KKKT na babu wao waanza rasmi biashara

Mpendwa kabla ya kuhukumu jiangalie wewe umechangia kiasi gani yeye kufikia hali hiyo? Pamoja alichokisema kakisema kwa hasira lakini kasema ukweli ambao wakristo wengi kwa sababu ya selfishness wameshindwa kuhubiri injili na kuishia kuhubiri dini, makanisa na vyeo vyao. God is not respector of persons, kwake kila aliitiaye jina la bwana humokoa pasi kujali ni nani na hukumu ni yake wala sisi hatupasi kuhukumu kwani hata sisi wokuvu wetu ni kwa neema na wala si kazi ya mikono yetu. Ingekuwa si neema basi ungeketa wewe uko huko club unabadilisha chupa za bia kwa frustrations za maisha. mbele ya Mungu mahita na JK ni watakatifu sana tena wenye kufaa sana maana kawaumba kwa sura na mfano wake ila kwetu sisi tunaweza waita mashetani. Kama ndivyo kuwa wao hawafai kiasi hicho basi Sauli asingeweza kuwa mtume aliyefanya kazi ya Bwana kwa nguvu na akili zake zote hata akafikia hatua ya kuona kuishi kwake ni kristo na kufa ni faida.

Mungu hamchukii mtenda dhambi bali anachukia dhambi tujifunze kutenganisha haya mawili. Maana mtenda dhambi alimfanya Mungu akaja duniani na kumpokea alivyo na dhambi zake apate kumsafisha na kumfanya mwenye kufaa sana. Dhambi haikuwahi kumfanya Mungu kufanya kitu kwaajili yake. Kazi ya utakaso ni ya Mungu mwenyewe kwa damu ya kristo so tusiwa hukumu watenda dhambi kwani mwanawaadamu hakuja hukumu bali kutafuta kilichopotea, apate kuitenga dhambi na wanadamu hata ziwe mbali nao kama ilivyo kusini na mashariki. Vipi wewe kuhukumu kitu cha mtu mwingine? Imetupasa kuhubiri habari njema ya msamaha wa dhambi lakini kuondoa hizo dhambi si kazi yetu, hiyo kazi aliimaliza Yesu mwenyewe pale kalvari. Hapo Kalvari alilipa deni na binadamu wote wako huru kupokea msamaha saa yeyote watakapo amua kuipokea na pale ambapo Mungu atawapa neema hiyo kwanjia anayoijua yeye.

Nashukuru saaana kwa hoja zako. Mimi hata siku moja siongozwi na jazba. Na ndio maana nilichagua kutomjibu huyo aliyenitukana (kama hiyo ndiyo waiita kweli). Pamoja na sympathetic language yako mambo ambayo tunakubaliana kama ifuatavyo:

Ni wapi ambapo nimehukumu? Nimeuliza kwa lugha ya picha tu kutaka kujua kama hawa nao (imekuwa ikiandikwa humu forum kwamba walikuwa Samunge) wamempokea Yesu? Lengo langu lilikuwa kuonyesha jinsi gani kazi ya Kristu inawaleta watu kwake. Kwamba wanadhambi, sijawahi kusema. Kwamba wanaokwenda Samunge wanakiri kazi ya Kristu, nitauliza kila siku. Kama kwako huko ni kuhukumu, basi unihesabu hivyo.

Kuhubiri injili. Hivi unajua msingi wa injili ni nini? 1 Cor. 15:1: "Moreover, brethren, I declare unto you the gospel which I preached unto you, which also ye have received, and in which you stand By which also you are saved, if you keep in memory what I preached unto you, unless you have believed in vain. For I delivered unto you first of all that which I also received, how that Christ died for our sins according to the scriptures; And that he was buried, and that he rose again the third day according to the scripture." Hivyo hiyo injili aliyoihubiri yeye na kukufanya wewe kuwashambulia wakristu kwamba wanahubiri dini sijui ni ipi?

Umesema vema, kila aliitiae jina la Bwana. Hebu jiulize ni jina gani hilo. Tena jiulize hao muendao Samunge mnaliitia jina hilo? Na ndio msingi mkuu wa swali langu hapo awali. Je, kweli hilo jina mnaliitia mpate kuokolewa? Kama hilo linatokea Samunge, haleluya. Kristu ni mtawala pale. Mambo ya vague statements kwamba pale Samunge ni Mungu na si Kristo, haipo kibiblia. This is another gospel.

