KKKT Mna tamaa sana na hela , ona waliyoyafanya na Mzee Mengi

Kuzikwa machame hiyo ni lazima hawezi kuzikwa porini Dar es salam ,lazima akazikwe nyumbani eneo lililotengwa kwa ajili ya makaburi.

Wanawe wanaweza wakawa naye ila sasa kutakuwa na distance kubwa sana kati yake na ukoo wa akina Mengi pia na watoto wa Mke mkubwa .

Watoto wake hao ndo ponea ponea yake .

Na hawa ndugu zangu nawafamu sana .Kikukweli atapata tabu sana

Pia akiweka ngumu na yeye atakuwa amewatengenezea watoto distance na ukoo na ndugu wengine wengine ,,

Familia haitakubali kumuachia mali zote za Mzee yeye ndo awe msimamizi Mkuu, na sidhani kama ataweza kwenda mahakamani kudai haki ya kuwa msimamizi mkuu wa Mali alizochuma Mzee ,
Halaf Kuna kijana alisimamishwa Kama msimamiz was Mali baada ya mzee kuchoka so inabidi ajiongeze sana mlimbwende wetu
 
MENGI & KKKT DAYOSISI YA KASKAZINI MMEKOSEA
Juzi baada ya mke halali wa Reginald Mengi Mama Mercy Anna Mengi kufariki dunia huko Johannesburg Afrika Kusini, vyombo vyake vya habari hususani ITV Tanzania na Eatv Tanzania vimetumia nguvu kubwa kuficha ukweli halisi wa nafasi ya mama huyu kwenye ndoa yake takatifu ya Kikristo (KKKT). Huku vikijikita kumuelezea tu kama mmoja wa waanzilishi wa makampuni ya IPP.

Binafsi silaumu vyombo hivyo kuuficha UKWELI huu MCHUNGU kwa kuwa pengine wangependa kueleza uhusika wa mama huyu lakini hayo ndio maagizo waliyopewa kutoka juu. Wangefanyaje ikiwa nao wanatafuta unga wa watoto wao, wakiuke wafukuzwe?

Hapa ambaye nataka nimlaumu peupe ni Reginald Mengi kwa kumkosea heshima mkewe. Fedha na mali vitapita lakini kumkosea heshima na utu kwa mwanamke anayejua mlipotoka, akakuzalia hadi watoto ni jambo ovu na baya la kukemewa katika jamii yetu. Kulikuwa kuna ubaya gani kumtambua Mama Mercy Anna kama mkeo halali?

Wa pili wa kulaumiwa zaidi ni KKKT hususani Dayosisi zinazopatikana kanda ya yetu ya Kaskazini ELCT Northern Diocese (sina uzoefu na dayosisi za KKKT kutoka kanda nyingine). Kanisa hili niseme ukweli limekuwa na "desturi ya kushindwa kukemea vitendo viovu kwa waamini wake wenye ukwasi na fedha lufufu".

Tukio hili si la kwanza kutokea, miongoni mwa tukio ambalo lilishangaza wengi ni wakati mmoja wa mke wa Mremi (Dar Express) alipofariki. Waamini wa KKKT walingoja kuona namna ambavyo ile Sheria ya KKKT ya kuwatenga watu na kuwasulubu wakati wamekufa kwa sababu wako nyuma ya kundi ifanye kazi. Japokuwa wengi tulitarajia kuwa Sheria hii isingeweza kufua dafu kwa bwenyenye hili.

Nilisikitika sana kuona double standards katika utekelezaji wa Sheria za Kanisa pale ambapo Askofu alingojwa hadi atoke Marekani ili aje amzike mke wa Dar express kwa heshima zote.

Kuhusu Pombe wala usijiulize, KKKT imepoteza uwezo wa kukemea vileo kwa waamini wake matajiri. Pale kwa Dar express walikunywa kwa kiwango cha kusaza kuanzia migombani mpaka nje. Sikusikia popote kukilaumiwa kwa mambo haya ambayo kwa mujibu wa Sheria za KKKT ni makosa.

Lakini ukitaka kuona meno na utekelezaji wa Sheria hizi, jambo sawa na hili au hata huenda dogo zaidi liwe limetendwa na waamini masikini, mafukara na wale wa kipato cha kati ambao hawana ushawishi kwa Viongozi wa Kanisa hapo utaona Sheria, kanuni na taratibu hizi jinsi zitakavyosimamiwa. My friend watakutupa kaburini kama mbwa koko.

Nimeshashuhudia na kuhudhuria mazishi ya watu masikini wanaosulubiwa vikali na Sheria hizi kanda ya Kaskazini. Watahakikisha hata wimbo au sala hazifanyiki, wanahukumu Marehemu bila kujijua. Ukiwauliza majibu yao ni mepesi tu, watakujibu "iwe funzo kwa wengine".

Akifa masikini zitauliziwa documents zake zote zije, ole moja ya documents ikosekane. Lakini wacha afe bwenyenye ambaye ni mtoaji mzuri wa michango mbali mbali utasikia huyu hana neno tunamfahamu.

Hata kama wanafahamu fika kuwa Marehemu alikuwa mtoa kafara, anayedhulumu mali, mwizi, ameoa wake wawili achilia mbali masurufu yake. Hayo hutoyasikia.

Baadhi ya waamini wa KKKT ukanda huu wa Kaskazini huwa wanalazimika kufuata Sheria hizi za kile kinachoitwa " matoleo" mara utasikia sadaka ya ahadi, collect, misioni, mchango wa mradi wa hoteli ya Corridor ulioliwa na Viongozi wa Kanisa, shukurani ya ndoa, ubatizo nk. Na lazima utoe ndipo upewe huduma hizi haijalishi una uwezo au la.

