KLH Exclusive: ATC yatumia Milioni 400 ku"pimp our plane"

This JF hapendwi mtu hapa . Lisemwalo lipo na kama halipo basi laja . Kinvaba weka busara zako hapa pia uachane na utetezi na chuki za Membe kuandikwa na watu wengine kuhusishwa kule kwanza .Njoo hapa utupe busara zako .
 
Wakuu mi nilipata nafasi ya kumsikia DM(ATCL CEO) kwenye karedio kamoja cha FM asubuhi moja kuhusu hii issue hapa Tanzania. Alichosema yeye ni kama ifuatavyo:-
1. Kweli ndege hii ilikuwa ya Air Jamaica na ilikuwa inaruka kwenda USA.Kwahiyo ilipass flying standards za USA.
2. Umri wa hiyo ndege ni miaka 11. na kwa International Standard bado ni ndege mbichi. Maana hata huko marekani average age ya fleet zao ni 15-16 years
3. ATCL wamelease hiyo ndege kwa miaka 6. Hawajainunua.
4. Recommendation ya kulease hiyo ndege walipewa na Air Bus maana wanampango wa kununua ndege kwao.Na walifahamu ATCL wana shida na ndege kwa sasa.
5.Air bus ndo wanaoifanyia full check up(hapa alituamia technical term lakini nilivyoelewa ni kama dry dock ya meli yaani kila kitu kinafumuliwa nakuchekiwa)
6. Waataalam wa ATCL pamoja na wale wa Mamlaka ya Ndege nchini walikwenda na kuverify air worthness ya hiyo ndege na ilipasi kuruhusiwa kuruka nchini
7. Kulikuwa na matengenezo ambayo vendor alitakiwa ayafanye na mengine ATCL ilitaki kuyafanya(eg. Kubadilisha cushions, rangi ya ndege(maana ilikuwa na rangi za Air Jamaica), alama za kiswahili etc)
8. Ni kweli kampuni illiyoikodisha ATCl imekuwa registered Liberia kwa ajili ya tax benefits za nchi hiyo kwa investors.

Hayo ndo yalikuwa maelezo yake DM.Ila hakuzungumzia kuhusu Swala la Al Salvador na kama huko ndipo ipo service bay ya Airbus.

Mimi binafsi sina tatizo na ndege yenyewe, kwani uzima na umaira wa ndege umegawanyika katika sehemu mbalimbali. Kwa mfano, kuna engines ambazo ambazo kwenye ndege huweza kutolewa na kuwekwa nyingine kulingana na cycles. Na jambo hili ni la kitaalam zaidi kwani jambo lolote linalofanyika hapo ni lazima liwe limeidhinishwa na Manufacturer / Civil Aviation Regulator ( Hawa hutoa idhini [licence] kwa mafundi wa ndege) ambao hufanya kazi za engine. Kwa kawaida engine inapofanyiwa matengenezo aidha katika check 'C' au check 'D' hupewa lifespan ya masaa kadhaa kutegemea na aina ya ndege.
Eneo jingine katika ndege ni Frame, hii frame pia ina wataalam wake ambao kama wale wa engine ni lazima waidhinishwe na Manufacturer / Civil Aviation Regulator. Kazi zao, pamoja na mambo mengine ni kuhakikisha kuwa ile frame ipo katika hali ya kuiwezesha ndege kurua salama, kuhimili mikiki-mikiki ya angani na kutua salama. Uangalizi wa frame kama una nyufa nk huwezi kuufanya kwa macho yako meupe ni lazima utumike utaalam wa x-ray.
Eneo jingine ni la Miguu ya ndege (landing gears) yaani vifaa vile ambavyo hutumia kwa ndege kutua. Nalo hili kama yalivyo ambayo nimeyaeleza hapo juu yanahitaji utalaam wa pekee na ni lazima uidhinishwe pia. Kwani hapa ni mahali nyeti pia, fikiria wakati ndege imeweza kusafiri salama kwa masaa kadhaa halafu inashindwa kutoa miguu kwa ajili ya kutua, itakuwaje? au ina feli breaks wakati wa kutua?
Eneo jingine ni la Avionics, hili nalo ni eneo nyeti kama yalivyo mengine, kwani hapa ni kama tunaongelea mishipa ya damu ndani ya mwili wa binadamu. Avionics inahusisha masuala yote yahusuyo umeme na vitenda kazi zake. Kama ndege inakosa co-ordination katika mfumo wa kujiendesha then hapo hakuna ndege.
Yapo maeneo mengi ambayo ningeweza kuyataja hapa kuonyesha kuwa ndege haiwezi kufananishwa na gari katika jinsi ya kuimaintain.
Sasa, ili ndege iweze kufikia kiwango cha kuruka, kuna mamlaka kadhaa ambazo zinatoa idhini baada ya kukagua kazi za matengenezo.
Kwa hiyo kwangu mimi ndege mbovu ni ile ambayo haiwezi kuruhusiwa kuruka na mamlaka yeyote iliyopewa idhini ya kusimamia shughuli za anga.

