Klabu Bingwa Afrika: Simba SC ya Tanzania yashinda 1-0 dhidi ya Al Ahly ya Misri katika Uwanja wa Benjamin Mkapa - Dar

Replica

JF-Expert Member
Aug 28, 2017
1,441
7,780
Timu ya soka ya Simba leo iko dimbani kupambana na Al Ahly ya Misri katika mchezo wa hatua ya makundi ukiwa ni mzunguko wa pili kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa majira ya saa kumi jioni. Pamoja na timu zote kuwa na alama tatu baada ya kushinda mechi zao za mzunguko wa kwanza, Al Ahly inaongoza kundi kutokana na tofauti ya idadi ya magoli.

Kapteni msaidizi wa Simba, Mohammed Hussein amesema morali iko juu na watafanya kila linalowezekana kupata matokeo chanya. Msemaji wa Simba, Haji Manara amesema waliifunga Al Ahly 2019 na slogan ya safari hii ni 'Total war in Dar'

Kwingineko kwenye kundi A, Al Merrikh ya Sudan itaikaribisha AS Vita club ya DR Congo watapokutana kwenye dimba la Al Hilal mjini Omdurman kwenye vita ya kutoka mkiani.

Ni mechi ya mabingwa wa Tanzania dhidi ya Mabingwa wa Afrika, kuwa nami kukujuza yatakayojiri.

Timu ya soka ya Simba imeshawasili uwanja wa Benjamin Mkapa

Saa 03:54' Timu za Simba na Al Ahly zinaingia uwanjani

========

00' Kipenga kinapulizwa kuashiria mwanzo wa mchezo

04' Simba wanafanya shambulizi la kwanza kuelekea lango la Al Ahly, Miguu ya Luís Jose Miquissone inakwama kwa golikipa wa Al Ahly

08' Al Ahly wanapata mpira wa adhabu kuelekea lango la Simba lakini unashindwa kuzaa matunda

13' Simba wanafanya jaribio jingine lakini Mugalu anakuwa kwenye offside

16' Kahraba wa Al Ahly anapiga shuti kuelekea lango la Simba lakini linapaa juu kidogo ya goli

Simba Al Ahly.PNG


27' Simba wanajaribu tena langoni kwa Al Ahly lakini walinzi wanasimama imara

30' GOOOOAL, Luís Jose Miquissone anatandika mkwaju mkali kutoka nje ya 18 na kuandika bao la kwanza kwa Simba

35' Al Ahly wanapata mpira wa kona lakini unakuwa mfu

38' Simba wacheza gonga nyingi na mlinda mlango anapangua mpira wa Shomari kapombe kuzaa kona

39' Mugalu anajaribu tena mlinda mlango kupangua

44' Al Ahly wanapata kona lakini inaishia kwa kipenga baada ya Bwalya kumuingia Aishi Manula wakati akita kudaka mpira.

45+3' Mpira unaenda mapumziko

Umiliki wa Mpira ni Simba 58% kwa 42% za Al Ahly

Luis.PNG

SHUTI LA LUIS MIQUISSONE LILILOZAA GOLI
Kutoka SUDAN mchezo ukiwa mapumziko, Timu ya soka ya Al-Marreikh imepata goli moja dhidi ya mbili za Vita Club ya DR Congo. Goli pekee la Al-Merrikh limefungwa na Elsamani dakika ya 8' huku magoli ya Vita Club yakifungwa na Mukokiani dakika ya 28 na mkwaju wa penati ya Djuma Shabani likiupa uongozi timu ya Vita Club.

45' Mpira uanarejea kutoka mapumziko, Lwanga anatoka nje baada ya kukutana na Yassir Ibrahim, unakuwa mpira wa adhabu kuelekea Al Ahly

54' Mpira wa Adhabu karibu kabisa na 18 kuelekea lango la Al Ahly baada ya Shomari Kapombe kuangushwa chini

56' Shuti la Luis linagonga ukuta wa Al Ahly

59' Al Ahly wanafanya mabadiliko ya wachezaji wawili

61' Fahdy analamba kadi ya njano baada ya kumkandamiza Bwalya

68' Thadei Lwanga yuko chini na Nyoni anaamka kwenye bench

71' Mzamiru anaachia shuti kali na mlinda mlango mlango wa Ahly kuipangua baada ya kupokea pasi maridadi kutoka kwa Bwalya

75' Dakika moa ya kunywa maji

86' Luis anatolewa nje kwa machela baada ya kuumia

87' Mugalu anaenda nje na kuingia MK14 na Luis anaenda nje, nafasi yake inachukuliwa na Kahata

90' Aishi Manula anaokoa shuti kali, Simba 1-0 Al Ahly

90+1' Manula yuko chini na madaktari wanaingia kumtibu

90+4' MPIRA UNAMALIZIKA NA SIMBA INAIBUKA KIDEDEA NA KUONGOZA KUNDI A IKIWA NA ALAMA SITA, AL AHLY NA VITA CLUB WAKIFATA KILA MMOJA AKIWA NA ALAMA 3 HUKU AL MERREIKH AKIBURUZA MKIA AKIWA HANA ALAMA YOYOTE MPAKA SASA.

SUDAN:
Al Merreikh inatandikwa bao nne kwa moja nyumbani na Vita Club na kusokomezwa mkiani

MSIMAMO KUNDI A
  1. SIMBA
  2. VITA CLUB
  3. AL AHLY
  4. AL MERREIKH
 
NI. NGUMU KUAMINI
HIiZ N SABABU 3 ZA. SIMBA KUFUNGWA LEO

1)KUJIAMINI KUPITILIZA
2( KIWANGO KIDOGO CHA UWEZO KULINGANISHA NA WAARABU

3)IMANI MBOVU ZA KICHAWI
HII N SABABU KUBWA LEO SIMBA KUFUNGWA
WANAINGIA UWANJAN WAKIAMINISHWA USHINDI KUPITIA NGUVU ZA GIZA BADALA YA KUTAFTA MBINU ZA KUMMLIZA. MWAARABU

4;.......SIJJUI NISEMEEEE...

WALE WA MZIGO
GG
GG N OV2.5
HT OV 0.5
 
Lesson 3: Numbers (1-10)
واحد wahed. one.
اثنين ethnein. two.
ثلاثة thalatha. three.
أربعة arba-a. four.
خمسة khamsa. five.
ستة sitta. six.
سبعة sab-a. seven.
ثمانية thamanya. eight.
Tutaanza kuhesabu leo vizuri saa kumi jion, karibu darasani
 
Lesson 3: Numbers (1-10)
واحد wahed. one.
اثنين ethnein. two.
ثلاثة thalatha. three.
أربعة arba-a. four.
خمسة khamsa. five.
ستة sitta. six.
سبعة sab-a. seven.
ثمانية thamanya. eight.
Tutaanza kuhesabu leo vizuri saa kumi jion, karibu darasani
 
Nikicheki sofascore prediction ni yeyote anaweza kushinda.

Game ya mwisho Simba alishinda 1 bila.

Simba ana odds 3, Al Ahly ana odds 2. Waarabu wana tabia ya kufosi suluhu ugenini ukienda kwao ndiyo wakupasue Simba ikienda na mbinu safi watatoboa.
 
Back
Top Bottom