KKKT na babu wao waanza rasmi biashara

Oooow...kashfa zimeshaanza,ni imani yangu kua Babu hatojali propaganda hizi na badala yake ataendelea na wito wake kwa kazi aliyotumwa! Nadhani wenye matatizo ni wengi kuliko wapuuzi ambao ni wachache!
 
ibada ya kikombe ni ibada ya sanamu. hata wanaoziabudu sanamu hawasemi kuwa wanaiabudu ile sanamu, bali husema wanamuabudu Mungu aliye ndani ya ile sanamu!

zinduka ndugu yangu, Mungu wetu hawezi kuwemo kwenye kikombe, Mungu wetu anakaa mioyoni mwetu.

Bwana kwetu sisi ni kimbilio na nguvu, ni msaada utakaoonekana tele hata wakati wa mateso. kikombe hakiwezi kuwa kimbilio na nguvu yetu kama vile sanamu isivyoweza kuwa kimbilio na nguvu yetu. mtu yoyote akimbiliaye kikombe wakati wa mateso (kama hayo ya maradhi) anashiriki ibada ya sanamu. hana tofauti na yule aipigiaye magoti sanamu na kuiabudu. mkiijua kweli, hiyo itawaweka huru. mbarikiwe sana

sisi hatutaogopa ijapoharibika nchi
na kutetemeka milima moyoni mwa bahari
na tutakapomaliza vita hivi kwa ushindi wa Mwana Kondoo tutapewa kula matunda katika ule mti wa uzima

kila m2 anauelewa wake juu ya imani, usitake wa2 waielewe kama wewe. Ni haki wenye shida kutafuta kuifwata hiyo dawa maana ndo kimbilio lao kwa sasa
ni maoni yangu.
 
kila m2 anauelewa wake juu ya imani, usitake wa2 waielewe kama wewe. Ni haki wenye shida kutafuta kuifwata hiyo dawa maana ndo kimbilio lao kwa sasa
ni maoni yangu.
Kimbilio litabaki kuwa Yesu Kristo pekee.
 
Nyenyere b4 colonial era watu walikua na imani zao na namna zao za kuwasilana na Mwenyezi Mungu...baada ya ukoloni tumepata njia "za kistaarabu" kuwasiliana na Mungu...sivyema kusahau asili moja kwa moja! Haya ya Yesu/Mtume tuyaache ili tusimkosee Mwenyezi Mungu!
 
KNACHOSHANGAZA...... HIVI HATUJIULIZI!!?
MBONA WALE MA-BABU, BIBI, ANKO, ANTI, SHAROBARO WANAOGAWA VIKOMBEZ HAWATANGAZWI NA VYOMBO VYA HABARI KAMA BABU WA LOLIONDO?

Kuna siri gani hapo???
 
we dada unayejiita miss judith ni mwendawazimu tu. Hakuna jingine dadaangu
....naogopa sana kusema "MARA NYINGI WENDAWAZIMU HUWAONA WAZIMA NDIO WENDAWAZIMU!" Hii ina maana kwamba "mbwa hujiona ndio kiongozi wa mmiliki wake.. ndio mana mnaotembea na mbwa wako yeye hutangulia mbele"

Ukipanua akili hapo utanielew vema!

Namaanisha kwamba 'KILA MMOJA ATETEE KWA HOJA ANACHODHANI NI SAHIHI NA AELEWEKE. Kama mtu atatumia lugha ambayo inafurahisha masikio na macho yake asidhani HATOJIBIWA kwa lugha ya aina hiyohiyo ambayo itafurahisha upande mwingine!
 
Kama wewe si mgeni humu jamvini wala huwezi kupoteza muda wako na watu hawa wawili ambao ni mwili mmoja.

