Klabu ya Bayern Munich yamtimua wake Kocha Carlo Ancelotti

Ghazwat

JF-Expert Member
Oct 4, 2015
20,413
2,000
Klabu ya Bayern Munich ya Ujerumani imemtimua Kocha wake Carlo Ancelotti raia wa Italia kufuatia mwenendo mbaya wa hivi karibuni wa klabu hiyo.

Kocha huyo wa mabingwa watetezi wa Bundesliga, ametimuliwa ikiwa ni siku moja baada ya kufungwa mabao 3-0 na Paris St Germain (PSG) kwenye ligi ya mabingwa Ulaya Champions League.

"Ningependa kumshukuru Carlo Ancelotti kwa ushirikiano, Carlo ni rafiki yangu na ataendelea kuwa rafiki yangu lakini inabidi tufanye uamuzi kiueledi. Mechi yetu na Paris St Germain imeonyesha wazi kuwa tunapaswa kupima matokeo", amesema Karl-Heinz.

Ancelotti alijiunga na Bayern msimu uliopita na kuchukua ubingwa wa Bundesliga, lakini aliondolewa katika hatua ya robo fainali ya ligi ya mabingwa ya 2016/2017 na timu ya Real Madrid kutoka Hispania.
 

Glycel

JF-Expert Member
Mar 14, 2017
417
250
Ilikiwa lazima aondoke lig ameanza kwa kisuasua sana plus kipigobcha jana ilikuwa inamlazimubaondoke
 

kiatu kipya

JF-Expert Member
Dec 4, 2016
3,278
2,000
Karl Heanz aliona mzee anafanya utani na Club yao ,wakati mwingine wanakwambia ni vigumu kufundisha timu kama bayern maana wakati mwingine pale wale wazee ni mafundi kuliko hata kocha mwenyewe
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom