Klabu Yenye Kutandaza soka Muruwa Kwenye Premier League

IshaLubuva

JF-Expert Member
Dec 4, 2008
250
11
Nilikuwa napitia mtandao wa Soccernet nikakutana na habari kuhusu utandazaji wa soka murua katika ligi ya Uingereza. Hii hapa ni sehemu ya nukuu ya habari hiyo:

"You speak to any fan around England and ask who do they most look forward to playing, and I will guarantee most of them are going to say Arsenal because of the way they play football, and that's a credit to Arsene Wenger."

He said: "You have to admire them. You have to say Arsene Wenger is bordering on genius, the way he does it.

Habari yenyewe iko hapa;

Anton Ferdinand and Steve Bruce united in praise for Arsene Wenger - Barclays Premier League - ESPN Soccernet

Hoja ninayoileta kwenu wadau ni hii: kwa vile ndo Ligi imeanza hebu tuwe tunaitazama na kutoa tathmini zetu ni Klabu gani ambayo inatandaza soko muruwa kwa sasa na kuendelea hadi mwisho wa msimu. Karibuni
 
Hoja ninayoileta kwenu wadau ni hii: kwa vile ndo Ligi imeanza hebu tuwe tunaitazama na kutoa tathmini zetu ni Klabu gani ambayo inatandaza soko muruwa kwa sasa na kuendelea hadi mwisho wa msimu. Karibuni[/QUOTE said:
mkuu yani umeanza kutoa jibu alafu ukamalizia na swali lool.
 
Kauli yako mtoa mada naweza kufananisha na yule nahodha wa timu ya zanzibar enzi zile walipokuwa wanacheza na waarabu yaani walikuwa wanatandaza soka safi lakin hakuna magoli..Yakheee chenga twawala lakini twafungwa tu!!..Hii naona inafanana na Timu ya wenger.Watu wanataka magoli na vikombe kibindoni!! Spain wao ndo wanapenda ligi ya shoo zakina Messi
 
Hamna club ya kufananisha na Arsenal ulimwengu huu....
sema labda kwa england ndio wanajua kukaa na mpira au gonga nyingi lakini mafanikio zero,ila kwa duniani,wakifika spain hawakamati kwa barcelona,tafuta mkanda wa video 2000 ktk champions league nou camp 1-1 ball possession ilikuwa barca 71 arsenal 29 ktk kipindi cha kwanza,na msimu uliopita nadhani uliona mwenyewe kuanzia emirates hadi nou camp,hapo emirates utadhani arsenal alikuwa ugenini wenger mwenyewe na bendtner fowadi wenu mahiri mnaemtegemea walikiri barca ni kiboko,na hata kwa nyuma deportivo nao walikuwa balaa,barca alishawapigia liverpool pasi 40 mpaka goli pale anfield,liverpool walipigwa 3-1 owen alitangulia kufunga goli,overmars,rivaldo na kluivert wakarudisha na kuongeza ktk champs ligi mwaka 2001 mwezi nadhani septemba au novemba kama sijakosea.
 
Kauli yako mtoa mada naweza kufananisha na yule nahodha wa timu ya zanzibar enzi zile walipokuwa wanacheza na waarabu yaani walikuwa wanatandaza soka safi lakin hakuna magoli..Yakheee chenga twawala lakini twafungwa tu!!..Hii naona inafanana na Timu ya wenger.Watu wanataka magoli na vikombe kibindoni!! Spain wao ndo wanapenda ligi ya shoo zakina Messi

Jamani mtoa hoja yuko wazi kabisa anataka kujadili ni timu gani inatandaza soka murua ligi ya Uingereza. Jibu hapa ni wazi na dhahiri kabisa kwa kila mpenda soka murua. Ni timu ya ASERNAL
 
Kumbe hata JF vilaza wapo; toeni majibu kutokana na swali uliloulizwa, sio hadithi ndefu! Swali linahusu timu inayocheza soka murua linakuja jibu la timu iliyochukua vikombe vingi, na ukiulizwa timu iliyochukua vikombe vingi EPL utajibu nini?
 
Hebu tuwaimbie kipande hiki..
"Hujaulizwa...,unajibu...,ukiulizwa utajibu nini wee...,utaambiwa wewe hayakuhusu..."
Messi anaingiaje hapo wakati hachezi EPL...!?
 
Hebu tuwaimbie kipande hiki..
"Hujaulizwa...,unajibu...,ukiulizwa utajibu nini wee...,utaambiwa wewe hayakuhusu..."
Messi anaingiaje hapo wakati hachezi EPL...!?
wajerumani walikuwa wana kipindi chao na kujitangaza football made in germany,sasa sisi tunasema football made in spain especially in barcelona,england na premier league yao madomokaya tu wanajitangaza sana mafanikio hakuna,siku wakibeba world cup england nadhani hata huko watu wa mapangoni jalalabad ambao mpira umewapitia kushoto watajua tu itakuwa breaking news kila siku/wiki na hata mwezi,utasikia beckham,lampard,terry,gerard,rooney,walcott sasa hivi adam johnson
 
hiyo kilabu inayotandaza soka lenye kusisimua je imewahi kubeba champions league mara ngapi?

Au ndo uhuru wa kuongea basi hata uharo mna bwabwaja tu?
 
wanaojuwa soka hawaangali utandazaji wa soka.
Wanaangalia vikombe na ngao kabatini ziko ngapi?
Na ndo maana wachezaji wenye utiamamu wa akili wote wamewakimbia na mmebaki na hao hao kina Bendtner, Diaby na konokono wengine
 
hiyo kilabu inayotandaza soka lenye kusisimua je imewahi kubeba champions league mara ngapi?

Au ndo uhuru wa kuongea basi hata uharo mna bwabwaja tu?
Wapi AC Milan special thread? Tuwekee humu au kama ipo, ipe oxygen tuwe tunatembelea na kujua kilichojiri!
 
Back
Top Bottom