Did you find this post helpful? |
icon1.png
Re: Kumbe wahindi walioteshwa kabla ya "babu"


Miss Judith ndiye Mohammed Shossi wala msijisumbue nina uhakika 100%​

judith a.k.a shoshi inawezekana? Shoshi ni mpemba aliyekuwa bara kwa masomo ya stashahada mpaka mwaka 2007. Kama kweli kajihita Judith basi kadhalilika. Kwa kurudi msitarini, Miss Judy nadhani ni mfuasi wa mungu asiye Mungu Muumba. Yeye kavaa gwanda la kumtetea mungu anayemjua yeye peke yako. Kama babu si kutoka kwa Mungu Muumba, uyu Judi kajuaje kama si muabudu gizani? Kamwe haujatokea muugiza wala ishara ya kuonesha babu Loliondo hajatumwa na Mungu,na wote wapingao bila kuonesha ushaidi kuwa Mungu hajamtuma babu,basi wote wako gizani na wanaongozwa na giza kuipinga nuru. Kwa babu si dini wala kabila,yeye anatoa dawa tu!
 
MAOMBI NDIYO SILAHA KUBWA. TUANGALIE TUSIJE TUKABAKI NA MALUMBANO, NA MANENO MENGI, WAKATI DAWA YA MAMBO YOTE NI MAOMBI. KAMA TUNAVIPIGA VITA VYA IMANI, SILAHA NI MOJA TU. MAOMBI, KWA HIYO NINYI WATU MNAODHANI MKO KIROO, PUNGUZENI MANENO, ZAMENI KWENYE MAOMBI. Mbarikiwe.
 
Mtu anapojiona si mwehu kwa kujilinganisha na wehu..hivi tukichunguza sana si tutakuta binadamu wote ni wehu? Kwa mfano hebu chunguza wale wanaoomba kura na wale wanaoombwa kura,km kuna totauti na wehu. Au wale wanaoiba kura ilihali wakijua hawana uwezo wa kuongoza na wale wanaojua wanaibiwa wanakubali kuibiwa kabla hawajaibiwa! Ngoja niache maana sitaki ushahidi maana na mimi ni mwehu ila najijua!
 
kama huyo mzee wa laliondo amepewa kipaumbele kama mkombozi wa magonjwa sugu,basi na hawa walio jitokeza wapewe basi waheshimike kwa sababu bado wanafanya kazi ile ile ya kikombe lasi hivyo itaonekana kama bihashara,halafu na hao watoa vikombe wasipondeane kama kweli wameoteshwa kweli
 
Judith naamini hujambo! What is wrong if ELCT builds a better place for people who are coming to get cured of deadly diseases? Are you angry because of that? Or you just don't like the idea that people are getting healed? I am surprised! If you are one of those who are against what God is doing in Samunge then you still have a long way to go because God isn't done yet with His precious people. If what I am saying about your attitude is not true then perhaps you are speaking, thinking and writing out of total ignorance! If this is true then you need to take time to learn and think before you start a topic.

Any ministry has to be supported by people of good will, and what Pastor Masapila is doing there deserves to be supported because he is doing what God commanded him to do and if you don't believe what God is doing there it is better to keep quiet as it is wiser than opposing you really don't know. Keep in mind that God uses people as he pleases and according to His own will. He also uses weak people and things to ashame the great! So I would advice you to keep silence or at least pray if you doubt that what Pastor Masapila is doing is not from God. Many people have been healed from different ailments and to me healing cannot be Satan's work. It is God's work and healing is one of Jesus' works He came to do according to Isaiah 53. Building a place for the purpose of administering God's people is the right and noblest thing the church (the body of Christ) can do.

If you do not believe in what Pastor Masapila is doing you still have a long way to go. You will have to wrestle with the testimonies of those who got healed by God through the ministry of pastor Masapila. Let me remind you a story of a man who was born blind in John 9 who suffered the ridicule and the questioning of the Pharisees. God read that story of this man and you will see that neither the Pharisees nor any one can refute or render false what God does. At the end the blind man said call Him whatever but what I know is this: "If He's a sinner I don't know. What I know is that I was blind but now I see." Dear Judith, God is not limited by geographical boundaries or denominational lines. He's a God of all mankind and He uses anyone from any where to accomplish His purposes for the glory of His holy name.

