KKKT na babu wao waanza rasmi biashara | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

KKKT na babu wao waanza rasmi biashara

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Ms Judith, Mar 31, 2011.

 1. Ms Judith

  Ms Judith JF-Expert Member

  #1
  Mar 31, 2011
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 2,569
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  Babu Loliondo ajengewa jengo la milioni 100
  • Ni mchango wa KKKT, litamwezesha kutibu watu 700 kwa mpigo

  na Mwandishi wetu


  [​IMG] KATIKA kuboresha tiba ya maono ya Mchungaji Ambilikile Mwasapile ‘Babu' katika Kijiji cha Samunge, wilayani Ngorongoro, Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Kaskazini Kati itajenga jengo la mviringo litakalohudumia watu 700 kwa wakati mmoja, litakalogharimu zaidi ya sh milioni 100.
  Hatua hiyo ya kanisa imekuja wakati muafaka tangu kuanza kwa tiba hiyo miezi mitano iliyopita watu na wagonjwa walikuwa wakisimama katika jua kali na wakati wa mvua hususan hizi za masika wakisubiri kupata ‘kikombe cha Babu' katika adha kubwa.
  Akizungumza na waandishi wa habari jana Arusha, Askofu Thomas Laizer, alisema jengo hilo litakuwa na vyumba vya kuchemshia dawa zitakazotolewa na Babu, chumba cha kuhifadhi dawa hizo, ambapo sehemu ya ukumbini kutakuwa na jukwaa la kutolea huduma hiyo katika mistari mitano ya watu 20, kila mstari kwenda kupokea dawa hiyo.
  Alisema ujenzi wa jengo hilo utaanza hivi karibuni, ambapo eneo la ujenzi wake limeshapatikana karibu na anakotolea huduma mchungaji huyo aliyepata umaarufu wa aina yake kutokana na tiba hiyo, ambapo michoro ya jengo hilo inakaribia kumalizika.
  "Sisi kama kanisa tumeona ni wakati muafaka wa kujenga jengo hilo kwa ajili ya kuhifadhi watu hao ambapo kwa muda wote tangu kuanza kwa tiba hiyo watu na wagonjwa wanaotoka maeneo mbalimbali nchini na nje ya nchi walikuwa wakisimama kusubiri tiba hiyo," alisema Askofu Laizer.
  Sambamba na hatua hiyo, kanisa hilo limefungua akaunti maalumu katika Benki ya CRDB Na. 0150036432600, ambapo aliwaomba watu wenye mapenzi mema kuchangia huduma zinazotolewa na Mchungaji Mwasapile ili ziwe endelevu.
  Katika hatua nyingine, Mkuu wa Wilaya ya Ngorongoro, Elias Wawa Lali, amesema kuwa foleni katika Kijiji cha Samunge imeanza kupungua kwa kiwango kikubwa na anao uhakika kwamba muda uliotolewa na mchungaji huyo utafikiwa.
  Aidha, alikiri kuwa kulikuwepo na madereva wakorofi ambao walikuwa wakichakachua njia ya Longido hadi Ziwa Natron na kumfikia Babu kirahisi na kusema kuwa hiyo ilitokana na watu wa Longido kuchelewa kuweka kizuizi ambapo sasa hali hiyo imerekebishwa.
  Wakati hayo yakiendelea, makusanyo ya sadaka inayotolewa na wagonjwa ya sh 500 wakati wakipatiwa kikombe na Babu yamefikia sh milioni 50 tangu kuanza kwa tiba hiyo mwishoni mwa mwaka jana ambapo kanisa katika mgawo wake utakaoingia moja kwa moja katika ujenzi ni sh milioni 20. Fedha nyingine zinabakia katika matumizi ya kawaidi na kidogo kwa ajili ya Babu.


  source: Babu Loliondo ajengewa jengo la milioni 100

  ngoma ikilia sana i-karibu na kupasuka, yetu macho,

  lama injili imesitirika, basi imesitirika kwao wasioamini ambao mungu wa dunia hii amewapofusha nafsi zao isiwazukie nuru ya utukufu wake Kristo aliye sura ya Mungu
   
 2. Mwita Maranya

  Mwita Maranya JF-Expert Member

  #2
  Mar 31, 2011
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 10,569
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  The same old shit,......

  Huna jipya judith, kadanganye wengine lakini hapa hakuna kitu!!
   
 3. Zemu

  Zemu JF-Expert Member

  #3
  Mar 31, 2011
  Joined: Jun 5, 2008
  Messages: 517
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  :tape:
   
 4. M

  Mwera JF-Expert Member

  #4
  Mar 31, 2011
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 968
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hiyo ni biashara,yalisemwa tokea mwanzo ila sasa ndio mambo yako wazi,ni biashara ya kkkt,a.k.a kunywa kikombe kimoja tu.
   
