Klabu ya Yanga maji ya shingo Msemaji afunguka yaomba msaada

Ghazwat

JF-Expert Member
Oct 4, 2015
23,718
66,262
Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara Klabu ya Yanga kupitia Msemaji wake Dismass Ten imefunguka na kuomba msaada kwa wadau mbalimbali wa soka nchini kuwasaidia vifusi vya mchanga ili waweze kurekebisha kiwanja chao cha Kaunda kilichopo Jangwani, Dar es salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari leo kwenye makao makuu ya Klabu hiyo Dismass amesema kulingana na ukubwa wa uwanja huo wanahitaji watu ambao wataweza kujitolea ili waweze kukamilisha zoezi la ujenzi.

"Taratibu za awali zimeanza kufanyika za ujenzi wa uwanja wetu wa mpira hapa Kaunda kwa sababu tunahitaji sehemu nzuri na tulivu ya kufanyia mazoezi. Kwa hivyo ambao watapata nafasi ya kupita Makao Makuu ya Klabu Jangwani, wataona vifusi vya mchanga vikimwaga", amesema Dismass

Aidha, Dismass amesema Wanakarabati uwanja huo kwa maelekezo mazuri kutoka kwa wataalamu wa ujenzi ili timu yao iweze kupata sehemu ya kufanyia mazoezi.

"Bado tunahitaji kifusi kwa ajili ya ujenzi huu kwa sababu eneo ni kubwa, wale wote ambao wanaweza kutusaidia kwenye eneo hili tunawakaribisha kutokana Wanayanga wanahitaji kujenga Yanga yao, kwa maana timu iweze kupata sehemu maalumu ya kufanyia mazoezi. Pia niwashukuru wale ambao wameshaanza kutusaidia katika hili kwa namna moja ama nyingine", amesisitiza Dismass.

Klabu ya Yanga inatarajia kushuka dimbani kesho kuwavaa Mtibwa Sugar katika michuano ya Ligi Kuu Tanzania Bara huku ikimkosa mchezaji wake wa Kimataifa, kiungo Tshishimbi Kabamba anayetumikia adhabu ya kukosa mechi moja baada ya kupata kadi 3 za njano katika mechi 3 zilizopita.
 
Zile nyasi zenu za bandia mlishazikomboa bandarini?
Au pesa imekwama kwenye utakashishaji?
 
  • Thanks
Reactions: SDG
images-2.jpeg
Ndiyo huuu?!
 
Hadi mwezi huu wa Septemba unaenda ukigoni, magugu maji bado yapo yamestawi licha ya hiki kiangazi kikali. Pale watengeneze bwawa tu la samaki.

Serikali kupitia NEMC wapigeni marufuku Yanga wasijenge kwenye hilo eneo la wazi ambalo ni mapumulio ya bahari kulingana na uoto wa asili.

Kuna wakati ilisemekana kuea Yanga wanamiliki Jengo tu, lile eneo la uwanja ni eneo la wazi Mali ya Serikali. Kama hilo lina ukweli tunashauri hatua kali zichukuliwe dhidi ya uvamizi huo.

Tunaipenda nchi yetu, sisi ni wazalendo.
 
Hajaitaja Simba, angekuwa kilopolopo asingeweza kumaliza mazungumzo pasina kuitaja Yanga.
 
Mkuu Tambua Kuwa YeboYebo hawana Uwanja Bali Wana Bwawa tu Pale Lililojaa Magugu na Vyura Vingi
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom