KMC FC nimeshamaliza kila Kitu, tafadhali msiniangushe leo mnapocheza na Njaa Vitisho Malalamiko Albadiri Jangwani FC kwa Mkapa

MINOCYCLINE

JF-Expert Member
Apr 2, 2015
8,011
16,748
Nataka tu Mshinde au Mtoke Sare tu, ila msikubali Kufungwa kabisa leo kwani mtanikera.

Hao Mabeki wenu waambie Wawagongegonge ( wapige Buti ) sana akina Kisinda na Ntibanzonkiza.

Tumeshamaliza Jukumu la Kimataifa ( CAF Champions League ) na tunarudi VPL.

Nawaonea mno Huruma watakaokutana na Simba SC kwa Vipigo Vitakatifu.

Jana Mwarabu kanijeruhi kidogo tu ila kuna Mtu May 8 atajuta Kunifahamu kwa Mkapa.

Ule msemo wa kila Mtu acheze Mechi zake urejee rasmi na hatutaki Visingizio tafadhali.

KMC FC yale Mambo yetu ya ' Kiutamaduni ' niliyowaelekezeni msisahau Kuyafanya Uwanjani.

Na Wewe Waziri Innocent Bashungwa acha Mahaba yako yaliyopitiliza kwa Yanga SC sawa?

Mwenzako Waziri Mwigulu Nchemba alikuwa kama Wewe tukamuonya na ilimgharimu pia.

Wewe ni Waziri wa Michezo na siyo Waziri wa Kuibeba Yanga SC tu. Usitukwaze mapema hivi.

Kazi Kwenu tu KMC FC nimemaliza Kazi.
 
Wapiga Ramli Mmeanza Kujitokeza.

Mtani subiri huyo KMC tutamalizana nae vyema japo mechi kweli ni ngumu kwa upande wetu.

Ila wape salaaam!
 
Nataka tu Mshinde au Mtoke Sare tu, ila msikubali Kufungwa kabisa leo kwani mtanikera.

Hao Mabeki wenu waambie Wawagongegonge ( wapige Buti ) sana akina Kisinda na Ntibanzonkiza.

Tumeshamaliza Jukumu la Kimataifa ( CAF Champions League ) na tunarudi VPL.

Nawaonea mno Huruma watakaokutana na Simba SC kwa Vipigo Vitakatifu.

Jana Mwarabu kanijeruhi kidogo tu ila kuna Mtu May 8 atajuta Kunifahamu kwa Mkapa.

Ule msemo wa kila Mtu acheze Mechi zake urejee rasmi na hatutaki Visingizio tafadhali.

KMC FC yale Mambo yetu ya ' Kiutamaduni ' niliyowaelekezeni msisahau Kuyafanya Uwanjani.

Na Wewe Waziri Innocent Bashungwa acha Mahaba yako yaliyopitiliza kwa Yanga SC sawa?

Mwenzako Waziri Mwigulu Nchemba alikuwa kama Wewe tukamuonya na ilimgharimu pia.

Wewe ni Waziri wa Michezo na siyo Waziri wa Kuibeba Yanga SC tu. Usitukwaze mapema hivi.

Kazi Kwenu tu KMC FC nimemaliza Kazi.
Mmeshaaza kutuhumu watendeji wa wizara Mbumbu FC, kulikoni?
 
Vijana wa Kino wapigeni hao Wazee wa Mafuriko, Vijora, Madela, Malalamiko, Gongowazi, Albdir, Manyani, Vidimbwi, Chura, Utopolo, Kilo 800 FC warudi kupalilia mpunga kule bondeni kwao.
 
Yametimia

Endeleeni tu Kutoniamini kwenu hapa JamiiForums na kudhani kuwa Mimi Generalist huwa nakurupuka tu kuwaleteeni Tabiri na Nujumu zangu ambazo kwa 99.999% huwa ni kweli ( sahihi )

Ahsante sana Mwenyezi Mungu wangu.
 
We bhana na wewe unatuchanganya Mala uwe Gentamycin juzi ukawa All rounder Leo umekua Generalist
All in all nakubali nondo zako mzee 🙌

Haya wote Sema kimeumanaaaa 😁😁😁

Naitwa Generalist na siitwi GENTAMYCINE tafadhali na ni kwanini huwa hamnisikii na mnalazimisha?

Nimeshatoa Ufafanuzi wa kutosha tu kwanini nimebadili Jina la ID yangu ya awali nikijiita All - Rounder na sasa najiita Generalist hivi sijui kwanini mnakuwa Wagumu Kunielewa.

All - Rounder au Generalist au Jack of all trades maneno yote haya yana maana sawa ( moja ) ila nimependa kubadili na Kujiita Generalist kwakuwa ni neno fupi.

Halafu sioni sababu ya Wapumbavu kadhaa Kukwazika na Kushangaa Mimi kubadili Jina kutoka All - Rounder kuja Generalist wakati katika Settings za huu Mtandao wa JF kuna Kipengele Maalum cha Kubadili ID ukitaka ilimradi tu uwe na sababu Maalum.

Na kama ni hivyo kwanini mnakereka na Mimi kubadili Jina na hamkereki na Mtandao wa JamiiForums ulioweka Kipengele na ruhusa kwa Member kubadili ID / Jina? Nikiwa nawadharau wengi wenu na Kuwaiteni Wapumbavu msiwe mnakataa na Kukasirika kwani kwa 100% huwa nakuwa sahihi.

Hapa tu nilishatoa Ufafanuzi wa kuibadili ID kutoka All - Rounder kuja Generalist mnakereka na Kuniandama Kutwa hivi nisingeamua Kiuwazi tu kuwawekeni sawa ingekuwaje?

Unakuta nimeanzisha Uzi wa Kimjadala badala ya Watu Kuuchangia wao concern yao ni kuhusu ID yangu na Kunihusisha na ID's zingine za Mabasha / Mabwana zenu. Mmekalia tu Utoto, Upuuzi na Ushamba na ndiyo maana Watanzania nje ya mipaka tunadharaulika kuliko kutokana na Uswahili wetu.

Mwisho namalizia kwa kusema kusa kutokana na kwamba mnanihusisha na ID's mbalimbali ( nje ya hii ya Generalist ) sasa nawarahisishieni Kazi fanyeni tu ID's zote zilizopo hapa JamiiForums ni zangu Mimi pamoja na hizi zote mnazonishambulia kwa kusema nina Multiple ID's hapa.

Utume huu Ujumbe kwa Fools Wenzako.

Cc: Komeo Lachuma , Mailman, nguvu, Yuzo mawe
 
Back
Top Bottom