KKKT Mbezi Beach msilazimishe waumini kuabudu kwa Kiingereza

Kwa mbezi beach ni sawa kule wakishua wengi na wageni wengi.kuna kitu wamekiona.huo mpango hawawezi kuuleta huku buza kwa mpalange
 
Je! Kuna Jamii au watu especially mataifa ya nje wanaozungumza kingereza??? Kama hakuna huo ni ushamba...

Mfano Catholic...Dar
1.St Peters ipo Englisha mass kwakuwa upande wa. Masaki na Obay kuna Balozi nyingi....hivyo kuna ulazima wa English service

2. St Immaculate Upanga....Ipo English mass Kwakuwa upande ule ni balozi za UN..hivyo community inayohitaji Kingereza ni kubwa...

3. St Joseph Metropolitan Cathedral....ipo English mass kwasababu mjini kuna jamii kubwa ya Wahindi hasa Wagoa hivyo uhitaji wa misa ya Kingereza ni mkubwa...

Sasa huo usharika wa mbezi Beach kuna huo uhitaji wa namna hiyo????? Au ndio ubishoo....mass must be Patispatory....
 
Huyu jamaa ana lake jambo,,bahati nzuri leo Upendo Tv walikuwa wanarusha 'Live' ibada ya saa1 asubuhi kutoka Usharika wa Mbezi Beach(KKKT) katika matangazo waliweka bayana kuwa Ibada za saa 1 na saa 4 asubuhi ni za Kiswahili na ya saa 8 alasiri ni ya Kiingereza.Sasa kama 'No English' nenda za Kiswahili
 
Leo wana Jf wengi mmekumbuka kwenda kanisani!!

naona mnalalamika kila kona

Uzi wa tatu huu.
Wametuwakilisha na sisi, mimi nimeipenda hii. Tuwatie moyo wenzetu hawa ili katika sala na maombi yao waiombee na JF dhidi ya wote wenye husda na kijicho.
 
Sasa makabwela watasali Wapi!
Duh! Hahaa sijajua makabwela umemaanisha nini?

Sijajua kwa Mbezi beach ila Azania front kuna option ya ibada ya kiswahili hii ya kiingereza ina muda wake tofauti kabisa na ibada ya kiswahili.
 
Kuna baadhi ya makanisa misa ya kwanza inakuwa na waumini wengi kuliko ya saa nne. Watu wengi wanapenda wawahi ili wawe na siku nzima ya kufanya mambo ya kidunia. Inawezekana hili nalo liliangaliwa.

Amandla...
 
Ila kama umekwazika sana na wewe ni muumini mzuri hapo kanisani ungeanza kwa kuangalia kama mko wengi wenye mtazamo kama wa kwako. Mkiwa wengi wa kutosha ndio mnaweza kuongea na uongozi wa Kanisa ili hili suala lipatiwe solution. Hapa JF utapata michango ya mawazo lakini ukweli ni kuwa hayana uwezo wa kubadilisha mfumo wenu wa ibada.

Amandla...
 
Wakati taifa lina lengo la kuimarisha matumizi ya lugha yetu kwenye nyanja zote ikiwa ni pamoja na elimu wapinzani wa taifa kujikomboa kwenye ukoloni wa lugha na utamaduni wa kigeni wanajibu mapigo kupitia makanisa...
Ibada ya kingereza kkt mbezi beach ni once a month, na ni option sio unalazimishwa, binafsi mimi na watoto wangu tunasali engkish service na first born wangu mafundisho ameopt english kwa sababu ndio lugha amekua akiitumia shule na tuliona kiswahili kitasumbua

Cha mshingi wewe chagua ibada unayoimudu, kama ni kiswagili au kingereza
 
Kuna misa ya kiswahili na kiingereza. Muumini unachagua inayokufaa. Na tukumbuke kuwa Tanzania hatuishi watanzania peke yetu, tuna wageni ambao wangependelea zaidi misa ya Kiingereza...
Huyu jamaa mleta mada sina uhakika kama ni msharika mwenzetu, maana amekuja na lawama wakati englidh service ni option kwa wale wanaomudu na sio lazima
 
Nikuulize wanao wapo st kayumba au shule zinafundisha kiingilishi,

Kama ni zinazofundisha kiinglishi basi huna hoja!! Endelea kuabudu au hama kanisa!
Sababu ya kutumia lugha ya kingereza kwa watoto ni kwamba asilimia 98 ya watoto wa sunday school mbezi beach wanasoma shule za english medium au international school na walimu wanapata ugumu kuwafundisha kwa kiswahili

Na hata mafunzo ya kipaimara wameweka option ya english na kiswahili, mtoto anachagua anachoweza
 
Umejibu vizuri sana. Naongezea tu kuwa Kiingereza ni lugha ya taifa kama kiswahili. Ndio maana sheria zinaandikwa kwa lugha zote mbili.

Walla hujui lugha ya taifa ni kiswahili. Lugha rasmi nchini ndio kiswahili na kingereza na serikalini shughuli zote kinatumika kiswahili.
 
Back
Top Bottom