hassan kisabya
Senior Member
- Jun 14, 2014
- 165
- 109
Political Leaders Club ni chombo cha viongozi wa vyama vya siasa kinachoundwa na wenyeviti wa vyama vya siasa taifa na makatibu wakuu wa vyama taifa.
Kila chama cha siasa katika club hii kinawakilishwa na viongozi hao wakuu wawili wa juu yaani Mwenyekiti na Katibu Mkuu.
Chombo hili kina kinaundwa na vyama visivyo na uwakilishi ktk bunge la jamhuri. Vyama hivyo ni NRA, TADEA, AFP, UMD, TLP, SAU, UPDP, DP, CCK na ADC.
Club hii ina malengo ya kujenga jukwaa la mashauriano juu ya masuala ya kisiasa, katiba,a mani, umoja wa taifa, changamoto za sheria za kisiasa na kutatua migogoro ndani ya vyama hivyo.
Katika kikao cha jana, club imejadili kuhusu mahitaji ya kisheria juu ya vyama vya siasa nchini, hali halisi ya siasa nchini, hususani suala la ruzuku ya serikali kwa vyama vya siasa na sheria ya gharama za uchaguzi no 6 ya mwaka 2010 na mengine kama hadhi ya ofisi za vyama, bendera, kadi za vyama, mawasiliano nk. Kwa mapana sana, wakuu wa club walijadili kazi na majukumu ya Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi mkuu wa fedha za umma (CAG) na Katiba Mpya.
Club hii imeunda kamati maalum ya viongozi 6 itakayoratibu masuala mbali mbali ikiwa ni mpango kazi wa club hii kwa sasa.
Taarifa mbalimbali, kazi na majukumu ya club zitawajia kila panapokuwa na na mahitaji hayo. Kamati itakutana tena Dar es Salaam tar 4/3/2017 saa 9 alasiri katika hotel moja hapa jijini kuandaa mpango kazi.
Imetolewa na Mwenyekiti wa club;
Com. Fahami n. Dovutwa
Mwenyekiti.