Tatizo ambalo ninaliona kwa ATCL ni la kiutendaji hasa, menejimenti iliyopo sasa hivi ATCL siyo iliyohitajika kuwepo, ni dhaifu mno ukilinganisha na majukumu ya kulijenga upya shirika hilo.
Mpaka sasa nikiangalia jinsi ya mambo yanavyokwenda nina wasiwasi mkubwa juu ya 'going concern' ya ATCL seems to be another 'false start'. Lakini muda haujapita sana, ni vema maamuzi ya haraka yakachukuliwa kurekebisha hali hii kungali mapema, vinginevyo jitihada zote zitakuwa ni bure.
Nazidi kurejea ushauri wangu wa awali kuwa ni vema kukodisha menejimenti toka kwenye makampuni yaliyobobea katika kutoa huduma za mennejimenti ya usafiri wa anga walau kwa miaka miwili ili kuwawezesha wazalendo (hapa ninawalenga zaidi vijana) kujifunza na baadae waweze kuwa wataalam na viongozi kwenye sekta ya anga. Vijana wapo wengi na wanaweza kutayarishwa katika hili.
Ninasema hivyo kwa sababu, leo hii mafundi wa ndege na wataalam wengi wa ndege walikuwa ni vijana ambao walitayarishwa siku za nyuma kwa kupewa nafasi mbalimbali za kushiriki katika kujifunza fani za usafiri wa anga. Walikuwepo wataalam mbalimbali wa kigeni kuanzia marubani, mafundi, fedha nk ambapo vijana wetu walifaidika sana na kuwapo kwao.
 
Inasikitisha lakini kweli.. hiyo siyo ile mpya ambayo kiongozi wetu mpendwa anajiandaa kuangusha saini yake. Hilo ni lile kolokolo lililokuwa pimped up kwenye "gereji" ya kampuni ya Aeroman huko El Salvador. ...

Ndege hiyo ambayo ilikuwa ni ya Air Jamaica kiumri ina chini ya miaka 10 tu lakini uharibifu wake ni kama mtu alikuwa anaikomoa. Mchunguzi wenu toka KLH News anaripoti kuwa licha ya gharama ya kuipaka rangi ATC imetumia hadi hivi sasa karibu shilingi bilioni moja kama malipo mbalimbali ya kuiwezesha ndege hiyo kuingizwa nchini.

Sasa hivi dege hilo linafanyiwa mpango wa kurushwa na kuletwa Tanzania...



To be continued.

