Klabu ya simba msiipokee mil.50 za Kessy, pelekeni suala lenu FIFA

Mpira wa kona

JF-Expert Member
Nov 25, 2016
350
338
Viongozi wa Klabu ya Simba nawaomba mzingatie Ushauri uliotolewa Na Mwenyekiti Mstaafu wa Simba Alhaj Rage Juu ya kupeleka suala la Klabu 6a Yanga wa Kimataifa ya kusafiri , kumchezesha mchezaji halali aliye ndani ya mkataba Hassan Kessy kinyume Na Sheria za Fifa.

Ushahidi wa TFF ndio utakaotumika.Sh.milioni 50 Simba mnazo Na Kwa Maelezo ya Alhaji Rage faini hiyo in ndogo hivyo hampaswi kuichukua.Pia kumbukeni hao Yanga wamekuwa wanawachezea rafu katika usajili wenu wamekuwa wanawarubuni wachezaji wenu hivyo wakati umefika wa kuwafundisha Sheria za sika.

Nilitegemea TFF pamoja Na hukumu ya Kessy ingekwenda mbali zaidi kujiuliza Je Yanga wakati inamchezesha Kessy alikuwa in mchezaji wa Simba au wa Yanga? Kama wa Simba adhabu yake nini? Lakini TFF imenyamaza.
 
We jamaa bhana...
Tatizo umeongozwa na mawazo ya Rage kuleta uzi bila kuyatafakari.
.. Kwanza kesi ikienda FIFA hata hizo 50 hampati .
Najua hujui kilichokuwa nyuma ya pazia mpaka TFF ikafikia maamzi hayo.
Najua leo mapumziko, pengine bado umelala na uko ndotoni
 
We we ndio uko ndotoni mpira una Sheria zake MKUU huwezi kuongea Na mchezaji masuala ya usajili wakati yuko kwenye mkataba timu ikimfungia mchezaji wake sio mnakurupuka kumsajili wa kimataifa bwana mbumbumbu
 
Wamezungumza nae akiwa kabakiza muda gani kwenye mkataba wake?hapo ndio pa kuanzia. .....akiwa kabakiza na season moja basi anakuwa huru kuununua mkataba wake uliobaki au kuanza mazungumzo na club inayomtaka
 
We jamaa bhana...
Tatizo umeongozwa na mawazo ya Rage kuleta uzi bila kuyatafakari.
.. Kwanza kesi ikienda FIFA hata hizo 50 hampati .
Najua hujui kilichokuwa nyuma ya pazia mpaka TFF ikafikia maamzi hayo.
Najua leo mapumziko, pengine bado umelala na uko ndotoni
Umesahau kwanini rage aliwaita mbumbumbu.

We we ndio uko ndotoni mpira una Sheria zake MKUU huwezi kuongea Na mchezaji masuala ya usajili wakati yuko kwenye mkataba timu ikimfungia mchezaji wake sio mnakurupuka kumsajili wa kimataifa bwana mbumbumbu
Haya bhana... Kumbuka mambo mengi kuhusu Yanga Rage huwa hatoboi..
Mojawapo ni suala Twite...
Pia kumbuka TFF mara nyingi hutoa maamzi ili kukomoa au kukwepa lawama au kutetea maslahi yao..
 
Ni kweli ni wakati umefika sasa ili tuheshimiane

Waende Fifa wamecheza rafu nyingi sana Mkodisho FC
 
Mleta mada hujui kuwa TFF ndiye anaye wakilisha FIFA? Bila shaka umekurupuka na Rage wako!

Yanga itabaki kuwa yanga tu! Kama unabisha washawishi hao wamatopeni wenzio waende huko FIFA unapotaka kukimbilia! Hata 3ml hamtapata.

Kweli kukaa sana kwenye matope panageuza akili kuwa za matope pia.
 
Nahisi harufu ya woga kwa mbumbumbu f.c, hakuna namna, ili mbumbumbu f.c watwae ubingwa ni lazima yanga tulimwe point!
 
Hamna kitu hapo. Hao hao TFF ndio waliompitisha. Kama alikuwa na mkataba wangemkatalia usajili.
 
Nahisi harufu ya woga kwa mbumbumbu f.c, hakuna namna, ili mbumbumbu f.c watwae ubingwa ni lazima yanga tulimwe point!
Hakuna hata point moja itakayopokwa kutoka Yanga. Kosa la Yanga ni kumsajili kabla ya mkataba wake kuisha mikia fc, kipindi anacheza Yanga hakuwa na mkataba kabisa na mikia fc ndiyo maana TFF ilimuidhinisha kucheza Yanga kwa maelekezo kuwa suala la usajili wake ni issue ya madai ambayo haiwezi kumzuia kucheza mpira.

Tunatambua mikia fc wanayo hamu ya kupindukia kuchukua ubingwa wa Bara na Yanga ndiyo kikwazo kwao, tunaamini TFF ikitangaza kuipoka Yanga pointi zote za mechi alizocheza Kessy, watachekelea sana wala hawatahitaji hata hiyo Shilingi Milioni Hamsini.;):D;):D

Mikia fc wawe wanajiongeza angalau kidogo tu ili kuyaelewa haya mambo.
 
Back
Top Bottom