Klabu ya Simba yathibitisha kukamilisha usajili wa kiungo nyota Nassoro Kapama

Ghazwat

JF-Expert Member
Oct 4, 2015
23,718
66,262
Klabu ya Simba, Wekundu wa Msimbazi leo Julai 11, 2022 imethibitisha kukamilisha usajili wa kiungo nyota Nassoro Kapama kwa mkataba wa miaka miwili akitokea klabu ya Kagera Sugar.

Nyota huyu ambaye ni Kiraka ndani ya dimba, ana uwezo wa kucheza nafasi zaidi ya mbili, eneo la Kiungo cha mshambuliaji, Kiungo cha ulinzi, eneo la beki wa katikati huku akiwa amefunga mabao 2 na assist 3 katika michezo 25, akiwa na Klabu ya Kagera Sugar, hali iliyoivutia benchi la ufundi la Simba SC kumsajili.

"Kipaji kikubwa kutoka kwenye ardhi iliyobarikiwa ya Tanzania, kuja kuongeza nguvu kwenye kikosi chetu, Nassoro Kapama ni Mnyama". Imeeleza hivyo Taarifa ya Simba SC

Screenshot_20220711-131112~2.jpg
 
Tuna sisitiza Simba isajili, iache mambo ya maskara, Mtaanza kulalamikia Tff bila Sababu kama alivyo lalamika ndugu Mangungu msimu uliopita.

Mpira ni uwekezaji Sasa nyie endeleeni na kuchezea shilingi chooni.
 
Mbona wa kutetema naye hatujaona akiitwa timu ya Taifa naye mbovu? Maana anasifiwa ni mchezaji hatari
Mayele alimtoboa Juma kaseja pale Taifa akiwa anacheza timu ya Taifa ya Kongo. Ukiacha Samata na Msuva hakuna forward wa kibongo mwenye Kariba ya Mayele Kwa Sasa.

Ni kwasababu ya Chupri za Marefa ndio maana alikosa kiatu Cha mfungaji Bora ila hakuna mshabiki asiyejua ukweli kuhusu uwezo wa Mayele.
 
Back
Top Bottom