Raia Mwema - Gazeti Jipya Kabisa la Kiswahili Kuingia Tanzania Kuanzia Tarehe 31 Oktoba

Gazeti jipya kabisa la Kiswahili linatarajiwa kuingia katika vibanda, maofisi, na mitaa ya Tanzania kuanzia tarehe 31 Oktoba mwaka huu. Jarida hilo la "Raia Mwema" litakuwa na habari mbalimbali zikiwemo za uchunguzi, utafiti, siasa, biashara, maoni n.k Jarida hilo liitwalo "Raia Mwema" limeanzishwa kutokana michango ya hali, mali, na vipaji ambavyo vimekusanywa chini ya Mhariri wake Mtendaji John Bwire

Kuanzishwa kwa jarida hilo ni alama ya kuvunjika rasmi kwa ndoa ya gazeti lililosifika sana nchini miaka hiyo la "Rai".
Waandishi waanzilishi wa gazeti la Rai - ukiondoa Dr. Shoo na Salva - na waandishi wengine ndani na nje ya Tanzania wamefikia uamuzi wa kuanzisha gazeti hilo wakizingatia haja ya kupanua uhuru wa maoni, habari na mawazo na kuchangia kwa namna ya pekee kuhamasisha kizazi kipya cha "Raia Wema".

Gazeti hilo litajumuisha waandishi mbalimbali wakiwemo:

Jenerali Ulimwengu
Issa Shivji
Padre Karugendo
Prof. Haroub Othman
Maggid Mjenga
Joseph Mihangwa


na wenu mtiifu, na wengine wengi ambao mtapata bahati ya kusoma kazi zao kwenye gazeti hilo ambalo litapatikana pia kwenye mtandao wakati huo.

Napenda kutoa pongezi kwa ushirikiano wote wa wale ambao wamewezesha gazeti hili kupata mtaji, kibali, na nyenzo za kutendea kazi.. Natarajia kuwa toleo la kwanza litaiweka fani ya uandishi katika ngazi nyingine kabisa nchini.

Tafadhali copy na watumie wabongo walioko kwenye orodha yako ya anuani.

Ndugu yenu,

M. M.

Karibu Raia mwema,

Hiyo list ya waandishi ni kali sana.
I cant wait kuliona.

Mwanakijiji naomba ujibu swali la masatu kama hilo gazeti litakuwa daily au weekly?
 
Nafikiri sasa baada ya kifo cha Rai tutapata gazeti la maana.

Tulikuwa tumekoza Jenerali. halafu sasa tunapata tena watu wapya ambao hawezi kuyumbishwa na MAFISADI (Othmani,Issa nk).
 
main3T_01.jpg
main3T_02.jpg
main3B_02.jpg


main3B_03.jpg
main3B_03.jpg
main3T_03.jpg


Pongezi za dhati kwa waanzishaji wa hili gazeti
Jenerali Ulimwengu
Issa Shivji
Padre Karugendo
Prof. Haroub Othman
Maggid Mjenga
Joseph Mihangwa
na waendelee kuwa raia wema. Bila kumsahau Mtiifu.
 
Kwanza ninawapa hongera waanzilishi wote wa gazeti hilo.ninaimani kuwa watanzania Tunayoipenda nchi yetu tutawaombeeni kwa mungu ili manyang'au wasiwazuru!.
Mungu ibariki Tanzania,
mungu wabariki waanzilishi wa gazeti la raia mwema na wasomaji wake watakaoanza kulisoma
MKJJ,Hongera sana mzalendo wewe!
 
Mie sipendi kukubali ila ukweli; mwenzenu machozi yananilenga...kiu niliyokuwa nayo ya habari zilizoandikwa na waandishi professionals haisemeki mtu akanielewa...yaani ukitaka kupata idea tu; jana asubuhi nilikuwa nasoma kwa mara nyingine TENA makala ya gazeti la Rai toleo la Nov 6, 1996 yenye kichwa "Tukae Chonjo Ubeberu Washambulia Tena" iliyoandikwa na Gregory Lugaila. Yale yaliyoandikwa humo mwaka 1996 na yanayotokea sasa 2007 ndani ya Tanzania ni kama vile kitu halisi mbele ya kioo; inatia majonzi na hasira. Sina la ziada; Hongera kwa wote walioona hili pengo kupata Ujasiri na kuweka Juhudi za kuliziba.

Kila la Kheri "Raia Mwema", Taifa linakuhitaji.
 
Ni vizuri watu kuonesha source za info zao zinatoka wapi, sasa kukopy neno kwa neno halafu kujifanya ni maneno yako.. inajina lake kitaaluma...
 
Back
Top Bottom