kmbwembwe
JF-Expert Member
- Aug 16, 2012
- 10,408
- 7,190
Wakati Taifa lina lengo la kuimarisha matumizi ya lugha yetu kwenye nyanja zote ikiwa ni pamoja na elimu wapinzani wa taifa kujikomboa kwenye ukoloni wa lugha na utamaduni wa kigeni wanajibu mapigo kupitia makanisa.
Kama muomini wa KKKT Mbezi Beach sioni mahitaji na ungezeko la ibada na mafunzo ya sunday school kwa Kiingereza.
Ilianza kidogo kwa misa chache sasa kila Jumapili na kwa sikukuu ya chrismas na mwaka mpya. Naona kuna wazee wa usharika wamejaa kasumba ya Kiulaya, binafsi sipendelei jambo hili.
Nina hakika mahitaji ya misa kwa Kiingereza ni madogo sana au hakuna kwa hiyo viongozi wasitulazishe kukosa misa ya pili saa 4.00 asubuhi kwa Kiswahili eti inageuzwa ya Kiingereza.
Ingekua jambo la maana kanisa kuanzisha darasa la lugha ya kiswahili kwa hao waomini wachache badala ya kuwawekea ibada muda muafaka kwa waomini wengi.
Kama ndio usomi mwenyewe ni msomi ngazi ya uzamili ila sipendi kulimbukia utamaduni wa watu wengine.