Kliniki ya Moyo ya Hospitali ya Mwananyamala ni tatizo

Apr 21, 2016
1
1
Naomba samahani kwa nitakao wakwaza hapa ila ni vyema kuweka bayana ukweli wa mambo.. Hasa ule unao onekana na sehemu kubwa ya jamii.

Mwananyamala ni hospitali ambayo ni rahisi kuifikiria kwenda hasa unaposumbuliwa na magonjwa sugu, uzazi, kuumia kwa ajari n.k. .. Mwaka jana Mke wangu alijifungulia pale kwa kisu Huduma zao zilikuwa nzuri na stahiki, Walikuwa madaktari vijana bila shaka walikuwa katika mazoezi ya vitendo, walikuwa wakiwakarimu vizuri wagonjwa na hata wageni wanaokwenda kuwatembelea wagonjwa hao, kwa kweli sikuwa na lalamiko la aina yoyote kila kitu kilikuwa vyema.

Kitengo cha mapokezi nimekipenda Yule mama (Bi Fatuma Mbatta) na Yule kaka Wa kichaga (samahi simjui kwa majina) wako vizuri sana katika kusimamia foleni na kuzungumza na wagonjwa vizuri.

Pale Chumba namba 8. Kuna mama mtunza mafaili yote ya wagonjwa (ana rangi ya kahawia waswahili tumezoea kuita mweupe.. na aliyevaa uso wa smile muda wote...) Huyu mama jamani muongezeeni tu mshahara, anavyo ongea vizuri na kuwachangamkia wagonjwa mpaka kuna mama alihisi kapona maradhi yake ya moyo hapo hapo kwa jinsi alivyo ifurahia Huduma yake iliyojaa ukarimu.

Lakini... Hiki kitengo namba 10 (clinic ya Moyo) kunani???.. ni nilitegemea kuwa; kwa kuwa MOYO ni sehemu muhimu na makini basi kungekua na uangalizi na uhudumiaji wenye taaluma iliyo zaidi kidogo ukitofautisha au kulinganisha na vitengo vingine(clinic).

MAJIPU:
-Kwanza Ada ya kumuona Daktari kuwa Tsh. 10,000 inaumiza sana wagonjwa hao wa Moyo hii itapelekea Vifo vya wagonjwa Wa Moyo kuongezeka nyie wataalamu wa wagonjwa ya Moyo mnaujua ukweli huu, kinacho umiza zaidi kurudisha majibu kwa Daktari pia unatakiwa ulipie Tsh. 10,000. Hii imeleta maswali mengi sana miongoni mwao wagonjwa hao kwa kweli imewafika nafsini mwao.

-Yule mama mpanga mafaili na mgawa namba pale ofisini kabla ya Daktari hana maelekezo kwa mgonjwa wala salamu Amenuna utafikiri anafanya kazi kiwanda cha Nondo, jamani hii sio jinsi ya kiwanda cha ukarimu inavyo paswa iwe, hili tuliangalia vizuri zaidi ukizingatia yeye ndio yupo mapokezi ya kwa Daktari (first impression).

-Daktari Wa wagonjwa ya Moyo anaingia saa tatu na dakika arobaini na tano (03:45 asubuhi) sijui kama ndio muda aliopangiwa na msimamizi au vipi lakini hii inawaumiza sana wagonjwa ikiwa ofisi inafunguliwa saa moja na wagonjwa wanapanga foleni kuanzia saa kumi na mbili asubuhi, basi kama ni hivyo watuandikie pale mlangoni muda wa kumuona Daktari.

-Tangu nimeanza clinic sijawahi kumuona msimamizi wa kazi kuja kukagua watumishi.. Jamani hatutibiwi bure sisi.. Tunalipia pesa tunastahili Huduma japo hata kidogo yenye taaluma au mnataka mletewe wasimamizi wa kizungu (maana mzungu huogopwa hata asipotembelea maeneo ya kazi watumishi wanakuwa na shauku ya kazi wakijua kuna bosi mzungu hii ni shida iliyopo hapa Tanzania.

-Vyoo Viko katika hali hatarishi vimejaa na havizibuliwi.. Tutapataje kupona???.. jamani choo ni sehemu muhimu kwa maisha ya mgonjwa na kila mmoja wetu.

Angalizo: Nimefurahiahwa kwa kuwekwa namba ya simu za Mfuko Wa Taifa Wa Bima ya Afya pale Famasi ikitokea kama haujaridhishwa na Huduma uwasiliane nao , lakini tumejaribu kupiga kufikisha malalamiko kwamba ofisi ya Moyo haijafunguliwa mpaka saa tatu, wanatuambia tufike ofisini namba 39, sisi tulitegemea watafika haraka kuangalia huduma au kumpigia Daktari Hawahi kufika Wanajamii nielimisheni Mimi kuhusu ukarimu. Wahusika kwa niaba ya wanajamii naomba marekebisho katika hayo kwani tunaipenda sana hospitali yetu.

Haya Siku njema wanajamii!!
 
Back
Top Bottom