Mzee Mwanakijiji,
Nakushukuru kwa jitihada zako unazozifanya kufuatilia masuala ya ATCL. Lakini hii mitundiko yako nadhani kwa namna moja au nyingine inaweza isiisaidie ATCL kwa kutokuonyesha hali halisi na badala yake itaonekana ni ushabiki wenye malengo ya majungu. Tuisaidie ATCL kama shirika letu sote watanzania na si vnginevyo, kwani hakuna siasa katika hili.
Unaposhangaa kutumika kwa Shs. 400m/= bado unakuwa kama unataka ku-dramatize tu pasi na kutoa data kamili. Uchumi wa Tanzania huwezi kuufananisha na uchumi wa nchi zilizoendelea ambazo ndiyo wamiliki wakubwa wa hizo ndege. Kwahiyo gharama halisi unapozitafsiri kwenye shilingi ya Tanzania pasi na kuweka mtiririko wengi huweza kufikiri ni mapesa mengi.
Kumbuka matengenezo hayafanyiki Tanzania kama tunavyotengeneza gari, hapa tunatengeneza ndege kwa kutumia viwango vya kimataifa vinavyokubalika.
Kufananisha in terms of Tanzanian shillings kuna weza kukupa mlingano usio sawa.
Kwa mfano in US nywele watu hunyoa kwa $10 sawa zaidi ya sh. 10,000 wakati Tanzania ni 500.
Tufikirie hasa tunataka kuisaidia kivipi ATCL na ni nini matatizo yake ya kweli.
 
Koba,
Mfano huo wa kudeliver unaouzungumzia hakuna duniani isipokuwa hao makampuni binafsi huchukua contract za kuendesha mradi ambao bado mmiliki ni serikali. Nje ya hapo haiwezekani ktk dunia hii ya Utandawazi na soko huria na hakuna sheria ya biashara itakayoweza kumbana mtu ambaye ameuziwa kampuni jinsi ya kuiendesha. Kama tulivyokwisha ona Privatization ina sura nyingi sana na mnapodai kuuzwa ni kujiweka kitanzi sisi wenyewe..

Swala la ATCL hakika ni zito sana isipokuwa tusije linganisha ovyo...Nauli ya ndege Afrika na within nchi zetu ni kubwa sana kuliko hata nchi za Ulaya (kutokana na kutokuwepo ushindani) kwa hiyo sielewi watu mnapochukua mifano mingine lengo lake ni lipi hasa. Nauli ya Dar hadi Mwanza ni kubwa kuliko ile ya Marekani toka kwa mfano Chicago hadi NY hata kama mtabadilisha kwa dollar.
 
Wewe mkandara shauri yako,waulize microsoft wanavyopigwa lawsuits za ant trust kila siku,umeme ni issue nyeti hata kama ni private company lazima serikali ina mkono wake kwa namna moja au nyingine...sio kwa sababu ni free market & private ndio unaweza kufanya chochote,waulize Excell energy ya midwest walivyoshughulikiwa na state 1995 walivyoshindwa kuwasha umeme kwa siku mbili tuu kwa upuuzi wao tena ni mtambo tuu uliharibika wakashindwa kuset back up on time..wakaambiwa wazembe wakaishia kulipa millions,ipo in one of the case studies(dont remember the book)
 
PUndamilia, somo la hiyo namba ni kuelewa ndege ilikuwa mbovu kiasi gani. Kwa vile wao wanasema kuwa haikuwa na matatizo yoyote, ushahidi wote uliopo unaonesha kuwa matatizo ni mengi na ambayo ni ya kushangaza kwa ndege ya chini ya miaka 11.

Ila nimekuelewa unachosema.
 
PUndamilia, somo la hiyo namba ni kuelewa ndege ilikuwa mbovu kiasi gani. Kwa vile wao wanasema kuwa haikuwa na matatizo yoyote, ushahidi wote uliopo unaonesha kuwa matatizo ni mengi na ambayo ni ya kushangaza kwa ndege ya chini ya miaka 11.

Ila nimekuelewa unachosema.