May God the Father of our Lord Jesus Christ the Wounded Healer enlighten you so that you may know the truth about His will. Jesus told His disciples who came with a complaint about a man who was casting out demons in His name and Jesus' answered them and I am parahrasing what He said, "If anyone is not against us he is for us" (Read Mark 9:38). What side are you Judith?

Well said Oldarasu. You know some people simply critic things for fame. It is wise not to say much or to comment after you have given a critical thinking to the issue. Martin Luther once said in one of his writings "There is no wisdom save in truth. Truth is everlasting, but our ideas about truth are changeable. Only a little of the first fruits of wisdom, only a few fragments of the boundless heights, breadths and depths of truth, have I been able to gather."
What is the "truth" that is being referred here to? When Jesus speaks about the truth, he refers to himself as the truth...truth is a wholistic manifestation of God...and I mean wholistic not some propositional truth. In other words, when the Bible speaks about truth is invites us to see God/Jesus for who he is...and Who is God? And our Lord Jesus is God’s definitive and perfect Word expressing who God is, what He’s like, who we are, and what we need to do to be saved from misery and futility. God is love incarnate...and that love is the major part of that truth. When Jesus came on earth he manifested that love not simply through concepts or empty words but through actions. Healing ministry was part and parcel of that manifestation of love. So the church is commanded to love not with tongue or mere words as Apostle John puts it: "Dear children, let us not love with words or tongue but with actions and in truth." 1 John 3:18. The church is given the same mandate....to show love through actions that is why they have built many hospitals....So Judith must also be against these church hospitals!!!! I am sure you, your family, and friends are recipients of the church social ministry of healing through their hospitals. For that you don't make a noise but only when ELCT decides to build a shelter in Samunge...why is that such a bitter thing for you? Plus you say KKKT na babu wao" na kama ni KKKT na babu wao, why is it any of your business if they built a shelter as part of the healing ministry there? Have they asked you to contribute? Why is that account such an issue for you? Please take time to think before you utter perverse words in public in order to offend the whole Church...remember ELCT is not an individual, it is some of us who are reading your comments and many more millions in Tanzania and we have nothing against that.



So Judith spare ELCT and their Babu....and like Oldarasu I say what Jesus teaches us..."If anyone is not against us he is for us." God bless you with broader discernment of his Word
 
1. Of course, ndiyo maana sasa kuna Mbeya, Mtwara, Morogoro, Tabora, Mwanza, Kigoma and believe me this god isn't done yet!

2. Mungu amesema tupime kila jambo kulingana na maandiko. Vinginevyo nyie mna-act out of ignorance kwa kutoyajua maandiko.

3. BIG NO! Siyo kila ministry, bali ni zile zinazotangaza utukufu kwa Mungu juu mbinguni. Mungu aliyemtuma mwanaye ya pekee ili kila amwaminiyee asipotee. Yule aliyekuja ili wawe na uzima kisha wawenao tele.

4. Mungu yupi aliyemwamuru?

5. Tumeamuriwa tuiseme iliyo kweli na siyo kukaa kimwa na kutazama tu. Tutadaiwa siku ya mwisho.

6. Mapenzi ya Mungu kwa wanadamu ni yapi?

7. What about traditional healers?

8. Yesu alikuja kutafuta kilichopotea, hakuja kuwaponya watu gizani na kuwaacha wafurahie afya njema katika giza. Yeye ni nuru ya ulimwengu. Popote palipo na nuru giza hutoweka. Hivyo kama nuru hiyo ipo Samunge, basi hakika watu wanakombolewa kutoka gizani.

9. Huduma gani ya kiroho wanayopata ambayo ndiyo msingi wa huduma za kanisa?

10. NOT TRUE. Mwisho yule kipofu alikiri kuwa Yesu ni Kristo mwana wa Mungu. Hata familia yake ilikiri.

11. Ndio maana tunashangaa masharti ya kutosogea hata kilometa moja toka samunge vinginevyo dawa haitafanya kazi. Ni Mungu gani basi huyo?

