KKKT Mbezi Beach msilazimishe waumini kuabudu kwa Kiingereza

Je! Kuna Jamii au watu especially mataifa ya nje wanaozungumza kingereza??? Kama hakuna huo ni ushamba...
Kuna wageni wengi Mbezi. Wamama zaidi ya watatu ninao wafahamu wamepata ndoa za ukubwani na Wamarekani weusi.

Hawa wababa walikua wanajeshi na wamestaafu. Jeshi la Marekani unastaafu baada ya kutumikia miaka 16. Wengi wao wako kwenye 40’s na wana pension ya uhakika wameamua kumalizia maisha yao Afrika.
 
Sababu ya kutumia lugha ya kingereza kwa watoto ni kwamba asilimia 98 ya watoto wa sunday school mbezi beach wanasoma shule za english medium au international school na walimu wanapata ugumu kuwafundisha kwa kiswahili

Na hata mafunzo ya kipaimara wameweka option ya english na kiswahili, mtoto anachagua anachoweza
Kwa hiyo watoto wa mbezi beach hawajui kiswahili na wazazi ambao ni watanzania mnaona fahari watoto wenu hawajui kiswahili? 😂😂
 
Nasikia ibada za lugha ya malkia zinakua fupi fupi..kwenye mahubiri hakuna zile longo longo za mifano ya uongo na ukweli
 
Ni kwa sababu ya mazoea. Hakuna waraka, kwa mfano, unaosema kuwa usitumie kiingereza katika mawasiliano ya kiserikali. Kwa mfano, mikataba karibu yote ya ujenzi iko kwa kiingereza hata ile ya kujenga matundu ya vyoo.

Lakini kwa vile jamii yetu wengi ni kama wewe basi tunaona ni rahisi zaidi kutumia kiswahili na kama unataka kuwasiliana na watanzania wengi, kiswahili ni lugha ambayo inaeleweka na wengi.

Tulikosea wenyewe kutokukijenga kiswahili ili kiweze kutumika katika mazingira yote, hasa katika elimu kuanzia msingi mpaka Ph.D. Hatukufanya hivyo na sasa kuna pengo kubwa sana katika uelewa wa lugha zote mbili. Walimu wa sekondari wanafundisha Kiingereza na masomo mengine kwa kiswahili pamoja na kuwa vitabu vyake vimeandikwa kwa kiswahili. Ndio maana wenye uwezo wanafanya kila jitihada ili watoto wao wamudu kiingereza kwa ufasaha. Kusoma Sunday School kwa kiingereza na kuhudhuria ibada kwa kiingereza ni sehemu ya juhudi hizo.

Amandla....
 
Bwashee sali misa ya kwanza.

Binafsi naona wamechelewa sana kuanzisha hii misa ya kiinglishi.

Kanisani kwetu pale Anglican St Alban Huduma kwa lugha ya malkia ina zaidi ya miaka 100 sasa.........Ni misa ya pili.
Ya kwanza na ya tatu ni za kiswahili!
Unajua anglican ni church of england. Hii kitu sio mchezo tunabishana tu ila bado tunahitaji ukombozi kifikra. Lugha na utamaduni ni njia imefanikiwa sana kwa sisi waafrika kuendelea kutawaliwa kifikra. Ukitawaliwa kama taifa lazima ubakie maskini.
 
Sababu ya kutumia lugha ya kingereza kwa watoto ni kwamba asilimia 98 ya watoto wa sunday school mbezi beach wanasoma shule za english medium au international school na walimu wanapata ugumu kuwafundisha kwa kiswahili

Na hata mafunzo ya kipaimara wameweka option ya english na kiswahili, mtoto anachagua anachoweza

Kama mtoto anaweza chagua anachotaka mtu mzima kinamshinda nn kuchagua sehemu ya kupata huduma anayotaka.

Waache watu waishi maisha yao wanayopenda as far hawavunji sheria za nchi!
 
Ibada ya kingereza kkt mbezi beach ni once a month, na ni option sio unalazimishwa, binafsi mimi na watoto wangu tunasali engkish service na first born wangu mafundisho ameopt english kwa sababu ndio lugha amekua akiitumia shule na tuliona kiswahili kitasumbua

Cha mshingi wewe chagua ibada unayoimudu, kama ni kiswagili au kingereza
Tena wakazie iwe kila week maana ni muhimu
 
Makanisa wajenge mabeberu wewe ukatae misa za kizungu hebu acha ungese
 
Kama mtoto anaweza chagua anachotaka mtu mzima kinamshinda nn kuchagua sehemu ya kupata huduma anayotaka.

