Klabu bingwa Afrika: Simba SC 1-0 Al Ahly

brave one

JF-Expert Member
Feb 5, 2013
4,876
7,366
Mechi hii Ni muhimu kwa Simba kutafuta points 3 muhimu ili kujiweka nafasi nzuri ya kufuzu hatua ya robo fainali
Mechi inatarajiwa kuanza saa Kumi kamili jioni hii

Kikosi Cha Simba tayari kimetoa Huku Zana Culibary akianza kwa Mara ya Kwanza.
Kiingilio Ni 2,000 tu wanasimba mkajaze uwanja

Simba nguvu moja
Kikosi kimeahidi ushindi mnono leo
==========

90+4' Filimbi inalia kuashiria mwisho wa mchezo, Simba anaibuka mshindi na kukusanya alama 6 akiwa nyuma ya Al Ahly mwenye alama Saba, mechi itakayofuata kwenye kundi D ni kati ya JS Saoura VS AS Vita.

Dakika ya 75 bado waarabu wapo kwa mshikaji Manula
Dakika ya 74 waarabu wanaanza safari kwenda kwa Manula wao karibu na eneo la hatar sasa
Dakika ya 73 waarabu wanaanza safari kwa Manula
Dakika ya 72 Kotei anacheza rafu kwa waarabu wanapata faulo haziai matunda.
Dakika ya 71 Okwi anarejea Uwanjani kuwavaa waarabu.
Dakika ya 69 Okwi anatolewa akiwa kwenye machela.

Dakika ya 67, Mkude, Bocco mchezaji wa Simba anapata majeraha dakika ya 68 Okwi baada ya kuanguka na kupoteza fahamu kwa muda wa dakika kadhaa.

Dakika ya 66 Chama anatoa Mpira nje

Dakika ya 64 Kagere anaandika bao tamu na kuwanyanyua mashabiki wa Simba akitumia pasi ya Bocco ya kifua baada ya kupokea krosi safi ya mmwaga maji Zana.

Dakika ya 63 Waarabu wanamfuata Manula , Wawa anaanua hatari.

Dakika ya 62 Bocco anatoa Boko akiwa eneo la hatari baada ya kupewa pasi na Okwi
Dakika ya 61 Simba wanarusha kwa kumtumia Mohamed
Dakika ya 60 Zana aliingiza majaro ya hatari eneo la hatari ila mira ukababatizwa ukatoka nje goal kick.

Dakika ya 59 Juuko anapoteza kwa waarabu, Wawa anafanya yake, Chama, Kagere anapoteza.
Dakika ya 58 Mkude anamsumbua Mwarabu na kumchezea faulo.

Dakika ya 57 Waarabu wanaanza safari kwa Manula Juuko anaanua
Dakika ya 57 Wawa anauza kwa waarabu.
Dakika ya 56 Juuko Murshid anagangwa gangwa guu lake la kushoto.

Dakika ya 55 Okwi anamchezea faulo Mwarabu karibu na eneo la hatari, Waarabu wanatumia nafasi ila mpira unapaa mawinguni.
Dakika ya 54 Zana anauza kwa Waarabu
Dakika ya 53 waarabu wanaanza safari kwenda kwa Manula, wanarejea nyumbani kisha wanaendela kupitia kwa Mohamed, Ramadhan, Khalid, Junior Wawa anazuia.
Dakika ya 52 Kager anashindwa kutumia nafasi ya mpira wa Zana.

Dakika ya 51 Waarabu wanapata faulo na mlinda mlango wao anapata hudua ya kwanza.

Kipindi cha pili Simba wanakosa nafasi za wazi tatu, dakika ya 45 Okwi, dakika ya 46 Okwi na dakika ya 49 Bocco.

Dakika 45 zinakamilika huku Simba wakishindwa kutumia nafasi walizozipata pamoja na Al Ahly nao wanakwenda mapumziko wakiwa ngoma droo.

Dakika ya 45 Waarabu wanaanua kona wanalifuata lango la Manula, Zana anachezewa faulo na waarabu.

Dakika ya 45, Chama anakataliwa na Warabu, Zana, Chama, Mkude, Chama, Kagere, kona.

Dakika ya 44 Waarabu wanalifuata lango la Manula kama hawana haraka hivi leo.
Dakika ya 43 Waarabu wote wanarudi langoni.
Dakika 42 Mohamed Hussen anafanya shambuliz mlinda mlango anadaka.
Dakika ya 42 Okwi anaangushwa eneo la hatari mwamuzi anapeta.
Dakika ya 41 Waarabu wanaliandama lango la Manula, Wawa anaosha majalo huko.

Dakika ya 40 Kagere anahindwa kutumia pasi ya Chama akiwa eneo la hatari na kuifanya iwe kona baada ya mlinda mlango kudakia nje.
Dakika ya 40 Waarabu wanaliandama lango la Manula.

Dakika ya 39 Kwasi anatoka anaingia Mohamed Hussen wa Simba.

Dakika ya 38 Kona haizai matunda, Kagre anatumia nguvu mpira unatoka nje.
Dakika ya 38 Kona inapigwa kwa sasa na Okwi.