12. His purpose was not healing, but all mankind attain eternal life. Alikuja ili wawe na uzima kisha wawenao tele.

13. Well said. Do we hear His name in Samunge? I wonder...!

Better read the Bible and God will shine His light in you.

Mungu akubariki.


mpendwa,

ubarikiwe sana kwa majibu haya mazuri na ya mstari kwa mstari. kweli watu wako gizani. inahitajika nuru ya Mungu iangaze. watu wanamtetea babu kama vile wa,eishamkubali kuwa mungu wao.

kweli hatupaswi kukaa kimya, lazima tuiseme kweli na tuitetee, ni wajibu wetu kama wakristo. maombi pekee bila kusoma maneno ya Mungu ni sawa na kuomba ukiwa kipofu. tumepewa neno la Mungu liwe taa na mwangaza katika maisha yetu.

nakuombea heri na baraka zisikupungukie maishani mwako mpendwa

.....ili litimie neno lililonenwa kwa kinywa cha nabii akisema:
zabuloni na naftali, ng'ambo ya yordani, galillaya ya mataifa
wale watu waliokaa katika giza na uvuli wa mauti nuru imewaangazia
 
Dhambi ni kunywa dawa au asili ya dawa au kuumwa?
Je kuhusu zile amri kumi za mungu je?
Tuache unafiki tujadili ukweli na uhalisia si ubishani...mwenye degree ya bible atuwekee hapa
 
Nyenyere b4 colonial era watu walikua na imani zao na namna zao za kuwasilana na Mwenyezi Mungu...baada ya ukoloni tumepata njia "za kistaarabu" kuwasiliana na Mungu...sivyema kusahau asili moja kwa moja! Haya ya Yesu/Mtume tuyaache ili tusimkosee Mwenyezi Mungu!

I can tell where your faith is. Lakini nakuacha na simple qn: babu ni dini gani? Je, unaelewa mkristo ni nani?

Jesus is the only way to heaven.

2 WAKORINTHO 5 : 17
HATA IMEKUWA MTU AKIWA NDANI YA KRISTO AMEKUWA KIUMBE KIPYA, YA KALE YAMEPITA TAZAMA YAMEKUWA MAPYA!

Hivyo achana na habari za ukoloni hapa.
 
kama huyo mzee wa laliondo amepewa kipaumbele kama mkombozi wa magonjwa sugu,basi na hawa walio jitokeza wapewe basi waheshimike kwa sababu bado wanafanya kazi ile ile ya kikombe lasi hivyo itaonekana kama bihashara,halafu na hao watoa vikombe wasipondeane kama kweli wameoteshwa kweli

Tena bibi wa Tabora anaonekana kuwa mkali kuliko babu!
 
Miss Juddy humu kuna watu wa imani mbalimbali.kwa kuwa wewe ni muumini wa KKKT maoni yako kayatoe kanisani au kwa askofu mkuu wa KKKT..hasa yule laizer,humu naona unawachezea wamasai taarabu.ama nenda loly ukamuhoji babu then uje na kitu kipya...sio ubishi tuu kutwa kucha...TURUDI KULE mmu TUELIMISHANE ZAIDI YALE MAMBO YETU
 
Tena bibi wa Tabora anaonekana kuwa mkali kuliko babu!

.
Ooh, inaonekana umemkubali bibi ila sii babu.
Watu wameshtuka kwamba wapinzani wa babu wametengeneza waigizaji wengi ili kuleta vurugu. Tunachomsukuru Mungu ni kwamba waigizaji wamefunikwa kwani chema kinajiuza chenyewe, kibaya kinatapatapa kujiuza kwa kuomba utambulisho.
.
 