Mzee MwanaKijiji,

Heshima mbele, ni jambo la kusikitisha kwamba na wewe huna data zozote za kuonyesha kwamba hiyo ndege ni mbovu kiasi gani... kama unazo tunaomba uziweke hapa kuna wahandisi pia watachambua...

Engineering ya ndege siyo kama ya Bitto ... Siku Njema, tumekuwa tujidali vitu robo robo... mara nyingi kwa sababu tu watoa hoja huwa hata siku moja walelete vitu ambavyo wamevifanyia kazi kidogo... Tunaogopeshwa tu na Tarakimu... 400Mil... ambayo ni sawa na kununua gari moja ya Waziri mkuu....
 
mie siierewigi ii miswairi. munaioneaga liloho ripaya rire renzenu ripopataga rimipango ra kuraga. rroo. ivi murikuwaga wapi iripopataga mifurusa yakuraga. mukatafutege minjia mingine yakutafunaga. iri rishirika ririanzaga kutajirishaga wandugu zenu ware wariorisigi. munachoka. musichomekege siikiibaga inakwendaga kujengaga riinchi.
 
Heshima mbele...... Kwangu naomba nimuunge mkono Pundamilia kwa sababu kuu kama nilivyosema mwanzoni, hata kama ndege ni bovu, la zamani, etc etc etc... tulipe muda na kuona performance yake!! Mimi kwa uelewa wangu wa haya mambo ya ndege I prefer Boeing to Airbus (anytime, mate) lakini kuna vigezo vinavyonifanya niamue kuwa a "Boeing Supporter" na kuna specifics models za Boeing ambazo najua ni bora kwa nchi kama zetu (B737, for old timers B727)....
Kwa hili la A320 kwa kweli naomba niseme kwamba kama Pundamilia aliposema hapo juu, hata kama MKJJ una data za ubovu (kabla ya matengenezo na maybe baada ya matengenezo) basi sisi kuwekewa hapa sio hoja, hoja ni kwamba kama imepitishwa na FAA, ICAO, IATA, TCAA (na wengine wengi wakiwemo Insurers) then sina shida nayo. Hata hayo ya kina BA, KLM, AA etc yalipitishwa na vyombo hivyo hivyo na leo ndio tunayaita madege/makampuni shupavu.... MKJJ, mkuu hata magari zamani tulikuwa tunaletewa yanaitwa "Reconditioned" na kwa kweli yalikuwa yametengenezwa yakarudi mahali pake... Sasa hata kama hii ndege ilikuwa dead (but not burried) lakini ikatengezwa ikapona sidhani kama kujua kama ilikuwa imekufa engine (labda wameweka mpya tayari), siti (zimeshwekwa mupya am sure), electrical and other systems (am sure tayari mambo ni bomba) - na walipomaliza vyote hivyo wataalam wakasema "certified" then hakuna haja ya kuangalia history etii..... Nina uhakia airframe ni 11 years old na kwenye ndege (to me with availability of spares) ndio kitu muhimu sana. Kuna nchi zimeanza ku-set restriction ya 20year old airframe to operate na sisi hii ina miaka 11, tumekodi kwa miaka 6 tukimalizana nayo itakuwa bado mbichi kabisa kwa standards za nchi nyingi sana wakuu!!

Pundamilia amesema tuangalie mbele na hapo ndipo tungeendelea kumkoma nyani na sio kupoteza mada kwenye ndege ilikuwa mbov na nini..... Kwangu nyani huyu ana sehemu tatu:
1. Matatizo ya management yakiwemo magari ya wakubwa, na matumizi mengine batili (waraka wa so-called wafanyakazi mwanzoni mwa thread hii http://www.jamboforums.com/showthread.php?t=9020&page=12)
2. Swala la ubinafsi lilijiri wakati wa Mahujaji (tumesikia kuna tume ilichunguza under directives from Minister)
3. Credibility ya mikataba ya kukodi ndege zetu (hapo sio hiyo A320 pekee, kuna DHC 8-300Q x2 na nina uhakika many more are coming)

Nadhani nitakuwa sawa nikisema kwamba issue sio ndege ni mbovu au nzima angali imeshakuwa cleared by wakuu wa Aviation Industrie and Airbus wenyewe, issue ni hayo matatu hapo juu - Tumkome mpaka kieleweke jamani na tusikubali ku-drift away from our main agenda etii!!!

