KKKT waraka wa Xmas: Kama unampenda Mungu huwezi kumtesa mwanadamu mwenzio, na kuwanyima Uhuru wa Kikatiba wa kukutana

Jina la asikou limekaa kiuganda ama rwanda na sio tanzaniaaa....hahhaaaa...to be deported
Kwa mbinu za utawala huu wa awamu ya tano, haitashangaza kusikia kuanzia kesho huyo Askofu anachunguzwa uraia wake..............

Hii ni awamu ambayo watu wote tunalazimishwa tujiunge na "Praise and worship team for Magufuli" na ukienda kinyume chake utapewa majina mabaya mabaya kama vile wewe si mzalendo, wewe ni msaliti na unayetumika na mabeberu
 
Huwezi kusema unapenda Mungu usiye muona huku ukimchukia nduguyo unayemuona.
Ninapotafakari sala na mafundisho kama haya ya kikatoliki ndipo napoona Catholic ni baba lao ingawa kuna wazinguaji kama akina Pengo wanatukatisha moyo.
 
Mungu anasingiziwa kuwepo tu.

Angekuwepo, madikteta wasingeweza kuwepo.

Imekuwaje Mungu mwenye uwezo wote, ujuzi wite na upendo wote aumbe ulimwengu ambao madikteta wanaweza kuwepo?



Sent using Jamii Forums mobile app
Sometime nakuunga mkono, eti ni Mungu gani anaruhusu watu wengine kuteka, kuua na kutesa wenzao halafu yeye anaona tu na asichkue hatua??

sometime naona kama tunadanganyana tu.
 
Kwa hiyo mahubiri ya askofu mmoja ni waraka Waraka Wa kanisa, uandishi mandazi on peak
 
Sometime nakuunga mkono, eti ni Mungu gani anaruhusu watu wengine kuteka, kuua na kutesa wenzao halafu yeye anaona tu na asichkue hatua??

sometime naona kama tunadanganyana tu.
Ukitumia akili, utaona hakuna Mungu.

Tatizo wanakuwahi na kukuambia "Mpumbavu asema hakuna Mungu".

Halafu wanakuambia Mungu hajulikaninkwa akili za kiutu.

Sasa wao wana akili gani zisizo za kiutu kujua hilo?

Tunadanganyana sana. Halafu, kutoamininuwepo wa Mungu ni ajabu huko kwetu Africa tu.

Ukienda Asia, Europe, America watu washajua sana habari za kutokuwepo Mungu.

Wanaona ni fikra nyingine tu, tena zinakubalika sana tu.

Ndiyo maana ukiwasikiliza wazee wa busara kama Nyerere, utagundua Nyerere na Ukatoliki wake wote, hakuwa na shida na watu wasioamini kuwepo Mungu.

Ndiyo maana hata kwenye hotuba yake moja alisema kwamba Tanzania hatuna udini, hata akitokea mtu asiye na dini, anaweza kuwa rais, tutatafuta namna ya kumuapisha tu.

Nyerere hakuyasema maneno yale kwa mchezo, aliyaamini kabisa. Kwa sababu yeye alisoma falsafa za enlightenment, ambazo waandishi wake wengi hawakuam8ni kuwepo kwa Mungu.

Mfano mmoja ni mwanafalsafa Jihn Stuart Mill. John Stuart Mill alikuwa agnostic na skeptic. Nyerere alimoenda sana na aliandika sana papers kutika dhana zake za "Utilitarianism". Ukiangalia misingi mingi ya Utilitarianism imeendana na Ujamaa.

Mtu mwingine aliyekuwa agnostic na skeptic alikuwa Miss Joan Wicken. Mama Muingereza aliyeacha maisha yake Uingereza ili kuja kumsaidia Nyerere kujenga Tanzania. Nakumbuka tukienda Ikulu wadogo, Miss Wicken yuko so simple, watu wa Ikulu wanakula vinono vya taifa, yeye anakula ki sandwich na apple.

Huyo alikuwa agnostic na skeptic. Lakini Nyerere na Ukatoliki wake wote alimkubali akafanya naye kazi vizuri.

Katika hilo, Mwalimu Nyerere alinifundisha somo kubwa sana.

Kuchukuliana.

Alikuwa na akili kubwa ya kusema hapa tupo kazini, tutafanya kazi kwa kujali uwezo wa kazi, bika kujali huyu anaamini Mungu wala hiyu haamini Mungu.

Watu wenye akiki wana uwezo mkubwa wa kutenganisha mambo. Kuioa dini sehemu yake na kufanya kazi bila kuangalia udini.

Na hata kutumia dini katika kukuza maendeleo.

Ndipo hapo wanakwambia "If God does not exist, it is necessary to invent him. He is too much currency to be left unused".

Sasa hapo ndipo kunatokea mgogoro.

Kuna wanafalsafa wanatafuta ukweli.

Watakwambia ukweli wa kuwepi Mungu ni sawa na ukweli wa kwamba karatasi ya dola mia moja ina thamani.

Karatasi biyo haina thamani kiukweli, ni thamani ambayo imeoewa na watu tu.

Siku wakiamua kuibadilisha dola mia moja kitoka karatasi hiyo kwenda nyingine, hiyo itakuwa haina thamani.

Sasa hapi kuna watu watakubishia, watakwambia kwa sababu unaweza kununua hiki na kile leo, karatasi hiyo ina thamani.

Ridiculous.





Sent using Jamii Forums mobile app
 
Haiji akilini kumuandama Mwenyekiti wa chama pinzani kumuandama kwa kumfilisi kwa hila malizake mpaka kuzifuata shambani kwake alipo zaliwa niaibu kubwa hilo halita sahaulika mpaka kizazi cha nne kuharibu masale ya jadi si haki hapo wakati wewe ukiwa ulipo zaliwa unadai serikali iliwanyanganya Ardhi yenu mlio kuwa mnachungia ngombe bila kuwalipa fidia Sasa nawe ni wakati wako kumlipa Mbowe SHAMBA lake la asili lililo haribiwa
 
Hivi huyu ni askofu kweli au ni mwenyekiti wa chama fulani cha siasa? Viongozi wa dini kwa usahihi wanapaswa kujikita kukemea dhambi na kuhubiri wokovu, sio kuja na hoja za kisiasa. Wakristo katika biblia wanaambiwa ya duniani hayana nafasi katika ufalme wa mbinguni ambao wanajindaa kuufikia.

Huyu askofu anajichanganya sana, haelewi lengo la kazi yake. Na kama haya mambo ya kisiasa yana umuhimu sana kwake namshauri tu aachane na wito wa uaskofu aambatane na mambo ya kisiasa (ambayo ni ya kidunia) kama alivyofanya Mh Slaa. KUANZA UPYA SI UJINGA.
 
KKKT Sasa hivi kila Askofu kaota ndevu.Waraka wa KKKT hautolewi na Askofu mmoja.KKKT toeni tamko kuhusu Huyo Askofu wenu bagonza mropokaji asiyejali hata utatatibu
 
Back
Top Bottom