 5. NewDawnTz

  NewDawnTz JF-Expert Member

  #5
  Mar 31, 2011
  Joined: Nov 15, 2010
  Messages: 1,675
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0

  Mungu anakazi jamani

  Haya unataka kusema nini hapa, "kanisa latumia sadaka kujengea mchawi nyumba ya kunogeshea uchawi wake" au tukueleweje

  Ni hatua nzuri by any mean, hata kama sio kwa mtazamo wa kidini basi kwa mtazamo wa kijamii kuwa wanajamii wanahitaji sehemu bora kwa ajili ya kupata huduma
   
 6. Ms Judith

  Ms Judith JF-Expert Member

  #6
  Mar 31, 2011
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 2,569
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  nyie ngojeni tu mamilioni yatakavyoanza kufurika kwenye hiyo ajaunti waliyofungua CRDB ndio mtajua kuwa ni biashara!

  Mungu kwetu sisi ni kimbilio na nguvu
  msaada utakaoonekana tele wakati wa mateso
   
 7. Sigma

  Sigma JF-Expert Member

  #7
  Mar 31, 2011
  Joined: Feb 26, 2011
  Messages: 5,015
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Kituo chake cha maombezi sadaka imeadimika, yote babu kabeba, wategemea response yake ni nini?
  Heal babu, heal.
   
 8. RealMan

  RealMan JF-Expert Member

  #8
  Mar 31, 2011
  Joined: Nov 9, 2010
  Messages: 2,352
  Likes Received: 160
  Trophy Points: 160
  [​IMG] Nini ukweli wa Dawa ya magonjwa sugu ya Mchungaji Ambilikile wa Loliondo?

  Kuna ukweli kwamba ameoteshwa na ina nguvu za Mungu? 1191 47.9%
  Ni dawa ya uhakika na salama isiyoingiliana na upande wowote wa dini wala ushirikina? 381 15.3%
  Ni utapeli wa kujipatia pesa tu kama baadhi ya waganga wengine wa jadi? 360 14.5%
  Ni dawa ya kienyeji ambayo ina nguvu za kuponesha magonjwa sugu? 345 13.9%
  Ina uhusiano na 'freemason'. 207 8.3%

  Number of Voters : 2484 First Vote : Friday, 18 March 2011 16:21 Last Vote : Thursday, 31 March 2011 07:12

  http://www.mwananchi.co.tz/component/poll/10-nini-ukweli-wa-dawa-ya-magonjwa-sungu-ya-mchungaji-ambilikile-wa-loliondo.html
   
 9. Ms Judith

  Ms Judith JF-Expert Member

  #9
  Mar 31, 2011
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 2,569
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  huyu hapa bibi wa tabora na rozali yake shingoni!


  [​IMG] Dada Magreth Mutalemwa mkazi wa Urban Quarter Uzunguni, Tabora Mjini, ambaye naye amejitokeza na kudai kuoteshwa kutibu watu na Bikira Maria, akiwa na kikombe chake cha dawa akiombea wagonjwa kabla ya kuwanywesha dawa nyumbani kwake. (Picha kwa Hisani ya Keronyingiblog).

  source: http://www.habarileo.co.tz/

  more to come, stay tuned!

  sisi tumemfanya Bwana kuwa kimbilio na nguvu yetu,
  hivyo hatutaogopa hata ijapotetemeka milima moyoni mwa baharii
   
 10. Tuko

  Tuko JF Bronze Member

  #10
  Mar 31, 2011
  Joined: Jul 29, 2010
  Messages: 11,186
  Likes Received: 397
  Trophy Points: 180

  Inakuuma nini!!!!!!
   
 11. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #11
  Mar 31, 2011
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,762
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  judith bwana unanichekesha kweli bado unao tuuu nia yako ni nini hasa! TUAMBIE BASI TUJUE!
   
 12. L

  Leornado JF-Expert Member

  #12
  Mar 31, 2011
  Joined: Nov 12, 2010
  Messages: 1,534
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
 13. Nyenyere

  Nyenyere JF-Expert Member

  #13
  Mar 31, 2011
  Joined: Sep 9, 2010
  Messages: 8,567
  Likes Received: 1,930
  Trophy Points: 280
  Muifahamu kweli ili muwe huru.
   
 14. Kiby

  Kiby JF-Expert Member

  #14
  Mar 31, 2011
  Joined: Nov 16, 2009
  Messages: 5,202
  Likes Received: 1,007
  Trophy Points: 280
  Heading yako ni tofauti na ya gazeti ulilo-copy na kui-paste hapa jf.
  Je baada ya kuifahamu kweli imekuweka huru?
  .
   
 15. m

  mwananyiha JF-Expert Member

  #15
  Mar 31, 2011
  Joined: Mar 11, 2008
  Messages: 244
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Ukweli unajulikana kwamba dawa inaponya na haina madhala.
   