Leo kwa haraka niwawekee press conference iliyofanywa na ATCL MD and officials kuhusu issue ya ndege zetu... Nimeipata kwenye Daily News la leo:
http://dailynews.habarileo.co.tz/home/index.php?id=2871
 
PUndamilia, somo la hiyo namba ni kuelewa ndege ilikuwa mbovu kiasi gani. Kwa vile wao wanasema kuwa haikuwa na matatizo yoyote, ushahidi wote uliopo unaonesha kuwa matatizo ni mengi na ambayo ni ya kushangaza kwa ndege ya chini ya miaka 11.

Ila nimekuelewa unachosema.

Mzee Mwanakijiji,
Kwa mara nyingine tena nakushukuru kwa ufuatiliaji wako.
Lakini naomba nikuelimishe kuwa hiyo namba unayoisema wewe katika matengenezo ya ndege ni namba ndogo sana. Ndege huweza kugharimu mara tatu ya hiyo namba hata kama haikuwa na tatizo lolote endapo tu muda wake wa matengenezo ya lazima utakuwa umefika. Kwahiyo hiyo namba haina tatizo, unless kama haikufanya kazi iliyokusudiwa.

Pili Mzee Mwanakijiji ninapata wasiwasi mkubwa na jinsi unavyojenga hoja juu ya ATCL kwani inaonekana hufanyi utafiti na kulenga matatizo hasa yanayoikabili ATCL, ninachokiona ni kama vile kuna mchezo wa kuigiza.
Kwa mfano, hebu angalia mtundiko wako unaoelezea kuwa ATCL imekodisha ndege mbovu ulivyokuwa siyo hoja yenye nguvu na ambayo ATCL menejimenti imeitumia kujielezea kwa kirefu kwa sababu wanaelewa they will score against allegations.
Huenda (lakini haya ni mawazo yangu binafsi) hii hoja yako ya ndege mbovu umepewa au umeshirikiana kwa namna moja au nyingine na hao wanaoijibu sasa kwa lengo la kuwajenga.

Ninashauri, bila ya kumhujumu au kumpamba mtu, tuyaangalie matatizo yaliyopo sasa na yanayotishia uhai wa ATCL. Kwa kufanya hivyo tutakuwa tunaitendea haki nchi yetu na kuwasaidia wale wanaofanya maamuzi kuwa na wigo mpana wa kuangalia na kufuatilia kwa undani matatizo yaliyokuwepo
 
K
Inasikitisha lakini kweli.. hiyo siyo ile mpya ambayo kiongozi wetu mpendwa anajiandaa kuangusha saini yake. Hilo ni lile kolokolo lililokuwa pimped up kwenye "gereji" ya kampuni ya Aeroman huko El Salvador. ...

Ndege hiyo ambayo ilikuwa ni ya Air Jamaica kiumri ina chini ya miaka 10 tu lakini uharibifu wake ni kama mtu alikuwa anaikomoa. Mchunguzi wenu toka KLH News anaripoti kuwa licha ya gharama ya kuipaka rangi ATC imetumia hadi hivi sasa karibu shilingi bilioni moja kama malipo mbalimbali ya kuiwezesha ndege hiyo kuingizwa nchini.

Sasa hivi dege hilo linafanyiwa mpango wa kurushwa na kuletwa Tanzania...



To be continued.
Kijijini Leo Hii (KLH) matango pori yalianza toka zamani kumbe
 
Back
Top Bottom