Klabu Bingwa Ulaya: Juventus yapokea kipigo cha goli 3-0 kutoka kwa Real Madrid! Bayern yapata ushindi mwembamba

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,877
6,326
IMG_20180404_063125.jpg

Klabu ya soka ya Real Madrid ya Uhispania imeitandika klabu ya Juventus ya Italia goli 3-0 katika Michuano ya Klabu Bingwa Ulaya

Katika mchezo huo uliofanyia katika uwanja wa nyumbani wa Juventus(Allianz Stadium), magoli ya Madrid yamefungwa na Cristiano Ronaldo (3' na 64') na Marcelo(72')

IMG_20180404_064319.jpg


Wakati huo huo Klabu ya Bayern Munich ya Ujerumani imepata ushindi wa goli 2-1 dhidi ya klabu ya Sevilla ya Uhispania

Sevilla wakiwa nyumbani(Estadio R. Sanchez Pizjuan) walifungwa magoli hayo na Thiago Alcantara(68') na Jesus Navas aliyejifunga(37'). Goli lao Sevilla lilifungwa na Pablo Sarabia(31')

IMG_20180404_063714.jpg


Mechi hizi zote ni mzunguko wa kwanza(first leg) na watarudiana tena Aprili 11, 2018
 
Ili nusu izidi kunoga pep anatakiwa awe in the mix, bila shaka liver atakalishwa. sipati picha hapa bayern, pale barca, huku madrid kule pep na city yake
 
Hiyo game nilibet mechi zote Mbili zitakwisha Kwa magoli 3 matatu
0+3=3
1+2=3
Nimejilia sh 64000
 
Back
Top Bottom