Shadida Salum
Journalist at JamiiForums
- Sep 11, 2020
- 69
- 104
Al Merrikh watawakaribisha Simba SC ambao wameshinda michezo yote miwili ya ufunguzi ya hatua ya makundi
Simba wanapewa nguvu na ushindi uliopita dhidi ya AS Vita Club ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na Al Ahly ya Misri, huku timu hiyo ya Sudan ilishindwa kupata alama hata moja kutokana na mechi zao mbili dhidi ya timu hizo.
Miamba hiyo ya Msimbazi ilichukua ushindi wa bao 1-0 ugenini dhidi ya AS Vita kabla ya kuangusha mabingwa hao wa Afrika bao 1-0 jijini Dar es Salaam wakati Al-Merrikh, walipata kichapo cha mabao 3-0 ugenini kwa Al Ahly mjini Cairo kabla ya kukubali kichapo cha mabao 4-1 dhidi ya AS Vita wakiwa nyumbani kwenye mchezo wa pili
Licha ya kupata jeraha wakati wa mechi yao ya mwisho ya Ligi Kuu Bara dhidi ya JKT Tanzania, kipa Aishi Manula anatarajiwa kuanza katika mchezo huo, baada ya kuthibitishwa na madaktari wa timu.
Kocha Didier Gomes Da Rosa kwa kiasi kikubwa anaweza kuweka safu ya kuanzia ambayo iliwakabili na kuwashinda wapinzani wa kundi hilo hapo awali kwakuwa lengo lake ni kufuzu robo fainali .
I
Michezo mingine itakayopigwa hii leo ya michuano hiyo ni kati ya TP Mazembe dhidi ya Mamelodi Sandowns, Teungueth dhidi ya MC Alger, Keizer Chiefs dhidi ya Petro de Luanda, ES Tunis dhidi ya Zamalek, Al ahly dhidi ya Vita Club na Wydad AC dhidi ya Horoya