Dakika ya 36 Simba wanapata kona baada ya Kwasi kupiga shuti eneo la hatari, Kwasi anazidiwa misuli inakaza anapewa huduma ya kwanza.
Dakika ya 35 Waarabu wanaendelea kuliandama lango la Manula, anaokoa sasa Simba wamezidiwa nguvu eneo la ulinzi muda huu hatari sana.
Dakika ya 33 waarabu wanafanya Counter attack, All Manashira, Amri, Mohamed,Mohamed, Mahanuz wanatoa nje ya hatari wachezaji wa Simba wanakabia macho hapa.
Dakika ya 33 Wawa, Chama, Mkude, Okwi, Chama, Kwasi, Bocco waarabu wanatoa mpira nje.
Dakika ya 32 Kagere anazidiwa ujanja na waarabu
Dakika ya 31 James Kotei, Bocco anazuiliwa na Mohamed Ally.

Dakika ya 31 waarabu wanafanya shambulizi kwa Manula anaokoa.

Dakika ya 30 Kwasi anatoa pasi kwa warabu akiwa eneo la hatari la waarabu.

Dakika ya 29 waarabu wanaanza mpira kwa kurusha kwenda kwa Manula.

Dakika ya 29 Chama anashindwa kupeleka mashambuliz kwa waarabu baada ya mbele kukosekana wachezaji.

Dakika ya 28 Waarabu wanakwenda lango la Manula wakiwa na Ramadhani, Okwi anazuia.
Dakika ya 27 Chama anafanyiwa faulo baada ya kuzidisha mbwembwe.

Dakika ya 26 Waarabu wanaingia eneo la Simba Kwasi anazuia.

Dakika ya 25 Manula anaanzisha mpira, Kagere, Chama, Okwi, Kwasi, Chama waarabu wanatoa.

Dakika ya 24 Wawa anaanzisha mashambulizi kwa Jonas Mkude anampa Kwasi, Kotei, Mkude, Okwi anakosa bao kwa kupaisa mpira mawinguni.

Dakika ya 22 Juuko Murshid anaosha hatari eneo lao.

Dakika ya 22 Kagere anamchezea rafu mchezaji wa Al Ahly.

Dakika ya 21 Al Ahly wanafanya jaribio la kwanza kwa Simba wanakosa
Dakika ya 20 Al Ahly wanapata faulo baada ya mchezaji wa Simba kucheza rafu
Dakika ya 19 Simba wanaanza mashambulizi kupitia kwa Zana Coulibaly
Dakika ya 18 Bocco anapaisha mpira mawinguni akiwa karibu na eneo la hatari
Dakika ya 18 Al Ahly wanarusha kwenda Simba
Dakika ya 17 Simba wanarusha
Dakika ya 16 Wawa anaanzisha mashambulizi kwenda kwa Al Ahly

Kwa hisani ya Saleh Jembe

Screenshot_20190212-134340~2.jpeg
Screenshot_20190212-134222~2.jpeg

1.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mpira hauko hivo
Al Ahly watalitia Basi hawawezi cheza Kama kule Misri
Simba 3 Al Ahly 1
Fact.

Sent using Jamii Forums mobile app
Wamezifuata point 3 zao ili wafikishe point 10 katika msimamo.
Halafu mda huo mtakaojichanganya nyinyi kujifanya mnashambia ili mpate goli kumbuka counter attack za waarabu na namna walivyo makini kwenye matumizi ya nafasi wanazopata. Bora na ninyi mpaki basi tu walao mfungwe goli 3.
 
Kwenye safu ya ulinzi naona shida hapo. Kwasi na coulibaly sio wakabaji wazuri na wakienda mbele ina kuwa shida kuzuia counter attack. Wawa na Juko muunganiko huo bado. Na mashaka na safu ya ulinzi sana na imeonekana haipo sawa. Bora mbeni akianza Mohamed Hussein na Gyan. Na kati Mpili pili ni mzuri kuliko Wawa. Pascal Wawa akiwa na mpira mzuri illa kwenye cross na kukimbiza mzito. Tuangalie tuone illa na mashaka Al Ahly huenda akapata bao. Na Al Ahly akianza kufunga Simba itapata shida. Killa la heri Simba.
 
Wamezifuata point 3 zao ili wafikishe point 10 katika msimamo.
Halafu mda huo mtakaojichanganya nyinyi kujifanya mnashambia ili mpate goli kumbuka count za waarabu na namna walivyo makini kwenye matumizi ya nafasi wanazopata. Bora na ninyi mpaki basi tu walao mfungwe goli 3.
Hawapati points 3 Leo mkuu Ni kipigo tu hakuna namba mwarabu Leo anacheza koki

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Zana Coulibaly atafanyiwa Sub mapema sana maana naona kabisa goli mbili za fasta fasta wakipigwa simba zitatokea upande wa Zana.[/QUOT

Bado nashindwa kuelewa nani alienda nje kusajili akaja na Coulibaly wakati bongo tuna namba mbili wengi zuri kuliko huyu jamaa.
 
Back
Top Bottom