Sehemu nyingine wamefika hatua ngumu kidogo, unakuta wale "single mother" kajaaliwa Mtoto wake anataka abatizwe, wanamkomalia kuwa hawambatizi Mtoto hadi mama yake afunge ndoa. Hivi kama hana mume aje afunge ndoa na nani? Au Kanisa linataka wasiobahatika kuolewa wafe bila watoto?

Hata kutembelewa na kushirikishwa habari za kiroho kama ilivyo desturi ya Kanisa kama wewe huna kitu kusema UKWELI MCHUNGU huwa ni nadra na ngumu mno. Lakini bwenyenye likituma SMS tu mara hiyo hiyo utakuta Mchungaji, Mwinjilisti, na Mzee wa Kanisa wamefika haraka sana.

Binafsi siamini kama haya ndiyo matengenezo ya Kanisa (Church Reformation) aliyoyamaanisha Padri Dr. Martin Luther wa Ujerumani kabla ya kuasi kutoka Kanisa la Roma.

Macho na masikio yangu yote nayaelekeza KKKT Dayosisi ya Mashariki na Pwani (DMP) pale Usharika wa Azania Front November 8 kuona kwamba, Je Askofu Dr G. Malasusa ataweza kuvunja mwiko huu wa wenzake wa Kaskazin na kumkemea Mengi? Je atasimama imara na kuhubiri hii DHAMBI ya kumtelekeza huyu mama? Au naye ataweka Sheria pembeni kwa muda? Kwa upande wa Dayosisi ya Kaskazini na dayosisi zingine zote za Kaskazini wala sina mashaka kuwa ukiwa na pesa haijalishi ulikuwa unafanya nini kila kitu kiko sawa.

Kwa kule Machame Moshi najua huenda hata Askofu anaweza asitaje kama huyu mama anayezikwa ni mke halali wa Mengi. Anyway tungoje November 10.

Kanisa hili lisipojitafakari litaendelea kuwa kisima cha migogoro ambayo ukiifanyia analysis sana utaona kuwa chanzo chake kikuu ni FEDHA.

Bwana Alitoa na Bwana Ametwaa Jina la Bwana Lihimidiwe.

Mungu aipumzishe Roho ya mke wa Reginald Mengi, Mama Mercy Anna Mengi mahala pema peponi. Amina.

Tujikumbushe na hapa

Askofu Shoo, KKKT ina mapungufu mengi irekebishe kwanza kabla ya kukimbilia siasa - JamiiForums
Britannica

Mtu huchangii chochote kanisani kwa kuwa huna hela halafu masharti ya kawaida ya bure ambayo hutoi hela nayo huwezi kuyatimiza, HUFAI NAKUTENGA KABISA. UNAFAIDA GANI MUNGU KUKULETA DUNIANI HAPA??
 
Mengi Ana ndoa moja tu hyo na klyn ni batili maandiko yanasema usimwache mke wa ujana wako. Hafu wanaume wakifiwaga na wake nao mda si mrefu hufatia wapendwa wao
Hapo kwenye bold hapooo
 
Anao watoto so asije waumiza kwa kukataa kabisa kpata urithi. Na kimsingi wanae ndio watakao rithi
 
Tifauti ya Jacline na Nandy ni moja tu,mmoja ni mjane mwenye watoto na mwingine ni mjane asiye na mtoto
 
Swali ni JE KANISA LITAMZIKA??? likimzika na ilihali dunia nzima inajua alikuwa anaishi maisha ya UZINZI hapo ndo nitahama rasmi KKKT watakuwa wamejivua nguo rasmi. Na hizi sheria sheria zao kwa MASIKINI ni UONEVU tu.
 
Kuna kitu nyuma ya pazia mahusiano ya marehemu Reginald na Mercy kumbukeni Nelson na Win Mandela
 
Kanisa katoliki liligoma kumzika yule tajiri wa Arusha mmiliki wa ngurudoto watu walilalamika sna ikawa hivyo
 
Kanisa lisimamie sheria zake mm naamini katika bible izi dini ni kelele za watu wachache
 
Ni lazima wamzike Mengi hajawahi kuwa na Tatizo na kabisa lake.
Alikua muumini Mzuri sana.

Matatizo yake ya kifamilia hayahusiani na Umoja wake ndani ya kanisa na ushiriki wake katika shughuli zote za kikanisa.
Hata Pombe ni haramu kulingana na mafundisho ya kanisa lakini walevi wanazikwa.

Pa ndani ya makanisa karibu yote kuna madhambi makubwa sana ukilinganisha na Mgogoro wa Mengi na mke wake uliopelekea kuoa mtoto mdogo ambaye naye ameibua mgogoro tena. Alifanya vyema kuutangazia ulimwengu kuwa amemuaoa tofauti na mamilioni ya waumini wanaofanya uzinzi na vimada na nyumba ndogo kila kona.

Chuki, fitina,woga, ushirikina ,ulafi,ulevi, zinaa , ulawiti,kuiba kura, kuua, utekaji, rushwa , kuabudu sanamu, kumkataa Masihi Yesu na mitume na manabii, ubaguzi,upendeleo, Hasira , uongo, matusi n.k yote ni dhambi.

Asiye na mojawapo kati ya madhambi hayo hapo juu awe wa kwanza kuacha kwenda kumzika Muumini mwenzake.
 
KKKT ina tatizo na marehemu Mengi baada ya kuachana na marehemu mkewe na kuoa tena. Marehemu alikuwa ametengwa na KKKT...hakupata kurudishwa kundini.
 
Back
Top Bottom