Kunguru Mjanja
JF-Expert Member
- Aug 22, 2012
- 2,036
- 3,929
Mrithi wa aliyekuwa kocha msaidizi wa Simba, Jackson Mayanja anatarajiwa kutua leo jijini Dar es Salaam.
Djuma Masudi ndiye anayekuja kuchukua nafasi yake na huenda akaiwahi mechi dhidi ya Yanga Oktoba 28 kwenye Uwanja wa Taifa.
Kama humfahamu Djuma enzi zake za uchezaji alikuwa straika wa Inter FC ya Ligi Kuu ya Burundi. Ni kocha kijana mwenye mizuka na uwezo mkubwa wa kupandisha morali ya wachezaji kama alivyo Jamhuri Kihwelu 'Julio' au Ettiene Ndayiragige wa Mbao FC.
Kwa mujibu wa wachambuzi wa soka la Rwanda, Djuma ni kocha mwenye maneno mengi na rafiki wa wachezaji na inapotokea timu imeshinda hupandisha wazimu kama kocha wa Chelsea, Antonio Kante.
Kocha huyo ameipa Rayon Sports ya Rwanda ubingwa msimu uliopita kabla ya kuachia ngazi. Mafanikio yake katika Ligi ya Rwanda msimu uliopita yameivutia Simba na kuona ni mtu sahihi wa kumsaidia kocha wa sasa Joseph Omog.
Mmoja wa mabosi wa juu wa Simba aliliambia Mwanaspoti.com kuwa wamevutiwa na kocha huyo na tayari wamefanya naye mazungumzo ili aje kuziba nafasi ya Mayanja ambaye anaachana na timu hiyo baada ya kufanya kazi kwa miezi 22.
CHANZO: Mwananchi
=========================================================================================
UPDATES
Klabu ya Simba Sports Club ya jijini Dar es salaam leo imemtambulisha rasmi kocha mpya msaidizi Djuma Masoud, akichukua nafasi ya Jackson Mayanja ambaye amejiuzulu nafasi hiyo kutokana na matatizo ya kifamilia.
Msimu uliopita Djuma alikuwa kocha mkuu wa timu ya Rayon Sports ya Rwanda ambayo aliisaidia timu hiyo kutwaa ubingwa wa ligi kuu ambapo baadaye alichanguliwa kuwa kocha bora wa msimu 2016/2017.
Djuma amewahi kuvichezea vilabu vya APR, Rayon Sports, Prince Louis, Inter Star pamoja na timu ya Taifa ya Burundi Intambamurugamba.