KLABU BINGWA ULAYA: Manchester City na Real Madrid zang'ara katika usiku wa Ligi ya Mabingwa

Shadida Salum

Journalist at JamiiForums
Sep 11, 2020
69
104
20210224_152357.jpg

Michezo miwili itapigwa leo majira ya saa tano usiku kati ya Borussia Monchengladbach dhidi ya Manchester city huku Atalanta akiialika Real Madrid .

Kiwango bora walichonacho Manchester City katika mashindano ya ndani kinakwenda kujaribiwa usiku wa leo wakati watakapomenyana na Borussia Monchengladbach kwenye uwanja wa Puskas.

Uwanja wa Puskas unatumika kama eneo la nyumbani kwa Gladbach kwa sababu ya vizuizi vya serikali ambavyo vinakataza timu ya kigeni kuingia Ujerumani.

Gladbach ambayo inashika nafasi ya nane kwenye msimamo wa Bundesliga ilikosolewa kwa uchezaji wao katika hatua iliyopita ya Ligi ya Mabingwa, kwa bahati nzuri ilifanikiwa kufuzu.

Kwa upande wa wapinzani wao wa leo Manchester City, kwa sasa ndio timu iliyo katika kiwango bora Ulaya. Imeshinda michezo 18 mfululizo kwenye mashindano yote na bado hawajapoteza mchezo hata mmoja tangu Disemba 2020.
----
Update
Manchester city imeendelea kuimarisha rekodi yake na sasa imeshinda michezo 19 kwa mfululizo baada ya kuitandika Mönchengladbach goli 2-0 .

Kwingineko mchezo kati ya Atalanta dhidi ya Madrid umemalizika kwa ushindi wa goli 1-0 kwa Madrid
 
Back
Top Bottom