Waache watu waishi maisha yao wanayopenda as far hawavunji sheria za nchi!
Nashangaa sana awamu hii mtu anataka upangiwe hadi ibada ya kusali kisa wanataka kukuza kiswahili

Watu wawe huru lufanya wanachotaka na wanachoweza
 
Kwa hiyo watoto wa mbezi beach hawajui kiswahili na wazazi ambao ni watanzania mnaona fahari watoto wenu hawajui kiswahili?
Wanajua kiswahili, binafsi wa kwangu anajua kiswahili lakini kinamsumbua, kumbuka shuleni since grade one anasoma masomo yote kwa.lugha ya kingereza, anapofika grade 3 ndio anaanza kusoma somo moja la kiswahili, unadhani hapo ni lugha gani atakua ameimaster sana kati ya english na kiswahili? Dunia imebadilika na maisha yamebadilika, ni lazima wazazi pia tujifunze kuadapt ulimwengu uliopo la sivyo watoto wetu watabaki nyuma
 
Wameshajua wapo wengi na vidigrii vyao kimoja Viwili na miziki wanapenda kusikiliza vinyimbo vya English.
Anakuwa na usafiri Wa below 15M na three bedrooms house ama akapanga na apartment ,akakamatwa na 9/5 jobs. Anapeleka Hela samaki samaki na watoto wakali lazima ahudhurie ya English apige selfie apost kuwa anasali kwa English.
Salary figures hizo 6 ama saba lazima wachungaji wasome upepo namna ya kugawana nao.
Ukitaka kula Hela ya mlevi nawewe sharti uelewe jamani.

Yaani hao jamaa Wa dini wamefaulu saikolojia jamani Yaani hao jamaa waogopeni wanatumia weakness ya MTU kumchota akili.

Yaani hao jamaa wao wakitaka Gari wanachangiwa ila Muumini yeye akiwa na hitaji Fulani anaombewa haujiulizi walivyo na akili jamani.
Wewe umepanga banda LA kuku kama mie yeye ana usafiri Wa Mana sio kama nyie Wa pàso. Watoto wao shule zao ni sauzi Africa afu Mie Wa kwangu ya bure saint kayumba.

Take care yourself
 
Kama Msomi, usomi wako ungekuelewesha kuwa Utamaduni ni Very very dynamic, na kwa kweli English, Wala sio umarekani au uingereza, Bali utamaduni wa dunia utalalia English, kinyonge wasiopenda wataingia tu. Nakuambia, easy your mind.
Smartphone zimeshafanya yao, English imekuwa rahisi hata kwa wasioenda Darasani
 
Kuna misa ya kiswahili na kiingereza. Muumini unachagua inayokufaa. Na tukumbuke kuwa Tanzania hatuishi watanzania peke yetu, tuna wageni ambao wangependelea zaidi misa ya Kiingereza.

Na kwa vile makanisa yako mengi, mtu akiona anakwazika kwa sababu muda walioamua kuwa na misa ya kiingereza ndio muda ambao angependa kusali basi anaweza kuhamia kanisa lingine la dhehebu hilo hilo ambalo halina misa za kiingereza.

Naamini viongozi wa kanisa hili wameona kuna waumini ambao wangependa kuabudu kwa lugha hiyo. Nao kama wachungaji wa Bwana hawawezi kuachia kondoo wao wapotee kwa kitu ambacho ambacho kiko ndani ya uwezo wao.

Amandla...

Huyu jamaa ana lake jambo,,bahati nzuri leo Upendo Tv walikuwa wanarusha 'Live' ibada ya saa1 asubuhi kutoka Usharika wa Mbezi Beach(KKKT) katika matangazo waliweka bayana kuwa Ibada za saa 1 na saa 4 asubuhi ni za Kiswahili na ya saa 8 alasiri ni ya Kiingereza.Sasa kama 'No English' nenda za Kiswahili
Ugonjwa wa kunung'unika kama sio kulalamika unawatafuna vijana wengi sana wa Kitanzania, yaani kuna fursa ya kuhudhuria ibada inayoendana na mtu lakini bado anakuja JF kulalamika badala ya kwenda moja kwa moja kwenye usharika wake kutoa mapendekezo. Bahati nzuri makanisa yote huwa yanaweka ratiba ya ibada zote na ni kiasi tu cha kuji-adjust kulingana na mahitaji ya lugha yako.

Lakini pia ibada ya kiingereza pia hata kama wanaozungumza hiyo lugha ni wachache bado unaweza ukaitumia kama sehemu ya ku-practice lugha ya english kwa sie wa St. Kayumba maana dunia ni kijiji kuna kesho na keshokutwa umeenda nchi za watu angalau unazoea taratibu za ibada kwa lugha ya kigeni hata kama una umahiri wa hiyo lugha
 
Back
Top Bottom