Sisi hatupaswi kuhukumu, bali imetupasa kuonyana na kuelezana iliyo kweli bila kuogopa watu watakaodai tunawahukumu. Kama kile nachokueleza kitakupelekea kwenye wokovu wa kweli, siwezi nyamaza. Vinginevyo ungependa injili ihubiriwe vipi? Injili haibembelezi. Palipo makosa yatopimwa kutokana na maandiko na kuwekwa wazi ili watu wajirudi. Ndivyo walivyofanya mitume. Sihubiri injili ya kuvumiliana. Nahubiri injili inayomhusu Kristu pekee, hivyo nje ya huyo siamini yale unayotaka niamini.

Wokovu ni neema. Unaelewa maana yake lakini? Kwamba hukuhitaji kufanya jambo lolote ili uokolewe. Si kwa kujitesa, wala kutoa mali yako yoyote wala chochote kile. Ni bure. Ndio maana nawahubiria wengine neema hii ya Kristu. Ama ungependa makanisa yafungwe ili tuiache neema ifanye kazi? Hapana, tutaendelea kumhubiri Kristu. Ni agizo la kristu hata kama wengine mtachukia.

Hao watu kama ni watakatifu sana na wenye kufaa hiyo ni judgement yako. Mimi nalitumia mfano halisi wa watu wanaofahamika kufikisha ujumbe. Kwamba wanamkiri Yesu, nitaendelea kuhubiria wao na wengine woote ambao hawajamkiri Yesu. Mungu Baba hamchukii mwanadamu. Na kama una uhakika ni watakatifu basi ni vema, kwani imetupasa wote kuwa watakatifu ili tuweze kumwona Baba. Kazi yangu hapa duniani ni kuwataka watu wote wampokee Yesu Kristu ambaye ndiye kiunganishi na Mungu Baba. Yeye pekee ndiye njia, na kweli, na uzima. Kwamba wawaita mashetani, hilo ni lako. Kwamba ni lazima wampokee Kristu, hiyo ndiyo njia ya kweli. Sauli alikuwa mtume akiwa gizani? Au alimpokea Kristu, akabatizwa, akapokea na Roho Mtakatifu? Soma biblia yako vizuri usipotoshe watu. Mungu hamwokoi mtu ndani ya dhambi zake bali kutoka katika dhambi. Hivyo watu wote yatupasa kuokoka ili tufike mbinguni.

Mungu hamchukii mwanadamu, lakini siku ya hukumu atawatupa wote wenye dhambi katika moto wa milele. Hivyo tuwaeleze watu ukweli kwamba kutenda dhambi ni kujitenga na Mungu, na ni kwa sababu hiyo Kristu alikuja duniani ili kutupatanisha na Mungu. Tusiwadanganye watu waenende katika dhambi kwani ni kutothamini kazi ya Kristu msalabani. Ndio maana tunawataka watu wamtazame Kristu msalabani wapate kutakaswa dhambi zao. Sisi tunawahubiria kile tunachokiamini kuhusu kazi ya ukombozi aliyofanya Kristu. Tutaendelea kumshuhudia Kristu mpaka watu wote wasikie, bila kuogopa watu wanaodhani tunahukumu. Ni matching orders walizopewa mitume na Yesu mwenyewe.

Je mpaka hapo umegundua kitu gani?
Haya mambo yote tunayojadili hapa hayapatikani Samunge!

Mungu akubariki sana.
 
kumbuka mungu eweza kutumia njia yeyote kudhihirisha ukuu wake, je musa alipotumia nyoka wa shaba jangwani ilikuwa ibada ya sanamu?
 
Sasa ushetani uko hadharani na shetani ameshaona mwitikio wa watu sasa ndo kazidisha kufungua matawi. Rozari ni nyenzo mojawapo azitumiazo shetani kuwahadaa watu. Shetani sasa ana matawi Mbeya, Tabora, na Morogoro kaibuka dada wa kiislamu naye na kikombe chake. Hii ni balaa. MUNGU aiponye nchi yetu na hawa waganga wa kienyeji.