Kwenye hizo red kweli Mungu hadhihakiwi. Nitakurudia baadaye nikufundishe NENO la Mungu badala ya kutoa mafundisho ambayo yanashambulia kazi ya Kristo hapa duniani. Pole sana ndugu kwa kufura hasira namna hiyo. Kumbuka tu kuwa imetupasa kudhibiti hasira zetu.

Mungu akubariki.

Mpendwa kabla ya kuhukumu jiangalie wewe umechangia kiasi gani yeye kufikia hali hiyo? Pamoja alichokisema kakisema kwa hasira lakini kasema ukweli ambao wakristo wengi kwa sababu ya selfishness wameshindwa kuhubiri injili na kuishia kuhubiri dini, makanisa na vyeo vyao. God is not respector of persons, kwake kila aliitiaye jina la bwana humokoa pasi kujali ni nani na hukumu ni yake wala sisi hatupasi kuhukumu kwani hata sisi wokuvu wetu ni kwa neema na wala si kazi ya mikono yetu. Ingekuwa si neema basi ungeketa wewe uko huko club unabadilisha chupa za bia kwa frustrations za maisha. mbele ya Mungu mahita na JK ni watakatifu sana tena wenye kufaa sana maana kawaumba kwa sura na mfano wake ila kwetu sisi tunaweza waita mashetani. Kama ndivyo kuwa wao hawafai kiasi hicho basi Sauli asingeweza kuwa mtume aliyefanya kazi ya Bwana kwa nguvu na akili zake zote hata akafikia hatua ya kuona kuishi kwake ni kristo na kufa ni faida.

Mungu hamchukii mtenda dhambi bali anachukia dhambi tujifunze kutenganisha haya mawili. Maana mtenda dhambi alimfanya Mungu akaja duniani na kumpokea alivyo na dhambi zake apate kumsafisha na kumfanya mwenye kufaa sana. Dhambi haikuwahi kumfanya Mungu kufanya kitu kwaajili yake. Kazi ya utakaso ni ya Mungu mwenyewe kwa damu ya kristo so tusiwa hukumu watenda dhambi kwani mwanawaadamu hakuja hukumu bali kutafuta kilichopotea, apate kuitenga dhambi na wanadamu hata ziwe mbali nao kama ilivyo magaribi na mashariki. Vipi wewe kuhukumu kitu cha mtu mwingine? Imetupasa kuhubiri habari njema ya msamaha wa dhambi lakini kuondoa hizo dhambi si kazi yetu, hiyo kazi aliimaliza Yesu mwenyewe pale kalvari. Hapo Kalvari alilipa deni na binadamu wote wako huru kupokea msamaha saa yeyote watakapo amua kuipokea na pale ambapo Mungu atawapa neema hiyo kwanjia anayoijua yeye.
 
huyu hapa bibi wa tabora na rozali yake shingoni!


03_11_rs6zzs.jpg
Dada Magreth Mutalemwa mkazi wa Urban Quarter Uzunguni, Tabora Mjini, ambaye naye amejitokeza na kudai kuoteshwa kutibu watu na Bikira Maria, akiwa na kikombe chake cha dawa akiombea wagonjwa kabla ya kuwanywesha dawa nyumbani kwake. (Picha kwa Hisani ya Keronyingiblog).

source: HabariLeo | Gwiji la Habari Tanzania

more to come, stay tuned!

sisi tumemfanya Bwana kuwa kimbilio na nguvu yetu,
hivyo hatutaogopa hata ijapotetemeka milima moyoni mwa baharii

Sasa ushetani uko hadharani na shetani ameshaona mwitikio wa watu sasa ndo kazidisha kufungua matawi. Rozari ni nyenzo mojawapo azitumiazo shetani kuwahadaa watu. Shetani sasa ana matawi Mbeya, Tabora, na Morogoro kaibuka dada wa kiislamu naye na kikombe chake. Hii ni balaa. MUNGU aiponye nchi yetu na hawa waganga wa kienyeji.
 
Back
Top Bottom