume hawa wanapambana kuwania alama tatu muhimu.

02' Mugalu Goooooooooaaal Goooooooaaal

Kope Mutshimba Mugalu anaipatia Simba SC bao la kwanza akipokea pasi murua kutoka kwa Chama | KMC FC 0-1 Simba SC

05' Almanusura Simba wapate bao la pili, lakini shuti la free kick la Chama linagonga mwamba na kuokolewa KMC

10' KMC wameamuka dakika hizi, wanapata Kona ya kwanza ambayo haikuzaa matunda.

15' Simba wanalisaka lango la KMC, kwa mashambulizi huku golikipa Manula akiwa rikizo.

20' Mpira unachezwa zaidi eneo la KMC, wataweza kuzuia wasifungwe? Ngoja tuone | KMC FC 0-1 Simba SC

25' Umiliki wa mpira ni zamu kwa zamu, lakini KMC wanatafuta bao la kusawazisha huku Simba wakitaka kuongeza bao.

35' Simba wanashindwa kutumia nafasi hapa, ilikuwa hatari sana lango la KMC, shuti la Miquissone linadakwa na golikipa Kaseja.

38' Chama anakosa nafasi ya kufunga ambapo mabeki wa KMC walipoteana, lakini shuti linatoka nje ya lango.

Onyango akionyeshwa Kadi ya Njano kwa kucheza madhambi..Ni Free Kick.. Inapigwaaaa wanakosa KMC

44' Mugalu Goooooooooaaal Goooooooaaal

Kope Mutshimba Mugalu anaingia kambani mara ya pili kwa shutiiiiii kali likimuacha golikipa Kaseja akiruka bila mafanikio | KMC FC 0-2 Simba SC.

45-2' Kuelekea kuwa mapumziko Dimba la Mkapa

Naaaam mpira ni mapumziko ambapo Simba wanaongoza kwa mabao mawili kwa bila dhidi ya KMC

VPL, HT; KMC FC 0-2 Simba SC


Kipindi cha pili kimeanza hakuna mabadiliko kwa pande zote mbili huku Vicent akionyeshwa Kadi ya Njano kwa kumchezea faulo Mugalu

47' Free Kick kuelekea KMC.. Inapigwa lakini wanababatiza ukuta wa mabeki wa KMC.

Chupu chupu KMC wafunge bao, lakini mpira uliokuwa ukielea unaokolewa na golikipa Kaseja | KMC FC 0-2 Simba SC.

58' Mabadiliko upande wa KMC FC, wametoka Anthony, Mwenda na wameingia Paul Peter na Samatta.

65'Vicent anaokoa mpira kwenye chaki, ilikuwa nafasi kwa Simba kufunga huku KMC wakipata faulo kuelekea Simba, lakini mpira unatoka nje ya lango.

70' Ametoka Mzamir na ameingia Dilunga upande wa Simba SC huku Manula akifanya Save moja bomba | KMC FC 0-2 Simba SC.

75' KMC wamepoteza nafasi mbili za kufunga..Naam Ametoka Kabunda na ameingia Cliff

Mugaluuuuuuuuuuu Lakini ni Offside alikuwa ameweka kambani kope Mutshimba | KMC nao wanakosa utulivu eneo la lango la Simba

81' Vicent anaonyeshwa Kadi Nyekundu kufuatia Kadi ya Njano ya kwanza. Huku Kaseja akiwa chini baada ya kupata rabsha.

85' Ametoka Miquissone na Ameingia Morrison upande wa Simba SC | KMC FC 0-2 Simba SC.

88' Shambulizi kali kuelekea kwa KMC, lakini mabeki wanakaa imara. Ametoa Mugalu na ameingia Bocco upande wa Simba SC.

90+4' Kuelekea kumalizika kwa mchezo huku Simba wakimiliki zaidi mchezo na matumaini ya KMC kupata bao yakififia.

Simba wanakosa nafasi ya kufunga ilikuwa hatari lango la KMC FC

Naaaam mpira umekwishaaa ambapo Simba SC wanaibuka na ushindi wa mabao mawili kwa bila dhidi ya KMC FC

FT, VPL; KMC FC 0-2 Simba SC

...... Ghazwat......
 
Yaani leo
FB_IMG_1625635996695.jpg
 
Simba wamepoteana baada ya kufungwa na yanga!! Wafungwe tena, maneno ya shombo ya Manara yanaudhi
 
Leo mnapigwa, game ya kwanza mlibebwa kwa kupewa penalty ya uongo, sasa Leo referee adhubutu kuwabeba some Cha mtema kuni. KMC komaza mimba hiyo aliyowekwa tarehe 3/7/021 na mme wake wa enzi na enzi.
 
Back
Top Bottom