Hapa kwenye Red mkuu, unakwaza imani za watu wengine, ambao hawashiriki kabisa katika malumbano haya. Ni afadhali ungesema rozari aliyovaa huyo dada ndo ina lengo hilo kuliko the way ulivyo wasilisha hoja yako
 
Nashukuru saaana kwa hoja zako. Mimi hata siku moja siongozwi na jazba. Na ndio maana nilichagua kutomjibu huyo aliyenitukana (kama hiyo ndiyo waiita kweli). Pamoja na sympathetic language yako mambo ambayo tunakubaliana kama ifuatavyo:

Ni wapi ambapo nimehukumu? Nimeuliza kwa lugha ya picha tu kutaka kujua kama hawa nao (imekuwa ikiandikwa humu forum kwamba walikuwa Samunge) wamempokea Yesu? Lengo langu lilikuwa kuonyesha jinsi gani kazi ya Kristu inawaleta watu kwake. Kwamba wanadhambi, sijawahi kusema. Kwamba wanaokwenda Samunge wanakiri kazi ya Kristu, nitauliza kila siku. Kama kwako huko ni kuhukumu, basi unihesabu hivyo.

Kuhubiri injili. Hivi unajua msingi wa injili ni nini? 1 Cor. 15:1: "Moreover, brethren, I declare unto you the gospel which I preached unto you, which also ye have received, and in which you stand By which also you are saved, if you keep in memory what I preached unto you, unless you have believed in vain. For I delivered unto you first of all that which I also received, how that Christ died for our sins according to the scriptures; And that he was buried, and that he rose again the third day according to the scripture." Hivyo hiyo injili aliyoihubiri yeye na kukufanya wewe kuwashambulia wakristu kwamba wanahubiri dini sijui ni ipi?

Umesema vema, kila aliitiae jina la Bwana. Hebu jiulize ni jina gani hilo. Tena jiulize hao muendao Samunge mnaliitia jina hilo? Na ndio msingi mkuu wa swali langu hapo awali. Je, kweli hilo jina mnaliitia mpate kuokolewa? Kama hilo linatokea Samunge, haleluya. Kristu ni mtawala pale. Mambo ya vague statements kwamba pale Samunge ni Mungu na si Kristo, haipo kibiblia. This is another gospel.

Sisi hatupaswi kuhukumu, bali imetupasa kuonyana na kuelezana iliyo kweli bila kuogopa watu watakaodai tunawahukumu. Kama kile nachokueleza kitakupelekea kwenye wokovu wa kweli, siwezi nyamaza. Vinginevyo ungependa injili ihubiriwe vipi? Injili haibembelezi. Palipo makosa yatopimwa kutokana na maandiko na kuwekwa wazi ili watu wajirudi. Ndivyo walivyofanya mitume. Sihubiri injili ya kuvumiliana. Nahubiri injili inayomhusu Kristu pekee, hivyo nje ya huyo siamini yale unayotaka niamini.

Wokovu ni neema. Unaelewa maana yake lakini? Kwamba hukuhitaji kufanya jambo lolote ili uokolewe. Si kwa kujitesa, wala kutoa mali yako yoyote wala chochote kile. Ni bure. Ndio maana nawahubiria wengine neema hii ya Kristu. Ama ungependa makanisa yafungwe ili tuiache neema ifanye kazi? Hapana, tutaendelea kumhubiri Kristu. Ni agizo la kristu hata kama wengine mtachukia.

Hao watu kama ni watakatifu sana na wenye kufaa hiyo ni judgement yako. Mimi nalitumia mfano halisi wa watu wanaofahamika kufikisha ujumbe. Kwamba wanamkiri Yesu, nitaendelea kuhubiria wao na wengine woote ambao hawajamkiri Yesu. Mungu Baba hamchukii mwanadamu. Na kama una uhakika ni watakatifu basi ni vema, kwani imetupasa wote kuwa watakatifu ili tuweze kumwona Baba. Kazi yangu hapa duniani ni kuwataka watu wote wampokee Yesu Kristu ambaye ndiye kiunganishi na Mungu Baba. Yeye pekee ndiye njia, na kweli, na uzima. Kwamba wawaita mashetani, hilo ni lako. Kwamba ni lazima wampokee Kristu, hiyo ndiyo njia ya kweli. Sauli alikuwa mtume akiwa gizani? Au alimpokea Kristu, akabatizwa, akapokea na Roho Mtakatifu? Soma biblia yako vizuri usipotoshe watu. Mungu hamwokoi mtu ndani ya dhambi zake bali kutoka katika dhambi. Hivyo watu wote yatupasa kuokoka ili tufike mbinguni.