 16. CAMARADERIE

  CAMARADERIE JF-Expert Member

  #16
  Mar 31, 2011
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 4,427
  Likes Received: 158
  Trophy Points: 160
  Kwani Shekhe wetu hutabiri bure?

  [​IMG]
   
 17. O

  Oldarasu Member

  #17
  Mar 31, 2011
  Joined: Dec 22, 2010
  Messages: 45
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Judith naamini hujambo! What is wrong if ELCT builds a better place for people who are coming to get cured of deadly diseases? Are you angry because of that? Or you just don't like the idea that people are getting healed? I am surprised! If you are one of those who are against what God is doing in Samunge then you still have a long way to go because God isn't done yet with His precious people. If what I am saying about your attitude is not true then perhaps you are speaking, thinking and writing out of total ignorance! If this is true then you need to take time to learn and think before you start a topic.

  Any ministry has to be supported by people of good will, and what Pastor Masapila is doing there deserves to be supported because he is doing what God commanded him to do and if you don't believe what God is doing there it is better to keep quiet as it is wiser than opposing you really don't know. Keep in mind that God uses people as he pleases and according to His own will. He also uses weak people and things to ashame the great! So I would advice you to keep silence or at least pray if you doubt that what Pastor Masapila is doing is not from God. Many people have been healed from different ailments and to me healing cannot be Satan's work. It is God's work and healing is one of Jesus' works He came to do according to Isaiah 53. Building a place for the purpose of administering God's people is the right and noblest thing the church (the body of Christ) can do.

  If you do not believe in what Pastor Masapila is doing you still have a long way to go. You will have to wrestle with the testimonies of those who got healed by God through the ministry of pastor Masapila. Let me remind you a story of a man who was born blind in John 9 who suffered the ridicule and the questioning of the Pharisees. God read that story of this man and you will see that neither the Pharisees nor any one can refute or render false what God does. At the end the blind man said call Him whatever but what I know is this: "If He's a sinner I don't know. What I know is that I was blind but now I see." Dear Judith, God is not limited by geographical boundaries or denominational lines. He's a God of all mankind and He uses anyone from any where to accomplish His purposes for the glory of His holy name.

  May God the Father of our Lord Jesus Christ the Wounded Healer enlighten you so that you may know the truth about His will. Jesus told His disciples who came with a complaint about a man who was casting out demons in His name and Jesus' answered them and I am parahrasing what He said, "If anyone is not against us he is for us" (Read Mark 9:38). What side are you Judith?
   
 18. Ms Judith

  Ms Judith JF-Expert Member

  #18
  Mar 31, 2011
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 2,569
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  ibada ya kikombe ni ibada ya sanamu. hata wanaoziabudu sanamu hawasemi kuwa wanaiabudu ile sanamu, bali husema wanamuabudu Mungu aliye ndani ya ile sanamu!

  zinduka ndugu yangu, Mungu wetu hawezi kuwemo kwenye kikombe, Mungu wetu anakaa mioyoni mwetu.

  Bwana kwetu sisi ni kimbilio na nguvu, ni msaada utakaoonekana tele hata wakati wa mateso. kikombe hakiwezi kuwa kimbilio na nguvu yetu kama vile sanamu isivyoweza kuwa kimbilio na nguvu yetu. mtu yoyote akimbiliaye kikombe wakati wa mateso (kama hayo ya maradhi) anashiriki ibada ya sanamu. hana tofauti na yule aipigiaye magoti sanamu na kuiabudu. mkiijua kweli, hiyo itawaweka huru. mbarikiwe sana

  sisi hatutaogopa ijapoharibika nchi
  na kutetemeka milima moyoni mwa bahari
  na tutakapomaliza vita hivi kwa ushindi wa Mwana Kondoo tutapewa kula matunda katika ule mti wa uzima
   
 19. Michelle

  Michelle JF-Expert Member

  #19
  Mar 31, 2011
  Joined: Nov 16, 2010
  Messages: 7,364
  Likes Received: 194
  Trophy Points: 160
  huna jipya...tafuta jingine Judith....usitake ku influence watu kwa unachoamini wewe.....acha kila mtu aamue anachofikiri ni sahihi...aliokuambia watu wanafata kikombe ni nani?watu wana imani kupitia Yesu Kristo wanapona kwa kunywa dawa iliyowekwa kwenye kikombe na kuombewa na Babu....kila siku unakuja na hila zako hapa....useless!!!:bored::bored::bored::tape:
   
 20. m

  mwananyiha JF-Expert Member

  #20
  Mar 31, 2011
  Joined: Mar 11, 2008
  Messages: 244
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Oldarasu amefafanua kwa urefu lakini huelewi. Kumbuka nyoka wa shaba,matope......
   
Loading...