Mungu hamchukii mwanadamu, lakini siku ya hukumu atawatupa wote wenye dhambi katika moto wa milele. Hivyo tuwaeleze watu ukweli kwamba kutenda dhambi ni kujitenga na Mungu, na ni kwa sababu hiyo Kristu alikuja duniani ili kutupatanisha na Mungu. Tusiwadanganye watu waenende katika dhambi kwani ni kutothamini kazi ya Kristu msalabani. Ndio maana tunawataka watu wamtazame Kristu msalabani wapate kutakaswa dhambi zao. Sisi tunawahubiria kile tunachokiamini kuhusu kazi ya ukombozi aliyofanya Kristu. Tutaendelea kumshuhudia Kristu mpaka watu wote wasikie, bila kuogopa watu wanaodhani tunahukumu. Ni matching orders walizopewa mitume na Yesu mwenyewe.

Je mpaka hapo umegundua kitu gani?
Haya mambo yote tunayojadili hapa hayapatikani Samunge!

Mungu akubariki sana.

Nataka tushauriane mimi na wewe katika mambo hayo niliyo weka red. Umesema hujahukumu na chini yake unaniuliza kama hao watu hao ni watakatifu basi huyo ni mimi. Sasa ni kuwa kwahabari ya utakatifu ama wadhambi mimi sijui maana hukumu ni ya mtu mwenyewe na Mungu kwani neno la Mungu linatuambia tujihoji na kuhukumu dhamira yetu lakini katu haturuhusiwi kwa mwingine. Ila neno la Mungu linasema kila mwanadamu ameumbwa kwa mfano wa Mungu hivyo tuwapende na kuwathamini kupendo hauhukumu kwa hivyo upendo wangu kwa hao watu unaniambia ni watu wenye kufaa sana maana wameumbwa kwa sura na mfano wa Mungu.

Swala lingine ni hukumu ya siku ya mwisho. Kwamba watenda dhambi wataenda motoni hilo halina ubishi lakini ni kinani hao, hilo jibu analo Mungu na si mwanadamu kwani hakuna ajuaye roho ya mwanadamu isipokuwa Mungu na yule mwenye hiyo roho. Lakini kila mtu kabla ya kufa ni candidate wa either Jehanam na paradiso kwani neno la Mungu linasema mtu hufa mara moja na baada ya hapo ya hapo hukumu; ni vipi wewe wamhukumu mtu aliye na pumzi na bado hajafa? Dhambi kubwa itakayo peleka watu motoni ni kukataa neema na hiyo neema huja kwa mtu na mtu kwa nyakati tofauti vipi je kama hiyo neema bado haija wafikia hao ambao unaowahukumu? Lakini neno la Mungu linatambua wapo ambao hata baada ya kupata neema na kupokea wokovu waweza kukataa kuishi ndani ya hiyo neema na hivyo kumsulubisha kristo mara ya pili; hao kwa hakika wanatenda dhambi ya kumkufuru roho mtakatifu ambayo haiwezi kusamehewa. Basi imetupasa kujihesabu kama watumwa wasio na faida bali kuitenda kazi ya bwana bila kunung'unika wala kuhuku ili kwa kipimo hicho tukipimacho nasi tuhesabiwe haki.

Ubarikiwe mtumishi wa bwana!
 
Tazizo lako ni kushindwa kuonyesha hasa ni wapi nimesema JK na Mahita wanadhambi. Onyesha halafu tutaendelea. Au hujui kuhukumu ni nini? Mimi nimeonyesha watu wa imani tofauti na Yesu ili tu kujua kama sasa wanamtangaza Kristu. Hiyo ni hukumu? Bila Kristu twajidanganya, tena twawapoteza wengi.
 
kumbuka mungu eweza kutumia njia yeyote kudhihirisha ukuu wake, je musa alipotumia nyoka wa shaba jangwani ilikuwa ibada ya sanamu?

Na sasa tunaye Kristu aliye mfano wa huyo. Hatuhitaji kurejea tena kwenye nyoka wa shaba. Vinginevyo Kristu alikufa bure
 
Tazizo lako ni kushindwa kuonyesha hasa ni wapi nimesema JK na Mahita wanadhambi. Onyesha halafu tutaendelea. Au hujui kuhukumu ni nini? Mimi nimeonyesha watu wa imani tofauti na Yesu ili tu kujua kama sasa wanamtangaza Kristu. Hiyo ni hukumu? Bila Kristu twajidanganya, tena twawapoteza wengi.

Sikuwa nimekusoma vizuri sorry mtumishi Mungu akubariki. Tuko pamoja!
 
wapendwa Nyenyere na Ame Mungu awabariki sana kwa ufafanuzi wenu mzuri na sahihi wa maandiko. Mungu awazidishie hekima na bidii katika kazi yake.

kisha aliwaambia wasitoke yrusalemu
hadi watakapovikwa ile nguvu itokayo juu kwa Baba
 
Back
Top Bottom